Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini umeratibu zoezi la kurejeshwa nyumbani kwa raia wa Tanzania waliokuwa nchini humo, kwa kushirikiana na mamlaka za Afrika Kusini kuhakikisha taratibu zote za safari zinakamilika kwa mujibu wa sheria.
Akisimamia zoezi hilo Julai 24, 2026, Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, James Bwana, amesema maandalizi yamefanyika kwa ushirikiano na maafisa wa Idara ya Mambo ya Ndani ya Afrika Kusini, ambapo wananchi hao wamesafirishwa kwa mabasi kuelekea viwanja vya ndege na vituo vingine vya usafiri kwa ajili ya kurejea Tanzania.
Baadhi ya Watanzania hao wameeleza kufurahishwa na hatua ya Serikali kupitia Ubalozi kuwasaidia kurejea nyumbani, wakisema ushirikiano huo umewezesha safari yao kufanyika kwa usalama na utaratibu.
Soma: