Watanzania hatutajikomboa kutoka kwa watesi wetu bila Katiba nzuri

Watanzania hatutajikomboa kutoka kwa watesi wetu bila Katiba nzuri

nashicha

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2021
Posts
279
Reaction score
524
Pongezi sana kwa Mbowe lakini watanzania hatujafanya yanayotupasa

Nchi ili ikamikishe maendeleo lazima ipitie kwenye hatua chungu na za wakati mgumu kwa baadhi ya wapigania haki kupata mateso makali ya kudhulumiwa haki na hata kupoteza mali au maisha yao hasa wakati taifa likipitia katika kipindi cha udikteta maana huo sio ukoloni ni watu wenye nchi kuwaumiza wenyenchi wenzao kwa ajili ya maslahi yao

Huu wakati ni mgumu sana maana watesi wanawajua na kuishi na wanaowatesa. Sisi kama taifa naona hatujafanya litupasalo kufanya ili kujikomboa dhidi ya watesi kenya majirani zetu walipitia hali ngumu sana wakati wa mzee Kenyatta na Moi. Hawa walikuwa ndio Katiba na ndio Serikali wakisema wao ukijibu umepotezwa walipogundua watesi wao wanatumia udhaifu wa katiba wakaamua 2010 kufa au kupona na walikufa wengi lakini leo hii hakuna nchi yenye uhuru na katiba nzuri kama kenya hata watesi wao wanapotaka kutumia ukabila kurudisha nyuma bado katiba inawabana mbavu tanzania tuamke hakuna uhuru wa fikra mawazo na kutembea bila kuutafuta kwa nguvu watesi huwa hawautakagi huo uhuru maana kwa mpaka wanapokuja uraiani ndio katiba inakuwa muhimu kwao
 
Katiba bora ni nafuu kwa kila mtanzania bila kujali vyama na siasa zao.
 
Mwambie kwanza aliekutuma kuandika huu ujinga akufunze na kuandika. Haya subiri bando lako kutoka kwa wachumia tumbo wenzako.
 
Mwambie kwanza aliekutuma kuandika huu ujinga akufunze na kuandika. Haya subiri bando lako kutoka kwa wachumia tumbo wenzako.
Wachumia tumbo mkisikia habari za KATIBA sukari inapanda yale mapambio mliyokuwa mnamwimbia dikteta kamfuateni muendelee kuimba mmesahau alisema atakuwa KIRANJA MBINGUNI
 
Wachumia tumbo mkisikia habari za KATIBA sukari inapanda yale mapambio mliyokuwa mnamwimbia dikteta kamfuateni muendelee kuimba mmesahau alisema atakuwa KIRANJA MBINGUNI
Mkuu aliekutuma kuandika uzi huu ki ukweli kakuingiza chaka. Si unaona wanaharakati uchwara wameususa uzi wako. Wenzio mpaka kuandika uzi hapa juwa wanakuwa tayari washalipwa na pia ni watu wanaofahamika na chama japo wanatumia ID fake ila viongozi wao wanaowatuma wanawajua vizuri. Sasa ww umeingia kichwa kichwa bila malipo wala kujulikana matokeo yake ndo hivi uzi umesuswa na malipo ya uchafu wako ulioandika haupati. Pole sana kijana!
 
Mkuu aliekutuma kuandika uzi huu ki ukweli kakuingiza chaka. Si unaona wanaharakati uchwara wameususa uzi wako. Wenzio mpaka kuandika uzi hapa jua wanakuwa tayari washalipwa na pia ni watu wanaofahamika na chama japo wanatumia ID fake ila viongozi wao wanaowatuma wanawajua vizuri. Sasa ww umeingia kichwa kichwa bila malipo wala kujulikana matokeo yake ndo hivi uzi umesuswa na malipo ya uchafu wako ulioandika haupati. Pole sana kijana!
Wewe umelipwa sh ngapi kujibu uzi wangu acha kazi iendelee
 
Back
Top Bottom