Watanzania hawaeleweki, wanadai hawamtaki Rais, akiondoka wanatamani arudi

Johnny Sack

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2017
Posts
9,504
Reaction score
20,293
Watanzania sasa hivi wamechachamaa hawamtaki Samia, kelele kibao mtandaoni

Lakini ukitazama kwa umakini, Watanzania hii imekuwa ndio tabia yao, wanasema hawamtaki kiongozi ila akindoka wanatamani arudi

Tuliona Kikwete walikuwa wanapiga sana kelele hawamtaki, ila alipoondoka na kuja Magufuli, Mwanzoni walimshangilia sana JPM, lakini baada ya miaka 2 Watanzania wengi wakaanza kusema Kikwete alikuwa afadhadhali, vyuma vimekaza, watu wanatekwa na demokrasia na Uhuru kupotea

Magufuli alivyokufa watu wengi wakashangilia, Mama akaingia, wakampenda sana, Jinsi watoto walivyokuwa na hasira na Magufuli, waliposikia mtu anamkosoa Samia tu wakampachika jina la Sukuma Gang, kauli ya "MAMA ANAUPIGA MWINGI" ikatamalaki

Miaka 4 baadae Samia hawamtaki tena, wanasema amekuwa analea mafisadi, ameuza rasilimali za nchi, na amekuwa anateka na kuua watu kuliko hata mtangulizi wake, Uhuru umepotea. Sasa hivi wanasema bora Magufuli, hata wale Sukuma Gang sasa hivi hawazomewi tena, wanapendwa

So kila Rais hafai ni bora aliyepit Huyu nae akiondoka atakuwa bora huyu 😁😁
 
kwa sensa/data ipi ya conclusion hiyo
 
Hakuna raisi ambae atakubalika 100%, duniani kote, lakini katika historia ya hii nchi huyu ametokea kutokukubalika kuliko rais yeyote, toka uhuru wa hili taifa, na huo ndio ukweli...
Magufuli nae walisema hivi hivi mkuu...Rais mbovu kukiko wote
 
Una macho lakini huoni, una masikio lakini husikii,
The statement "No research, no right to speculate" emphasizes the importance of grounding one's claims in evidence and research before making speculative statements. While speculation can be a starting point for inquiry, it should not be presented as factual without proper support
 
Wakwepa kodi, mafisadi na wazee wa posho ndio walikua wanamchukia Magufuli; sijui sababu gani hasa ilimfanya Magufuli avuruge uchaguzi wa 2020, Magufuli hata asingepiga kampeni, wananchi wa kawaida walikua wanampigia kura za ndio. Maadamu Humphrey Polepole yupo hai, anaweza kutwambia why waliamua kuuvuruga ule uchaguzi. Kwa wale waliokuwepo uchaguzi wa mwaka 1995, Mkapa alipita kwa shida sana lakini mwaka 2000 Mkapa alipiga kampeni kirahisi sana, hakua na mpinzani kwa kweli, hata uchaguzi wa 2005 uliomleta JK nao ulikua rahisi mno kwasababu ya kazi alioifanya Mr. Ben; kimbembe kilikua 2010 na 2015; ccm "ilishinda" kwa tabu sana kutokana na performance ya aliyeko madarakani.
 
Unadhani kwa hoja hizo Samia anastahili kupendwa au kuchukiwa??

Usichoelewa kwa Magufuli waliokua wanalalamika ni wanasiasa ila raia walimkubali, na kelele mtandaoni zilikua zinashindana wanao.msapoti na Wanao mpinga so akili kumkichwa ukilinganisha na huyu mama
 
Watanzania gani? Weka namba na data za demographics hapa tuchambue kisomi si kwa stories za vijiweni tu.
 
Wewe unacho observe ni kipi?
Kwamba Rais wa sasa hakubaliki au anakubalika au ni 50/50?
Maana kuna chama cha upinzani chenye wafuasi wengi mwanzoni walimpa hadi tuzo, sasa hivi hawataki kumsikia
 

..sawa tu.

..Samia aondoke, tukimhitaji tutamrudisha.
 
Uoga ndo ulimchanganya Magu Naweza kusema ndo Rais bora Magu baada ya Mkapa
 
Miaka 4 baadae Samia hawamtaki tena, wanasema amekuwa analea mafisadi, ameuza rasilimali za nchi, na amekuwa anateka na kuua watu kuliko hata mtangulizi wake, Uhuru umepotea..
Kwa matendo yake hayo uliyoandika hapo, wewe wasemaje unamtaka?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…