Watanzania hawajui sera, mikakati ya Taifa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363

Elvis Mushi.


Asilimia 75 ya Watanzania hawafahamu sera na programu za kitaifa ikiwamo Dira ya Taifa (2025), utafiti wa Twaweza kupitia kampeni ya Sauti za Wananchi, umebaini.

Kadhalika, asilimia 53 ya Watanzania hawafahamu kuhusu Mkukuta (Mpango wa Taifa wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini), wakati asilimia 52 wamesikia kuhusu Kilimo Kwanza lakini hawawezi kuelezea una maana gani.

Akizunguza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mtafiti wa Twaweza, Elvis Mushi, alisema utafiti unaonyesha viwango vya utambuzi na uelewa wa sera kitaifa miongoni mwa wananchi viko chini.

“Mpango wa Kilimo Kwanza unafahamika vema ingawa wananchi hawawezi kuelezea una maana gani na ni asilimia 33 tu wanaweza kuelezea kwa ufasaha,” alisema.

Alisema utafiti umebaini kwamba ni asilimia tano pekee ya Watanzania wanaoweza kuelezea Dira ya Taifa (2025) wakati asilimia saba ndio wanaojua vizuri kuhusu Mkukuta na asilimia 33 wanajua dhana ya Kilimo Kwanza.

Hata hivyo, alisema Watanzania wengi wana kiu ya kupata taarifa kutoka serikalini hususani za huduma muhimu kama elimu, afya, maji na uchumi.

Dira ya Taifa (2025) ni mkakati wa kitaifa unaokusudia kuhakikisha kwamba ifikapo mwaka 2025, Tanzania iwe nchi ya kipato cha kati kwa kuwa na maendeleo makubwa ya watu na kufuta kabisa umasikini uliokithiri na Kilimo Kwanza ni azimio la kitaifa kuleta mapinduzi ya kijani katika kilimo.




CHANZO: NIPASHE

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…