Watanzania hawana adabu kumsema Rais!

falesy

Senior Member
Joined
Mar 15, 2006
Posts
105
Reaction score
17
kwanza napenda niwashukru japo si kwa furaha wanablog hii kwani mnaonekana wenye mtazamo wa kutaka kuleta mapinduzi lakini shabaha ndiyo mbovu.
pili nimpe pole rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania mh. Jakay M. Kikwete kwa juhudi zake z akila siku katika kulipeleka taifa hili kule tunatakiwa japo ni wale tu wenye lensi kamili katika macho yao na ambao kichwani kuna ubongo wanaweza kulion hili.
tatu nimpe pole mzee wangu rafiki Yusufu makamba kwa kuwa sasa amekuwa kama jalala la hata watoto wadogo kumsema watakavyo. nadhani tungetumia uhuru huu kuelez aumma athari za sera kam agenda 50-50 na uzazi wa mpngo ingekuwa bora.
tatu nawapa pole wana blog hii walioigeuza kambi ya kupigia soga za siasa za chadema na kuwa msumari wa moto kwa ccm kwa hapo tumepoteza mwelekeo.
leo nakuja na hoja amabyo nitaitambulisha tu kisha nitaiacha hewani. hivi ni wapi na ni nchi gani ambayo watu wake wana uhuru wa kumsemea lolote mtawala wa nchi. najua ni uhuru lakini uhuru usio na mipaka ni vurugu. leo hii kila mmoja anaamua tu kusema mara hosea, mara mwanyika, mara oooooh fisadi fulani kama tunaishi nchi ya KICHAA iliyo katika tamthilya ya MFALME JUHA. hakuna cha wasomi wala wakulima wote tu tumepoteza maana ya blog hii.
wana blog hii wengi hawana uhakika wa yale wanayoyasema na ndiyo maana wameficha majina yao. nadhani ingekuwa ni vema kama tungejuana kwa majina kamili na kule tunaishi au kufanya kazi badala ya haya mwanakijiji, mpenda nchi na mengine kama hayo.
hakuna haja ya kuwa na watoa maoni ambao wameficha nyuso zao, ni watu wasio na ujasiri, ni sawa na shule ya msingi ambako darasani kuna kijana mkorofi lakini pia ni mbabe na msumbufu darasani, ikifika mwalimu wa zamu anauliza ni nani mkorofi kila mmoja huinama na kutaja jina la yule mkorofi ilimradi tu jina litajike, si una ujasiri wa kutaja? simama watu wakuone sema ni JUMA mkorofi naye akuone ajue hhakika huyu ni shujaa kanitaja.
huu sasa ni ujinga hatuwezi kuendelea kusema Rais hajafanya lolote kwa vile Lipumba kasema, ikiwa kikwete hafai kugombea 2010 basi akigombea msimpe kura msiwe vibaraka wa wale wanaowatumikisha pasipo kujua.
blog hii iliaanza nyakati za uchaguzi na miongoni mwa memebrs wa humu 90% walitoka kule na ni wengi waliompigania kikwete achagulike kutoka kura za maoni, mimi falesy nilkuwa kinyume na kikwete lakini leo hii ni rais wa jamhuri ya muungano, biblia inasema usiwasemee vibaya wakuu wa watu wako. Kikwete ni mkuu wa watu wangu watanzania hata siku moja siwezi kumsemea vibaya. MNA LAANA NYIE MNAOMSEMA VIBAYA RAIS KILA KUKICHA NA LAANA YENU HAITAPONA HATA VIZAZI VYENU VITATU NA VINNE. tafadhali sana najua mna jazba na RAIS lakini isiwe kila kukicha mnatafuta kumgombanisha na wananchi kama hawafai basi subirini 2010 msimchague.
na hao kina lipumba na slaa wanona hafai basi wasubiri 2010 wagombee washinde hapa jamani ni jukwaa la mawazo huru ya kujenga taifa hili si jukwaa la kujadili maamuzi ya Rais yapi afanye, yapi alitakiwa afanye na nani na nani wawajibishwe kama mnataka kasomeeni sheria na mfungue mahakama zenu na muanzishe majeshi yenu ya polisi muwakamate hao mnaotaka wakamatwe. pumbafuuuuuuuuuuuuuuuuuu
 

We mwenye adabu ni MMALAWI?
 


Huyu anaongea kama spy wa CCM aliyetumwa kukusanya majina na address za watu hapa ili CCM iwashughulikie.

Hivi unaelewa concept ya uhuru wewe? Vipi kuhusu uhuru wa kujieleza? Uasoma Amnesty International country report za Tanzania? Vipi kuhusu Transparency International? Unajua nini kuhusu privacy?

Wewe falesy unayetaka watu waanike majina yao halisi hapa JF mbona mwenyewe umeshindwa kufuata ushauri wako na kutupa jina lako, ubini wako, namba ya nyumba na mtaa unaokaa?

Unaelewa anonimity ilivyo central kwa free discussion wewe? Kuna watu wanakoma giladi mpaka familia zao wenyewe, we untaka waje kwa majina yao hapa?

Ushawahi kusoma historia ya "Publius" na service yake katika kuendeleza freedom of speech? Ushawahi kusikia kitu kinachoitwa "The Federalist Papers" na mchango wake katika public discourse in shaping public opinion?

Mbona unaongea kama mtu aliye na shallow horizons ambaye haoni mbali na mipaka ya Tanzania?
 
Aaah, mbona na wewe jina lako halina uhakika? weka jina full plus picha. Halafu mwenzetu ni mtu wa wapi? Mkenya weye? Mbona wasema watanzania hawana adabu ili hali na wewe ni Mtz? Ina maana na wewe ni kama hao unaowasema? Nayaunga mkono mawazo yako, but it seems hujatulia.
 
Hakuna aliyekamili,,kama akikosea asifiwe au aambiwe ili kama anaweza arekebishe?
Yeye(JK) kasema kwamba 70 % wanafuata upepo,(sijui alimaanisha nini) Je kama watu wamejitokeza hadharani na kusema JK anaenda vibaya na wameungwa mkono na wengi je sio kwamba kunaukweli fulani?
Mwenyewe umesema 90% ya member of this forum walimpigia debe JK aingie ikulu je unaweza kusema ni kwanini leo hao wanampinga?
 
nadhani una ubongo mdogo ndo maana unajaribu kujustify upuuzi kuwa maoni ya watu. ni lazima uweke mazingira magumu ya kuishi ili kuhalisha kuishi kwako. kama unatoa maoni na unaogopa kwamba ukijulikana weye ndiye mtoa maoni utapata shida na huenda kupoteza maisha, basi huna maana na maoni yako hayana maana. ukweli unabaki palepale hata kama nimetumwa na CCM au nimetumwa nyeyote, haiwezekani kuacha hali hii wapo watanzania wanhitaji tujadili mambo yao, tuwasemee lakini kila siku kudandia hoja kama nzi au mende kabatini, hakuna anayeibua vitu vipya ni majungu tuu, majungu tuuu hata haileti maana.
soma sana historia unaweza kupata hadi uprofesa kwa kusoma na kuandika historia za watu yako haitasomwa popote mchovu wa kufikiri wewe
 
nadhani una ubongo mdogo ndo maana unajaribu kujustify upuuzi kuwa maoni ya watu. ni lazima uweke mazingira magumu ya kuishi ili kuhalisha kuishi kwako. kama unatoa maoni na unaogopa kwamba ukijulikana weye ndiye mtoa maoni utapata shida na huenda kupoteza maisha, basi huna maana na maoni yako hayana maana. ukweli unabaki palepale hata kama nimetumwa na CCM au nimetumwa nyeyote, haiwezekani kuacha hali hii wapo watanzania wanhitaji tujadili mambo yao, tuwasemee lakini kila siku kudandia hoja kama nzi au mende kabatini, hakuna anayeibua vitu vipya ni majungu tuu, majungu tuuu hata haileti maana.
soma sana historia unaweza kupata hadi uprofesa kwa kusoma na kuandika historia za watu yako haitasomwa popote mchovu wa kufikiri wewe
 
yanii nchi inaoza tuendelee tu kuimba zidumu fikra za mwenyekiti wa ccm, to hell, acha na iwe laaana maana mpaka sasa ni kama tuna laana kama wageni wananeemeka na hii nchi kwa kupitia mgongo wa watu wachache wakati asilimia kubwa ya walipa kodi hatujui kesho tutakula nini, wazee wetu kijijini wakiumwa hata panado hamna hospitalini, wadogo zetu wanakaa kwenye mwae darasani, laana gani zaidi ya hii unataka, weke contact zako tuwasiliane labda una mbinu mbadala wa kuokoa hiii nchi
 
mkubwa anastahili kupigiwa makofi akifanya jambo la maana, na akikosea anatakiwa apigwe makofi pia, so he is getting his right share, please give out your contact, labda unaweza kuokoa hii nchi, mimi kama mtanzania ninaelipa kodi nisiyojua maana yake amd getting nervous
 
kaka/dada samahani mie ni mtanzania mwenyeji wa iringa kihesa semtema kribu na chuo kikuu tumaini, mkazi wa maeneo hayo natoka familia ya wastani kwa kipato wenye uwezo wa juu kufikiri na wenye uwezo wa kuthubutu kufanya mambo yasiyo tarajiwa. siogopi yajayo nachukia yaliyopita mabaya kwangu siku ni leo na bora kwa kuijadili kesho jana imekwenda, majungu si mtaji ndo tabia yangu nachukizwwa na wadandia hoja, kwetu wakubwa wanaheshimiwa na msingi wa dini yangu hauniruhusu kumsema mkuu wa watu wangu, ni msingi huo unanituma kuwaheshimu watumuishi wa Mungu Mfalme ni mtumishi wa Mungu na upanga na haubebi bure ni haja yangu kumheshimu atanikirimia na ni adhabu kwangu nikimletea jeuri.
tusihoji uraia tuangalie ukweli wa mantiki.
 

Kama unaamini katika uwazi jina lako nani?

Unatuambia nini sie tusioamini dini wala kuwako kwa mungu, tunaoona kama dini imetumika kupalilia ukondoo, na kuruhusu ubeberu wa watawala, kuanzia wafalme wa kichina kutoka Hsia, Qing na Ch'in dynasties na tawala za Hammurabi na nyingine za kibabeli mpaka George W. Bush na Kikwete kwa kupitia msanii wake Makamba? Kuanzia biashara ya utumwa, ukoloni, ukoloni mamboleo mpaka globalization? Tunaoona kwamba ukondoo huu, unaoambatana na dini na kuamini kwamba kila kitu anachosema mkubwa ni sawa, ndio uliotufikisha pabaya hapa tulipo?

Kama tungekuwa tuna operate under the principle kwamba wakubwa wako sawa all the time, then Galileo asingeweza kumsahihisha Aristotle, Copernicus asingeweza kumsahihisha Ptolemy, Einstein asingeweza kumu update Newton.

Usitake kutuambia kwamba wakubwa hawashawishiki.
 
tutakwenda mwisho twaweza fika kule twatrajia tufike.
nadhani tusitafute mbaya wa haya bali tukae kama watu wenye nia njema na watanzania milioni 36 wanaoutazamia ufalme huu uwape yale ya maana kwa maisha yao.
sidhani kama kurumbana kwenye internet wakati ubinafsi umetujaa twaweza okoa jahazi. karibu kwenye tamasha la wajasiria wasiojua ujasiria mahali, siku na wakati nitakaokupa. kontacts isiwe taabu matusi sipokei, usipige leo usiku sipokei cm, usipige kesho na keshokutwa weekendi sipokei cm ngeni, piga jumatatu kuanzia saa nne asubuhi
 


Just another deluded idiot
 
Naamini ulikuwa unataka ujulikane kama fallacy na sio falesy kama ulivyoandika, mwongo mimi?
 

Nashukuru kwamba umenifahamisha nina ubongo mdogo, nilitaka sana kuwa na ubongo mkubwa zaidi lakini sikupenda that Worf look



Lakini inaonekana, ingawa inawezekana nina ubongo mdogo, ubongo wako wewe ni mdogo zaidi.

Kwa sababu unataka watu waje na majina yao halisi bila kutoa jina lako mwenyewe.

Hilarious.
 

Waambie wana blog, maana sisi tukisema tumetumwa
 
Wewe Falesy unayejikomba kwa akina Makamba kwa kuwa ni marafiki zako umeficha jina lako,nenda Kenya ndio utaona Kibaki na Raila wanavyosemwa,ukiwa na makosa utasemwa hadi kaburini na habari ndio hiyo wewe mwenye vision ya kujipendekeza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…