Watanzania hawapendi maandamano au hawajui haki zao?

OLS

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2019
Posts
426
Reaction score
685
Achana na maandamano ya CHADEMA, miaka kadhaa iliyopita kulikuwa na maandamano ya wamachinga. Mtu mmoja ambaye alitajwa kuwa msemaji wa wamachinga alirekodiwa akiwataka watu wengine wasiandamane kwa kuwa wakivunjwa miguu watakaoathirika ni wao na sio walioandaa maandamano.

Nilipoona video ile nikaona ni mtu anayekataa kudai haki zake kwa kuwa anaona si haki yake kudai haki yake. Yaani hana sauti lakini hataki kutumia namna zinazotambulika kupaza sauti yake. Akisema kuna kuvunjwa miguu, maana yake alikuwa anaona ni haki kwa polisi kuwapiga badala ya kuwalinda ili sauti zao zifike mbali.

Hiyo si mara ya kwanza kwa wananchi kuonesha kuwa hawako tayari kutumia haki zao kupaza sauti zao. Mwaka jana kama nakumbuka, kulikuwa na ugomvi kwenye mziki wa kizazi kipya kati ya wakenya na watanzania. Mimi ni mtanzania lakini ile diss track ya "Bongo Favor" aliyoandika Kaligraph Jones ilikuwa na ujumbe maridhawa kwa wasanii wa Tanzania. Hata hivyo wasanii wa Tanzania wakawa wanai-diss Kenya "Eti wamezoea kuandamana". Yaani kupitia musiki msanii anawaona wanaotumia haki yao wanakosea. Hii ilinipa maswali sana kwa watu wanajiona wako-consicous kushindwa kutambua haki zao za msingi kiasi cha kuwadiss wanaosimamia haki hizo.

Suala hili halijaishia hapo, hivi karibuni, kumekuwa na maandamano ya CHADEMA miji mbalimbali, ni maandamano ya amani. Lakini kinaibuka chombo kudhihaki maandamano hayo. Najiuliza kama kweli wananchi wote wamelewa kwa kuamini wao ni serikali au ni kweli wananchi hawataki kupaza sauti zao kupitia maandamano.

Nawaza kama maandamano hayahitajiki, mbona sioni watu kudhihaki maandamano ya kusapoti vitu mbalimbali. Je wananchi hawaoni wanaongea ugumu kwenye maandamano ambayo yanalenga kudai haki? Haki ni tofauti na maandamano ya kusifia au kusapoti kitu.

Inakuwaje wananchi wanakubali kuzuiwa maandamano ya kudai haki kuziwa lakini hawahoji maandamano ya kusifu hayazuiwi. Je ni sahihi kuzuiwa kudai haki.?

Mbali na yote najua wananchi wana ujinga mwingi kuliko uwezo wakuchanganua mambo, hivyo ni wito kwa asasi za kiraia za kutetea haki za raia kufanya jambo kwa watu hawa ili kuongeza ufahamu. Fuatilia makala zangu za awali kuhusu elimu ya uraia
 
Umezungumzia suala muhimu sana linalohusu haki ya maandamano na ushiriki wa wananchi katika kudai haki zao. Ni kweli kumekuwa na mifano kadhaa ya hivi karibuni nchini Tanzania inayoonyesha mitazamo tofauti kuhusu maandamano na haki za kiraia.

Mfano wa msemaji wa wamachinga unaoelezea kuhusu kuvunjwa miguu ni wa kusikitisha. Inaonyesha wazi kukata tamaa na kukubali dhuluma badala ya kupigania haki. Ni muhimu kukumbuka kuwa maandamano ni njia halali ya kuonyesha kutoridhika na kudai mabadiliko.

Maandamano ya CHADEMA na majibu yanayotokana na vyombo vya habari yanaonyesha changamoto zinazokabiliana na waandamanaji nchini Tanzania. Ni muhimu kukumbuka kuwa maandamano ya amani ni haki ya kikatiba na yanapaswa kulindwa na serikali. Kuzuia maandamano bila sababu ya msingi ni ukiukaji wa haki za kiraia.

Ni kweli kuwa baadhi ya watu wanaweza kuwa na wasiwasi kuhusu gharama na usumbufu unaoweza kutokea kutokana na maandamano. Hata hivyo, ni muhimu kupima faida dhidi ya hasara. Maandamano yanaweza kuwa na ufanisi mkubwa katika kuleta mabadiliko chanya na kuhamasisha jamii.

Asasi za kiraia zina jukumu muhimu la kuhamasisha elimu ya uraia na kuwajulisha wananchi kuhusu haki zao. Pia wanaweza kusaidia kuratibu maandamano ya amani na kuhakikisha usalama wa waandamanaji.

Ni muhimu pia kukumbuka kuwa kuna njia zingine za kudai haki mbali na maandamano. Hizi ni pamoja na kuandika barua kwa viongozi, kushiriki katika kampeni za mitandao ya kijamii, na kujihusisha na vikundi vya kutetea haki.

Kwa kumalizia, ni muhimu kwa wananchi wote kuelewa umuhimu wa haki ya maandamano na kuwa tayari kutumia haki zao kudai mabadiliko chanya. Asasi za kiraia zina jukumu muhimu la kuhamasisha elimu ya uraia na kuunga mkono juhudi za wananchi kudai haki zao.

Pamoja, tunaweza kujenga jamii yenye haki na usawa zaidi ambapo sauti za kila mtu zinasikilizwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…