Watanzania huwa mnatamani zogo na Kenya, ilhali sisi ndio soko lenu kubwa ukanda huu

Watanzania huwa mnatamani zogo na Kenya, ilhali sisi ndio soko lenu kubwa ukanda huu

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Mara nyingi mnajipiga vifua mkisema tufungiane mipaka, kwamba hamtuhitaji kwa lolote wala chochote, ilhali data zinaonyesha Kenya ndio baba likija kwenye suala la masoko ya bidhaa zenu ukanda huu, yaani hata ujumuishe Uganda, Burundi, Rwanda bado hawafikii thamani ya manunuzi yetu kutoka kwenu.
Pia uhamiaji wakiwapa data ya idadi ya Watanzania wanaovuka mpaka wakija Kenya, mtashangaa sana.
Hivyo endeleeni kutamani kulianzisha na Kenya mkidhani sisi ndio tutaumia pekee yetu, ila kilio kitasikika kote huko, mtakula hiyo pamba wenyewe....hehehe
--------------------

THAMANI ya mauzo ya Tanzania katika Soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki imeendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi (pichani) alisema hayo jana wakati wa hotuba yake ya Mpango wa Makadirio ya Bajeti ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020.
Alisema katika kipindi cha mwaka 2018 mauzo yaliongezeka kufikia Dola za Marekani milioni 448.5 kutoka Dola za Marekani milioni 312.5 mwaka 2017 sawa na ongezeko la asilimia 43.6 Waziri Kabudi alisema mauzo kwenda Kenya yalikuwa ni asilimia 47.7 wakati mauzo kwenda Uganda yalikuwa ni asilimia 23.4 ikifuatiwa na Rwanda asilimia 17.8 na kuwa bidhaa zilizouzwa kwa wingi ni pamoja na mahindi, karatasi, viuatilifu, saruji, marumaru, konyagi, ngano na mafuta ya kupaka.
Alisema thamani ya ununuzi wa bidhaa kutoka nchi wanachama wa jumuiya ilipanda kwa asilimia 27.7 kutoka Dola za Marekani milioni 237.0 mwaka 2017 hadi kufikia Dola milioni 302.7 mwaka 2018 na kuongeza kuwa bidhaa zilizonunuliwa kutoka Kenya zilikuwa ni asilimia 81.75 wakati asilimia 17.40 zilinunuliwa kutoka Uganda.
Kwa mujibu wa Waziri Kabudi, soko kubwa la biashara za Tanzania katika Jumuiya ya Afrika Mashariki ni Kenya ikifuatiwa na Uganda na kuwa wizara imeratibu utekelezaji wa Himaya Moja ya Forodha ya Afrika Mashariki ambayo ni sehemu ya Umoja wa Forodha.
 
Hii ni moja ya sababu kuwa ya kuharakisha kukamilisha miradi ya transportation infrastructure ktk EAC, biashara zitaongezeka sana kama SGR zitakamilika, ofcourse bila wizi wizi lakini🙂
 
Kenya ni Baba yao. Am imagining Kenya boasting to The US eti "tunawavisha" nguo juu they are our largest consumer of textiles as if they can never have substitutes. Danganyikan mentality huwa ovyo Sana.
 
Weka thamani ya mauzo ya kenya kwa Tanzania tufanye comparison
Tukiamua tu KQ ije mara moja kwa wiki ndio utakua mwisho wa hilo shirika
Wewe mwenyewe unakuja Dar kuleta milo na sausages
 
Back
Top Bottom