Ukikutana na Mtanzania kipindi ambacho sio cha uchaguzi, unaweza fikri chama tawala kitaondolewa madarakani.
Mkulima atalalamika kuhusu bei mazao yake, atakwambia namna serikali isivyo mjali kwa kumpa ruzuku na namna anavyoumia kwa zuio la kuuza mazao nje.
Mfanyakazi atakwambia imepita miaka 5 bila nyongeza ya mishahara, na namna alivyopandishiwa makato kwenye HESLB.
Mfanyabiashara atakwambia tangu utawala huu uingie madarakani, biashara zimekuwa ngumu, biashara haiendi kabisa, vile vile atakwambia namna anavyokadiriwa kodi kubwa na mamlaka ya mapato ambayo haiendani na kipato chake.
Mhitimu wa chuo atalalamika namna serikali ilivyomnyima ajira, aidha atakwambia namna alivyojitutumua kufanya biashara bila mafanikio kutokana na mazingira kuwa magumu na ukosefu wa mitaji.
Wasanii nao utasikia wanalalamika namna ambavyo hawafaidiki na kazi zao, jinsi serikali isivyowajali kwa kuwatungia sheria za kulinda kazi, watakwambia hawanufaiki na kazi zao na namna serikali isivyojali.
Wagonjwa hospitalini watalalamika namna wanavyokosa dawa hospitalini.
Lakini sasa ikifika wakati wa kufanya maamuzi kwa mustakabali wa maisha yao hawaonekani tena, yule mkulima, Mfanyakazi, Mhitimu na Mfanyabiashara utamkuta na nguo zake za kijani akihamasisha watu wachague viongozi wale wale aliokuwa anawalalamikia,
Wasanii wao nyimbo wanatunga kabisa kukisifia chama kile wanachokilalamikia na kuwa kivutio kwenye kampeni.
Watanzania tunakwama wapi? Ni nani aliyeturoga?