Watanzania imefika kipindi sasa tusizuzuke sana na lugha za Kingereza na Kiswahili kwa wasio Watanzania

Watanzania imefika kipindi sasa tusizuzuke sana na lugha za Kingereza na Kiswahili kwa wasio Watanzania

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Hii tabia ya kuzuzuka na kusheherekea pale Mtanzania hasa mwanasiasa akijua kuongea Kingereza hata kwa kunyoosha sentesi mbili tu imepitwa na wakati na ni ushamba.

Pia wanasiasa wasiojua Kingereza ni vyema wakatumia Kiswahili tu, hakuna aibu kutumia lugha yako unayoimudu vizuri, hakuna haja ya kulazimisha lugha usiyoimudu vizuri.

Pia tabia ya kusherehekea na kushangaa mtu asiye Mtanzania anapozungumza Kiswahili kilichonyooka ni ushamba uliopitwa na wakati.

Kiswahili kimekuwa lugha kubwa sana, kinazungumzwa na raia wengi wa nchi zilizotuzunguka kama lugha yao na pia kwa sababu ya kuongezeka kwa muingiliano wa watu.

Pia watu wengi duniani hata nchi za mbali wanajifunza Kiswahili katika vyuo na wanaongea Kiswahili vizuri tu kabisa.

Tuache kuwa kama tuko kwenye chungu.
 
Akili ya waafrika walio wengi zinateswa na urithi wa ukoloni. Leo hii Afrika mashariki usipoweza kuongea kiingereza ambayo ni lugha ya wakoloni unaonekana mshamba
 
Back
Top Bottom