BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Jarida la Forbes katika toleo lake la 9 limetoa orodha ya ‘FORBES AFRICA 30 Under 30’ Vijana 30 wenye ushawishi mkubwa Barani Africa kwenye Sekta za Ujasiriamali, Uvumbuzi na Uongozi ambao unakuza uchumi na unaongoza mustakabali wa Afrika ambapo Tanzania imeingiza Vijana wawili akiwemo Mtanzania Jessica Julius Mshama (27) @jessicamshama ambaye ni Mkurugenzi wa Taasisi ya ‘Nakua Na Taifa Langu’ na Mkurugenzi wa Shule ya Assumpter Digital Schools pia ni Balozi wa Vijana wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mtanzania mwingine ni Isaack Damian Buhiye (28) ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya “Firm 23 Limited” ni miongoni mwa Vijana wenye umri chini ya miaka 30 walioorodheshwa kwenye jarida hilo la Forbes kwa mwaka 2023.