Wanabodi,
Ingetrex Tanzania, 2014, ni fursa za kushiriki biashara za kimataifa kwa bidhaa na huduma ambapo sasa kwa mara ya kwanza, fursa hii, imeletwa Tanzania ambapo itaanza kwa maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ambayo yanaitwa Ingetrex, yatafanyika jijini Dar es Salaam, katika ukumbi wa Diamond Jubilee kwa muda wa siku 3 kuanzia Alhamisi hii, Ijumaa na Jumamosi.
Sasa ili kubaini fursa hizo za Ingetrex Tanzania, fuatana nami asubuhi hii katika Kituo cha Television cha Chanel Ten, ambapo tutazungumzia fursa mbalimbali za Ingetrex na Watanzania, tufanye nini kuzichangamkia!.
Karibuni.
Pascal