ielewemitaa
JF-Expert Member
- Jan 7, 2014
- 11,016
- 9,722
Mbona sisi tumekwenda kuwasitiri wao?
Kwamba shetani hachukiwi na wote?
Bila shaka anachukia na wengi kama ilivyo sisi kwa sasa.
Mabibi na mabwana moja kwa moja kwenye mada.
Siyo siri tena zama zimebadilika na matukio yanakwenda kwa kasi sana. Taifa letu likipita katika kipindi kigumu ambapo kwa bahati mbaya kumezuka hata makundi katika jamii ambayo yamelenga kupiga makelele tu yakijaribu kulazimisha kuufanya uongo kuonekana kuwa ukweli au ukweli kuwa uongo. Mithili ya kujidanganya mchana kuwa ni usiku au usiku kuwa ni mchana.
Mifano iko mingi mno na katika nyanja nyingi.
Ikumbukwe kuwa ukweli ni ukweli na uongo ni uongo na utabakia kuwa hivyo bila ya kujali nani kasema nini au nani atasema nini.
Ukweli mchungu hulka mpya hii haikuwahi kushuhudiwa katika awamu yoyote ya uongozi kabla ya awamu ya hii.
Hivi karibuni tumeondokewa na mzee wetu rais mstaafu mzee Mkapa (rip). Pamoja na sisi kushiriki sana katika shughuli zote za wenzetu, ni Burundi peke yake ndiyo walioweza kutuma ujumbe wao rasmi kuja kutuhani kwenye msiba huu mkubwa kutoka nyumbani kwao.
Si Malawi tulikokwenda kwenye kuapishwa kwa rais Chakwera. Si Zimbabwe tulikokwenda kumhani raisi wao Mugabe (rip). Si Afrika kusini tulikokwenda kumhani Mandela (rip) wala Winnie (rip). Wote hawa, hawakutuma wawakilishi wao rasmi tokea makwao kuja msibani sisi yalipotukuta.
Si Kenya tulikotuma ujumbe wetu mzito kabisa wakiwamo marais Kikwete na Mkapa (rip) kwa pamoja kuwahani kwenye msiba wa rais Moi (rip), kuwa walikuja kutuhani sisi yalipotusibu miezi michache tu baadaye.
Si Zambia, si Mozambique, si Rwanda, si Congo wala Uganda waliofika msibani.
Si nchi za Comesa, SADC, Ulaya, Marekani kaskazini wala kusini, Si Asia zikiwamo Uarabuni, Afrika wala Australia waliotukumbuka.
Hamkani si shwari tena bila ya kujali makelele yetu yote, kwa hakika hatuko vizuri. Kama waungwana tunapaswa kujiangalia. Vinginevyo makelele yetu mengi yanaweza kuwa ni kutokea kwenye madebe matupu yasiyoacha kuvuma.
Tukumbuke maneno matupu hayavunji mfupa.
Alipotutoka baba wa taifa (rip), Afrika yote hata dunia walikuwa hapa. Marais karibia wote, SADC, COMESA, ECOWAS, nk achilia mbali wawakilishi wazito wazito mabeberu walikuwa hapa kutuhani msiba ule.
Walikuwapo hapa hadi kina Madeline Albright waziri wa mambo ya nje wa Marekani.
Hiyo ndiyo Tanzania iliyokuwa ikisomeka vilivyo duniani kote chini ya rais Mkapa (rip).
Uzi huu kwa hakika tulipo upo, unatuhusu sana na hasa katika zama za leo:
Corona: Mizozo ya mipakani, wa kulaumiwa ni Tanzania
Matatizo hayatanzuliwi kwa kuyakimbia, kujificha au kuyafumbia macho.
Kupafahamu wapi tulipojikwaa ni hatua njema katika kujipanga vizuri zaidi. Kujitenga au kuruhusu kutengwa kamwe hauwezi kuwa uchaguzi ulio bora.
Kujikwaa si kuanguka.
Na huo ndiyo ulio ukweli mchungu.
Mkuu brazaj majirani wivu tu unawasumbua,si unajua tupo uchumi wa kati,hao wanatuonea gere hawajaja lakin mzee wetu tumempumzisha kwa amani nyumba yake ya milele
Mungu ambariki Mzazi aliyekulipia ada, hakulipa bure! Mungu akajibu kila ombi la moyo wake!
Tunajiona tuko sahihi sana, tukikosolewa tunakua Wakali kama nyigu mjamzito! Kejeli, vijembe, ulimbukeni, kujikweza na kujiona kuwa tuna kila kitu na hakuna wa kutubabaisha....! Tutakuja kuanguka vibaya tukose wa kutusaidia
Hivi status yetu ikoje kwa mataifa mengine ukiachana na Kenya?
Burundi pekee ndiye mwenzetu aliyebakia. Wa kufa na kuzikana.
Mkuu nakusoma na hasa kwa mistari kwa mstari kama ulivyoandika.
Subiri waje na vibwagizo zaidi na mapambio ya kujazia. Huwezi kuamini!
Heshima kwake aliyeandika hili:
View attachment 1525514
Natamani ingekuwa ni jinamizi, lakini kwa bahati mbaya ndiyo ukweli wenyewe.
dah!
nshajiuliza san hili'
JPM ni mtu wa kujali vitu na sio watu.
Muwe wazalendo basi. Au mmetumwa na mabeberu? Hii ni vita ya kiuchumi. Bro Magu chapa kazi. Usisikilize kelele za chura. Hongera sana kwa kulijengea taifa heshima
Umeongea vitu vya msingi
But points of correction katika msiba wa Mandela JK Alienda na alitoa speech
Mkuu hiyo ni point of addition (badala ya correction) zaidi sana ya kuwepo tu. Tulikuwapo tukapewa na heshima zaidi kutoa speech.
Hata kwenye msiba wa rais Moi (rip) zaidi sana ya kuwapo, tulipewa pia heshima kama hiyo ya kutoa speech.
Hii ni kama ilivyokuwa kwa Madeline Albright mwakilishi wa beberu kwenye msiba wa mwalimu (rip).
1.Kwenda kuwasitiri ni uamuzi wetu ata tusingekwenda hakuna adhabu ambayo tungepewa
2.SHETANI hajawai kuchukiwa na wote , watu kibao wanampenda kimaneno na kivitendo
Ata Israel anachukiwa na waarabu wengi lakini ameendelea sana kiuchumi na kijeshi kuliko hao wanaomchukia , nimekwambia chuki zinaongeza hasira kuwa mbunifu zaidi mpaka wanaokuchukia wakuheshimu, tulia tuli dawa itawaingia vizuri
Kuna watanzania wapuuzi sana kama mtoa mada
Kwamba kujikombakomba kwa mataifa mengine ndiko kutatuweka pazuri!?
Hii nchi ni huru na ina misimamo yake tangu zamani. Tumeonyesha upendo kwa mataifa mengine pengine kuliko nchi yoyote.
Tumeshiriki ukombozi wa nchi zao dhidi ya ukoloni, tumewahifadhi wapigania uhuru wao hapa kwetu, tumesaidia kulinda amani, tumewapa misaada ya vyakula, kijeshi n.K, tumehani na kushiriki misiba ya viongozi wao kwa heshima kubwa.
KAma yote hayo hawayaoni na mnaendelea kutaka tuwanyenyekee basi tambueni ya kuwa IMETOSHA.
Ni wakati sasa wa Tz kujali mambo yake na maslahi ya watu wake baaaas.
Tumeanguka wapi?Mkuu kama taifa tunatatizo kubwa,lakini badala ya kuangalia tumeanguka wapi ili tubadirishe strategy na kusonga mbele,kazi yetu ni kunyoshea watu vidole na kuwalaum wengine hasa Kenya.
Wewe bado mdogo haya Mambo ni makubwa mno kwakoTumeanguka wapi?
Tubadilishe strategy zipi?
Nani ana walaumu wa Kenya na kwasababu gani Wakenya wanalaumiwa?
Umeraise hoja mwenyewe unashindwa kuzijibu,maana yake hata unachokiongea hukijui bali una payuka na kuropoka.Wewe bado mdogo haya Mambo ni makubwa mno kwako
Mkuu ulitaka nijitetee? Kama wewe huwezi kuona kwa direction tuliyochukua kudeal na covid_19 hasa kitendo Cha kuficha data hakikuwa sahihi,why nipoteze muda wangu kuargue na wewe?Umeraise hoja mwenyewe unashindwa kuzijibu,maana yake hata unachokiongea hukijui bali una payuka na kuropoka.
Ndio maana ukajiita Sijijui
Data zipi mbona huombi data za malaria,Ukimwi,Homa ya Ini magonjwa ambayo yanaua sana kuliko Corona,why unataka data za Corona?Mkuu ulitaka nijitetee? Kama wewe huwezi kuona kwa direction tuliyochukua kudeal na covid_19 hasa kitendo Cha kuficha data hakikuwa sahihi,why nipoteze muda wangu kuargue na wewe?
Mkuu corona was declared as global pandemic.upo category tofauti na hayo magonjwa uliyotajaData zipi mbona huombi data za malaria,Ukimwi,Homa ya Ini magonjwa ambayo yanaua sana kuliko Corona,why unataka data za Corona?
Sawa imekuwa declared sijakataa,sasa kwa nini huombi data za magonjwa kama Malaria,Ukimwi,Homa ya ini nk ambayo yanaua watu wengi zaidi ya Corona?Mkuu corona was declared as global pandemic.upo category tofauti na hayo magonjwa uliyotaja
Ndio maana mkuu nimetoka kueleza kuwa huko kwa wenzetu athari za corona tuliziona haikuhitaji takwimu kuweza kujua kuwa hali ni mbaya.Sawa imekuwa declared sijakataa,sasa kwa nini huombi data za magonjwa kama Malaria,Ukimwi,Homa ya ini nk ambayo yanaua watu wengi zaidi ya Corona?
Au issue ni kuwa declared na si impact (vifo) yake katika MAZINGIRA HAYA YA KWETU.
Mkuu acha umimi hata Kama wewe ni mama wa nyumbani,hivi Kama ugonjwa ulianzia Wuhan china na kusambaa dunia nzima unashindwaje this time around kutokea kwa watanzania ambao ni sugu kwa kila magonjwa na kwenda kuua watu wanaojari maisha yao huko duniani? Au wewe unadhani Tanzania ni kisiwa?kwamba hakifikiwi na mtu mwingine yeyote yule au watu wake hawatembei?Sawa imekuwa declared sijakataa,sasa kwa nini huombi data za magonjwa kama Malaria,Ukimwi,Homa ya ini nk ambayo yanaua watu wengi zaidi ya Corona?
Au issue ni kuwa declared na si impact (vifo) yake katika MAZINGIRA HAYA YA KWETU.
Nimekwambia kuwa hata mazishi ya Nkurunzinza hao uliowataja hawakwenda, je pia huko kuna tatizo gani pia?Kwani ni kwenye msiba huo tu? Pia umesahau kuwa sisi Corona haipo. Wataogopa vipi kuja kusiko na Corona hata kama kwao ipo?
Kwenye Kuukimbia ukweli, mambo iko huku:
"Mifano iko mingi mno na katika nyanja nyingi."
Hakutatusaidia.
Kwani wewe MAMA WA NYUMBANI?Mkuu acha umimi hata Kama wewe ni mama wa nyumbani,hivi Kama ugonjwa ulianzia Wuhan china na kusambaa dunia nzima unashindwaje this time around kutokea kwa watanzania ambao ni sugu kwa kila magonjwa na kwenda kuua watu wanaojari maisha yao huko duniani? Au wewe unadhani Tanzania ni kisiwa?kwamba hakifikiwi na mtu mwingine yeyote yule au watu wake hawatembei?
Nimekwambia kuwa hata mazishi ya Nkurunzinza hao uliowataja hawakwenda, je pia huko kuna tatizo gani pia?
Mimi naona unakuza mambo tu, kwasasa marais wa nchi zilizojifungia hakuna anayesafiri. Nina uhakika bila corona kuwepo wote wangekuja may be Kenyatta tu ndiyo angekosekana