Watanzania kwanini tunalipa kodi?

Watanzania kwanini tunalipa kodi?

Izia maji

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2021
Posts
2,997
Reaction score
5,385
Hebu tujiulize " Kodi tunayolipa ni kwa matumizi gani?"

Tunamfahamu fika kuwa serikali ina vyanzo vingi vya mapato ambayo yanachangia miradi ya maendeleo. Vyanzo hivi ni pamoja na mapato yanayotokana na huduma za bandari, mauzo ya madini na mazao ya kilimo, usafirishaji nk.

Kodi tunazolipa kwa kiasi fulani zinachangia huduma za jamii tunazopata. Sasa kama kodi hizi haziwezi kukidhi gharama za huduma za jamii basi tuambiwe ni kwa nini na kwa kiasi gani. Inawezekana kabisa kiasi kikubwa cha kodi zetu kinaishia mifukoni mwa watu na starehe katika kuendesha serikali.

Kama kweli kodi zetu hazitoshi kwa nini serikali inajiendesha kwa gharama kubwa kupita uwezo wa kikodi? Haiwezekani kodi zisitoshe kutuhudumia halafu Serikali inanunua magari ya kifahari ambayo yanatumia gharama kubwa wakati huo huo tunaambiwa tuchangie bima ya afya kwa gharama ambazo wananchi wanashindwa kuzimudu.

Tunaona jinsi fedha zetu za kodi zinatumika hovyo kugharimia msururu wa magari katika ziara za viongozi! Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu wakifanya ziara mikoani misafara yao haipungui magari 50 kila mmoja.

Serikali imepandisha posho kwa wafanyakazi jambo ambalo linawashawishi kupanga safari za hovyo ilimradi wapate posho.

Kama kodi zetu hazitoshi basi tuanze kuona kwa vitendo serikali ikibana matumizi.
 
Akili ya mtu mweusi ni tatzo,sisi tuliubwa tuwe watumishi na sio watawala,hatuna akili za kuwa watawala.

Kuna kiongozi alisema hayo maisha wanayoishi na magari wanayonunua ni lazima yafanyike maana wanajiweka katika standard fulani ambayo watawala wanatakiwa waishi hivyo hata kama mwananchi akifa njaa,
 
Akili ya mtu mweusi ni tatzo,sisi tuliubwa tuwe watumishi na sio watawala,hatuna akili za kuwa watawala.

Kuna kiongozi alisema hayo maisha wanayoishi na magari wanayonunua ni lazima yafanyike maana wanajiweka katika standard fulani ambayo watawala wanatakiwa waishi hivyo hata kama mwananchi akifa njaa,
Hakika tuna safari ndefu ya kujitambua na ustaarabu! Bila wananchi kuchukua hatua za kujikomboa kifikra mateso yataendelea!
 
Back
Top Bottom