Vhagar
JF-Expert Member
- Jun 8, 2015
- 20,550
- 39,949
Utafiti wangu usio rasmi nimekuja gundua kwa miaka inavyozidi kwenda watanzania wamekuwa watu wa kughadhibika sana. Jambo dogo tu hata lisilohitaji kutumia hasira mtu anaweza kukuwakia ukikaa vibaya anaweza tamani amuweke mtu vibao.
Ni ugumu wa maisha au tatizo nini? Ndugu zangu matatizo hayatatuliki kwa kuwaka hasira. Zaidi jazba zitafanya ushindwe kuchukua hatua sahihi.
Nawapa sana pole watu ambao shughuli zao kutwa nzima washughulika na watu tofauti tofauti kama makondakta hawa kazi yao ngumu sana.
Yaani hata humu kwenye nyuzi swala dogo tu mtu anapandwa na jazba. Huyo unayemkasirikia huenda si chanzo cha yanakusibu tuishi kwa upendo tonatofautiana uelewa usitake kila mtu awaze kama wewe.
Unamkasirikia nani na maisha umeyakosea mwenyewe?