Dunia nzima hakuna kutangazwa mshindi baada ya mshindi kujulikana ,anachofanya Odinga ni kujitekenya na kucheka mwenyewe.
Odinga alichofanya ni Kama alichofanya Hayati Seif alipoona kashindwa akaamua kujitangaza mshindi na huo ndio ukweli mchungu Odinga alidhindwa akaamua kushinikiza uongo uwe ukweli.
Sometimes uwa tunajitoa ufahamu kufikiri yasiyowezekana yanaweza kutokea kimiujiza, Ruto ni Rais aliyeandaliwa na mbingu kuiongoza Kenya na mbingu ikiamua hakuna wa kutengua.
Haya ndio makosa yaliyofanywa na Odinga na yamemgharimu pakubwa Sana.
Kwanza, kumpendekeza mpagani kuwa mgombea mwenza. Hapo ni Kama alijaribu uweza Mkuu wa Mungu. Sote tunajua Rais anapofariki makamu anakuwa Rais kwa matakwa ya katiba ya kenya hivyo ingetokea kwa mapenzi ya Mungu Odinga angetwaliwa basi ikulu ingeongozwa na mpagani. Mungu saidia CCM tusiwaze kuteua asiyeamini Mungu kuwa mgombea.
Pili, Sera za Ruto zilijikita katika maisha ya wakenya wa chini Sana kwa mfano Kama ile ya kuahidi kusimamia rasilimali za nchi kwa faida ya wakenya wote. Kama ilivyokuwa kwa Hayati Magufuli 2015 ahadi zake zilijikita katika kuijenga Tanzania. Watu wanaguswa na kiongozi aliye tayari kupambana kwa niaba yao.
Tatu, Nguvu za Ruto kisiasa. Ili Kenyatta ashinde alihitaji mtu mwenye nguvu Sana kwa siasa za Kenya na huyo hakuwa mwingine bali ni Ruto pia Kenyatta na Odinga wanalijua Hilo. Kwa hiyo Ruto anaweza kubezwa lakini ndani yake kuna nguvu Sana na nguvu hii inatokana na Imani na hofu ya Mungu.
Nne, Umri wa Odinga ulikuwa changamoto. Tukiachilia mbali nchi zilizoendelea kuchagua mtu mwenye umri wowote kwa nafasi ya Umri, kwa nchi zetu zinazoendelea kigezo Cha umri kinazingatiwa Sana na hii ni kwa Sababu umri mkubwa kwa Afrika una changamoto nyingi.
Tano, Ruto alikuwa ni Naibu Rais. Nakumbuka Mwalimu alikuwa anapenda Sana waziri Mkuu na mwanadiplomasia nguli Salim awe Rais baada yake lakini Getruda Mongela akaja na hoja iliyobadili upepo wa Salim kabisa na kumbeba mzee Mwinyi ambaye alikuwa makamu wa Rais kipindi hiko, alisema " Dunia itatushanga tukimchagua waziri Mkuu na kumwacha makamu wa Rais". Kwa kanuni hiyo hiyo wakenya ndio wameitumia kwamba wasingeweza kumwacha makamu wakamchagua waziri mkuu