Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,096
- 4,948
1. Tanzania na hasa upande wa serikali hakuna wanasheria wabobezi wa mikataba ya kimataifa
2. Kesi za Tanzania zilizofunguliwa kwenye mahakama za kimataifa zinasimamiwa na watumishi wa umma wanaona posho kama kipaombele na siyo wanasheria wabobezi.
3. Kesi hizi zinasimamiwa kwa siri kubwa huku timu ya Tanzania ikiwa imefichwa kuogopa uchambuzi wa CV za wahusika. Wengi wanaoshiriki hawajawahi kushinda kesi za ndani mahakamani. Ni waalimu wa sheria na watoto wa viongozi
4. Kwa sababu ya kukosekana uzalendo wanasheria wetu wameanza kulipa fidia nje ya maamuzi ya mahakama wakiwa wanabebwa na fikra za pre-bagaining mtaona kwenye kesi iliyoamukiwa hivi karibuni
5. Yapo majadiliano yanaendelea kwamba makampuni yaliyoshinda kesi yalipwe na yabadili majina yaje tena kuwekeza nchini fedha zilezile za fidia na shareholders wawe wale waliosaidia serikali kushindwa kesi. Fuatilieni makampuni yaliyoshinda kesi yanasambaza vipi faida zao...angalieni waajiriwa wao kama hawana nasaba na viongozi walioshiriki majadiliano
Pamoja na changamoto zilizotajwa hapo juu, nachukizwa zaidi kuona kwamba viongozi wote wa kitaifa wanaamini haya ni makosa ya JPM na hawana cha kufanya kuyarekebisha. Lakini tukumbuke hawa hawa ndio walikuwa wasaidizi wa JPM na walitetea kila jambo alilofanya.
Wapo viongozi wa upinzani wanashangilia kuona nchi inashindwa kesi. Huku ni kukosa uzalendo na kuombea taifa mabaya.
Hizi fidia wanaolipa ni wapiga kura wenu ninyi wapinzani. Kuchelea ni kufurahia wananchi kuendelea kunyonywa.
Mwisho, hata kama wana CCM na wapinzani mlimchukia JPM naomba mfahamu kwamba huyu Mzee alishamaliza mwendo. Hakuna namna ataamka kaburini kuja kulipa madeni.
Tunapaswa kumpongeza kwa sababu hakuna shilingi aliyochukua kwa mwekezaji akatia mfukoni mwake wala kuwekeza nje ya nchi. Alichukua akajenga barabara, reli, madaraja, madarasa, vivuko, meli nk Ninyi mmefanya lipi lakukumbukwa?
Pia soma
- Tanzania kuilipa Indiana Resources Ltd Bilioni 237 baada ya kuvunja mkataba mwaka 2018. Yatanguliza Bilioni 92