Watanzania na falsafa ya mpira biashara

Fredwash

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2009
Posts
1,400
Reaction score
2,010
Kwa yanayoendelea kipindi hiki kwenye soka letu.. Ni dhahiri bado tuna ushabiki wa kijima.

Ila lawama zote nazipeleka kwa hawa wanaojiita wachambuzi na waandishi wetu wa michezo. Ambao wamejipambanua wanauelewa mpana wa mpira na uendeshaji wake.

Cha ajabu hawana weledi wanaendesha mambo kishabiki yaan hawana tofauti na wale watu wa mambo ya shilawadu.

Wanaona jamii ya wapenda soka wengi wao hawaijui falsafa ya mpira wa kisasa ila wao kwa makusudi wanamua kutotumia nafasi zao kusaidia club zatu kwa maendeleo ya soka letu kwa kuwaelemisha wapenda soka kuwa hizo club kubwa zilifika huko kupitia njia hiz hiz.

Hawajui kuwa kwa nafas zao ndo walipaswa kuwa walimu wa kuwaelewesha watu nini maana ya kuwa professional player au professional league au professional club.. Maana wao wana wigo mpana wa kupata habari na tafiti.

Yaan haya yanayotokea sasa hv ni matokeo ya mafanikio ya club zetu .. Sasa mnataka kwenda kwenye level za wenzetu hamtak kuuza

Cha ajabu wachezaj wazur wa gharama pia mnasema bongo hatuna jeur ya kununua mchezaj wa 1b.. Sasa hamna jeur ya kununua ila bado mna jeur hamtak kuuza kwa hiyo 1b kwa hiyi mko kwenye mpira kwa ajili ya nini.

Akili za wapi hizi.. Kwa hiyo hawa wachezaj watafaidishaje club au wao na familia zao.. Au hamjui mpira ni kaz mtu ana ukoo nyuma yake.

Hv wanafikiri club hizo club za nje kuwa kubwa kifedha hizo pesa zinatoka mbinguni.. Au zinakuja kwa kubeba ubingwa tu..


Bingwa wa caf anapata kati ya 4b - 6b sasa jiulize aly ahal katumia shilingi ngap kwenye msimu wa mashindano uliopita tu.

Huyo kocha wake analipwa ngap kwa mwez.. Hivi wangekuwa na akili zetu wangejulikana.. Au unafikiri utajiri wao unatokana na kushinda makombe tu.

Sikatai ili team ikuwe na kujitangaza inatakiwa iwe na kikos imara kuliko cha mpinzan na pia nje ya uwanja inatakiwa iwe imejiwekeza kwenye facilities nzuri,

Sababu kumpata mchezaj mzur ni jambo la kwanza ila kuweza kumweka katika mazingira ya yy kuendelea kuwa bora ndo jambo lingine na ni gharama ndo maana kila leo club dunian zinaboresha system na miundombinu yao ya kiuendeshaji.

Club zenu hata viwanja vyake vyenyewe hazina.

Kuna njia mbili tu za kufika huko juu.. Mtu amwage pesa za kufuru kila mwaka ili alete wachezaj bora na ajenge mazingira ya kazi mazuri .

Hapo anatakiwa afumbe macho na awe na mapenz ya mpira hasa.. Kama alivyofanya katumbi wa tp mazembe.. Pesa za migodi ya dhahabu akawa anaziweka tp mazembe had iliposimama. Sasa hv kapunguza angalia kinachotokea mazembe.

Kama huwez kumwaga pesa za kufuru kama

Katumbi au waarabu wa mancity na psg au pyramid ambao mmilik wake aliinunua club akamwaga fedha kufuru ndan ya miaka miwili kafika nusu au fainali ya caf.

Ila katumia pesa nyingi sana yeye alitaka kuonyesha jeur ya fedha baada ya kuzinguliwa na kina alyahal au zamalek sina hakika ila alikuwa kwenye club mmoja kubwa.

Basi njia ya pili ndo hii ya kupata mafanikio uwanjan watu wakifika bei wachezaji wako uza then jenga team kiakili.

Itachukua mda kufika juu ila ndo njia pekee mbadala ya kukuza mtaji wako wa biashara ya mpira. Maana mchezaji naye ana malengo yake.

Zaid ya asilimia hamsini ya mafanikio ya club kifedha yako nje ya uwanja.. Pale uwanjan ni kujitangaza.

Maana yake club ikifanya vizur uwanjan.. Basi zitakuja deal za udhamin na zitakuja deal na kutaka asset zako.

Lakin wabongo bado akiuzwa mchezaj oh hamko seriuos.. Club zingekuwa haziko serious hata hao wachezaj mnaowapigia kelele msingewaona.

Hivi kuna anaejua simba au yanga wanaingia gharama kias gan kuhakikisha hao wachezaj wanakuwa na hali nzur ili waperfom.

Faida ya mchezaj mzur kwa club iko 50% ndan ya uwanja na 50% nje ya uwanja.

Maana yake akiperfom uwanjan na bado mkashindwa kupata kombe basi mnaweza mkamuuza kwa pesa nzuri, mkaboresha mara mbili ya pale.

Na bado hapo kila siku inayoenda kwa mungu haikupi guarantee ya huyo mchezaji kesho ataamkaje au atapata majanga gani.

Angalia yule mchezaj wa polisi alieumia miguu kwenye ajali.. Maisha yake ya soka yatakuwaje.. Halafu bado mnataka kubania wachezaj wakipata nafasi za kubiresha maisha.

Mchezaj mtaj wake ni mwili wake na bahat mbaya hana uwezo. Wa kuthibitisha kuwa atakuwa 100% fit hata kwa masaa 24 tu yajayo.
 
Bandiko zuri lenye afya ya mustakbali wa soka letu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…