Watanzania Na Kingereza (Ofisini na Movies)

Watanzania Na Kingereza (Ofisini na Movies)

fredito13

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2012
Posts
213
Reaction score
146
Wakuu, kwanini tunasikia vizuri sana kingereza cha kwenye movies kuliko mabosi wazungu ofisini???

Yaan kwenye movie, unasikia kila kitu, lakini ukikaa na bosi wa kimarekani ofisini, husikii kile anachoongea...unatoa macho tu. Nini tatizo hapo?

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Umenichekesha............!!

Kile cha kwenye Movie si kinaendana na vitendo ndiyo maana unaelewa haraka na sauti zimechujwa pia ili kukupa usikivu.
mzuri. Halafu hata kama hukuelewa vizuri unapotezea, au siyo? Sasa Boss kakueleza
kitu usipoelewa kijasho juu. Jaribu ku-relax utaelewa tu.
 
Plato, si utani! Fanya uchunguzi uone! Yaan kwenye movie, unasikia vizuri mbaya. Kesho unaenda ofisin, bosi anakupa majukumu husikii hata kidogo! Na tena anaweza hata asiwe bosi! Ni mzungu tu mnafanya mazungumzo...shida yake hiyo!

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Lafudhi (accent) kuna watu kama wascottish english yao ni ngumu au scousers, (liverpool people) kwahio ni kama kiswahili ukienda ndani ndani kuna watu wanaweza wakaongea kitu ikawa kazi kuwaelewa..

Lakini kwenye movies, ile ipo pale ili watu tofauti waweze kuelewa kwahio hata maongezi yao yanazingatia hilo, wanaongea kwa ufasaha..

Anyway binafsi sipati shida kuelewa wengi wao ingawa watu wa Scotland ni shida sana kuwaelewa
 
Back
Top Bottom