Watanzania na kizungumkuti cha Katiba Mpya

ASIWAJU

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2022
Posts
1,938
Reaction score
1,632
Habari za saa wanachama wenza wa Jamiiforums natumai ni wazima.

Nilikuwa na jambo linalo nitatiza na lenye kuhitaji majawabu kutoka kwenu wanachama na jambo lenyewe lina husu katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Kwa miaka ya hivi karibuni mpaka sasa hapa taifani kumekuwa na mijadala mingi ya wanasiasa kuhusu swala la uwepo wa katiba mpya hapa nchini ama la? Hali imepelekea mimi kuwaza kwa makini sana swala hili kupeleka kuni zalishia baadhi ya maswali ndani ya ubongo wangu yenye kuhitaji majawabu kutoka kwenu wanachama.

Maswali:
1. Je, wananchi wa taifa letu la Tanzania wanafahamu katiba nini au wana elimu yoyote kuhusu katiba?

2. Je, wananchi wana fahamu sababu za uwepo wa katiba ? Na umuhimu wake katika taifa?

3. Je, wananchi wana ifahamu katiba hii ya sasa ya mwaka 1977 kwa kuisoma na kuielewa?

4. Je, wananchi wana fahamu mapungufu ya katiba hii ya sasa?

5. Je, wananchi hawa itaki katiba ya sasa na wana hitaji katiba mpya?

6. Je, hitaji la katiba mpya ni la wana siasa au ni hitaji la Watanzania walio wengi?

7. Je, wananchi wana ifahamu katiba pendekezwa kwa kuisoma na kuielewa?

8. Je, wananchi wana shirikishwa katika mchakato wa katiba mpya au wana siasa pekee ndio wanao shiriki?

9. Je, wananchi wapo tayari kulipia gharama za upatikanaji wa katiba mpya? Na wapo tayari kuilinda na kuitunza endapo ikipatikana?

10. Je, upatikanaji wa katiba mpya ndio utakuwa mwisho wa matatizo yanayo wakabili Watanzania?

Hayo ni miongoni mwa maswali yanayo nitatiza kuhusu swala la katiba mpya na nafasi ya wananchi wa Tanzania katika hilo.

Karibuni kwa michango yenu.
 
MASWALI yote uliyouliza yalijibiwa na wananchi Kuelimishwa Wakati na Baada ya RASIMU ya WARIOBA ndio maana Wananchi Walitoa MAONI na MAPENDEKEZO yao YALIYOCHUKIWA na CCM na SERIKALI yake kwani yalikuwa MWIBA MKALI kwao.NAKIPONGEZA SANA Chama cha CHADEMA kwa kuendelea KUWAELIMISHA Wananchi Uzuri na Ubovu wa KATIBA iliyopo ambayo ilitungwa na Watu 20 kwa Maoni na Mapendekezo yao BILA kuwashirikisha WANANCHI ambao ki msingi ndio WENYE KATIBA .
Naomba nikuulize swali
Je KATIBA iliyopo CCM imewahi KUWAELIMISHA wananchi ?
 
Kwenye ukombozi sio watu wote wataelewa ,wataendelea kuelimishwa polepole yaani South Africa walisema waafrika wasitawale hapa south lakini Leo ni hadithi nyingine Kwa hiyo ni mchakato Tu watu wameelewa sana
 
Regarding hatuli Katiba basi TUTAFUTE kwanza chakula
Andiko halija zungumzia katiba kuwa ni chakula ni vema tutoe maoni kwa kuzingatia andiko lina taka nini na lina zungumzia nini .

Karibu kwa maoni yako tena ndugu.
 
Kwenye ukombozi sio watu wote wataelewa ,wataendelea kuelimishwa polepole yaani South Africa walisema waafrika wasitawale hapa south lakini Leo ni hadithi nyingine Kwa hiyo ni mchakato Tu watu wameelewa sana
Huo mchakato una fanyikaje na utakamilika lini ikiwa lengo la upatikanaji wa katiba mpya unaoneka haupo mbali ?
 
MASWALI yote uliyouliza yalijibiwa na wananchi Kuelimishwa Wakati na Baada ya RASIMU ya WARIOBA ndio maana Wananchi Walitoa MAONI na MAPENDEKEZO yao YALIYOCHUKIWA na CCM na SERIKALI yake kwani yalikuwa MWIBA MKALI kwao.NAKIPONGEZA SANA Chama cha CHADEMA kwa kuendelea KUWAELIMISHA Wananchi Uzuri na Ubovu wa KATIBA iliyopo ambayo ilitungwa na Watu 20 kwa Maoni na Mapendekezo yao BILA kuwashirikisha WANANCHI ambao ki msingi ndio WENYE KATIBA .
Naomba nikuulize swali
Je KATIBA iliyopo CCM imewahi KUWAELIMISHA wananchi ?
Je ni wananchi kwa asilimia ngapi katika taifa letu wana hiyo elimu ya katiba ya kujua ubovu wa katiba hii ya sasa ?.
 
Wewe mwenyewe hujui mchakato wa kutengeneza katiba Mpya
 
Hawafahamu na hawapo tayari. Wanaojua katiba nchi hii ni mawakili, wanasheria na wanasiasa.
 
Wajinga mpo wengi sana mnaishi kama kuku katiba kuijua ni kama kuijua Biblia au Quoran
 
Asante kwa maoni yako ndugu, hii mada ina paswa kuwa msaada mkubwa kwa watu wote wapigania katiba ili wajue wanacho pigania katika jamii kina tiliwa maanani ?
 
Wajinga mpo wengi sana mnaishi kama kuku katiba kuijua ni kama kuijua Biblia au Quoran
Maoni yako ni yapi ? Hayo yalikuwa maoni ya mdau naye anao uhuru wa kutoa maoni kwa mtazamo wake kutokana na maswali niliyo uliza .

Karibu kwa majawabu na maoni yako, zingatia lugha yenye staha.
 
Kwani katiba hii ya sasa tuliyonayo pindi ilipowekwa, wananchi wa ngapi walikuwa wanajua mambo ya katiba?
 
Nianze na namba 10, uwepo wa katiba mpya ndiyo mwisho wa matatizo? Hapana, zipo amri 10 za Mungu na pia zimo kwenye sheria za nchi lakini waumini ambao ndio wananchi wanazivunja wakiwemo polisi, mahakama, wabunge na viongozi wakuu wa nchi ambao ndiyo wanaozisimamia na kuzitunga sheria hizo, hata hivyo lazima tuwenazo kwa usalama wa nchi.

Kwanini katiba mpya inakwama, inakwama kwa sababu nchi imeshikiliwa na viongozi wa chama kimoja ambao wamegeuka kuwa wafanyabiashara na matajiri wakubwa, Mwalimu Nyerere aliwshi kusema nchi ikishikiliwa na viongozi ambao ni wafanyabiashara, basi twafwa, hawa watatumia kila aina ya njia iliyopo mbele yao kujilinda. Ni rahisi kupata uhuru kutoka ka mkoloni kuliko kupata katiba mpya kutoka kwao, tulishuhudia mchakato wa katiba iliyowasilishwa na jaji Warioba ulivyopigwa dafulao na chama kimoja na kuishia kugawana hela!

Nihitimishe kwa kusema kuwa unapokuwa na rais ambaye ndiye mwenyekiti wa wa chama kilichopo madarakani hatakuwa tayari kuona wenyeviti wengine wanapewa nafasi kufanya siasa, mwalimu Nyerere aliliona hili ndiyo sababu aliukataa mfumo wa kofia mbili, kuhusu wananchi japo ni muhimu kuijua lakini katiba ndiyo inawalinda wananchi kwa kila jambo nchini, yaani biashara, elimu, tiba, afya hata staha ya mtu binafsi japo wengi wanadhani ni kwa ajili ya uchaguzi wa urais tu.
 
Asante sana kwa mchango wako uliobora ndugu.
 
Wajinga mpo wengi sana mnaishi kama kuku katiba kuijua ni kama kuijua Biblia au Quoran
Kwa hiyo unadhani mimi ni mojawapo ya wajinga kwa kusema ukweli? Au kwamba mimi sijui katiba. Comment hiyo inatosha kukuonyesha najua abc to z za katiba.
Lakini sitaki kujidanganya kihisia kwamba a fair number of Tanzanian know about katiba.
Majority ya Watanzania hawajui katiba. Huo ndio ukweli.
 
Back
Top Bottom