Leak
JF-Expert Member
- Feb 22, 2012
- 52,916
- 43,505
Habari!
Pamoja na kazi nzuri iliyofanywa na serikali kujenga barabara ya njia nane Kimara-Kibaha lakini ukweli ni kwamba watumiaji wa barabara hii wananchi na madereva wameamua kuigeuza barabara hii kama machinjio!
Barabara hii kwa sasa hawezi pitisha wiki au siku tatu haijamwaga damu za watu na mara zote ajali asilimia 98.9 kwenye hii barabara husababishwa ni either na wananchi wa kawaida au madereva wa vyombo vya moto!
Madereva wa barabara hii hawazingatii alama zozote za usalama barabarani!
Madereva wa barabara hii hawajali wanaovuka hata kwenye Zebra wanapita bila kujali.
Watu wengi wanagongwa wakiwa nawavuka barabara kwa kutumia Zebra!
Madereva wa barabara hii wanaendesha gari kwa speed kubwa sana bila kujali watumiaji wengi!
Waenda kwa Miguu!
Ukweli ni kwamba waenda kwa miguu wanaotumia hii barabara hawazingatii kabisa sehemu za kuvuka hasa pale mbezi ambapo pamewekwa daraja la kuvukia, pale wengi wanavuka barabarani ambapo hawapaswi!
Watumiaji wengi hawazingatii kabisa alama za usalama barabarani na hawasikii hata wakiambiwa Watanzania wamekuwa wavivu hata kupanda ngazi kwa hiyo wako radhi kujiweka maisha yao rehani lakini wasivukie kupitia darajani!
Kwa hiyo hizi ajali zimekuwa zikisababishwa hasa na watumiaji wa barabara hizi, hasa wananchi na madereva!
Ukweli usemwe kuwa uhitaji kuwa mjuzi au mtabiri kujua kuwa kama Tanroads au Trafic hawatochukua hatua kwa wanao vuka pale mbezi stand kwa kutumia barabara badala ya daraja lazima tujiandae kwa machozi kwani sitokuja kushangaa hata watu ishirini kupoteza maisha kwa wakati mmoja!