Watanzania na tabia za kubaniana na kuzibiana riziki

Watanzania na tabia za kubaniana na kuzibiana riziki

Umkonto

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2018
Posts
2,652
Reaction score
4,593
Hii hali imeishawakumba watu mbalimbali. Hapa nazungumzia tabia ya kubaniana & kuzibiana ridhiki. Hizi tabia zinapatikana katika maisha ya kila siku katika kuajiriwa au kujiajiri. Hili limethibitika rasmi kwa kutumia sakata la Feisal.

Yaani unakuta mfano, boss anapata labda barua yako ya kwenda semina ila hakupi.

Au unakuta umeandika barua ya kuomba hela fulan ambazo ni haki yako ila boss hasaini ingawa hazitoi yeye!

Unakuta unamuomba mfanyabiashara uchangie gharama za kuagiza mzigo ili akubebe mana mtaji wako ni mdogo ila hataki ingawa nafasi kwenye gari au kontena anayo!

Huko vyuoni unakuta supavaiza anakubania kukupitia disetesheni makusudi tu baada ya kuona umeandika vizuri labda kumshinda yeye!

Sasa nawauliza wenye hizo tabia, huwa mnapata faida gani ya kumbania mtu?

Pia nawauliza, kuna ubaya gani Feisal kuhamia Azam? Kwani wachezaji wameisha Tanzania na Afrika kwa ujumla? Au ndio tabia ya Watanzania wengi kubaniana na kuzibiana riziki?

Hamjui maisha ya soka ni mafupi ndio maana Feisal kaona angalau apate hela huko Azam?

Hivi mnahisi Feisal akiendelea kukaa Yanga atashaini na thamani yake kupanda baada ya miaka mitatu ijayo?

Cha ajabu eti hadi watu na akili zao wanampigia simu mama Feisal kumtisha! Watanzania tubadilike jamani!
 
Sio watanzania sema binadamu kwa kua hiyo ni worldwide

Anyway wamekubania nini walimwengu
 
Imeandika vyema kwa ujumla wake kuhusu hiyo tabia mbaya ya kubaniana riziki lakini pia ufahamu soka ina sheria zake...tatizo ninaloliona watanzania wengi tunaongea mambo kwa ujumla wake bila kujua kila jambo hapa duniani linaongozwa na sheria....Edo kumwembe,Mhe Abbas Tarimba wameongelea vizuri sana habari ya Feisal Salumu hebu kasome au sikiliza kuna kitu utaokota
 
Kubaniana hiyo ipo toka mimba imetungwa mfukoni kwa mwanamke
Sperms huwq zinashindana ipi itaingia kwenye yai la kike
Wewe unashangaa kubaniana duniani??
Cha msingi komaa ukishakuwa mtu mnzima hakuna atakaye kufuta machonzi ni wewe nafsi yako
 
Back
Top Bottom