Watanzania ni maneno maneno na kulialia, Vitendo 0. Katiba ni maneno tu! Je, 2023 tuendeleze maneno matupu na kulialia au tubadilike tufanye kitu?


Haya yote ni sawa lakini vyama tawala Afrika ni vichache vilivyoandika katiba mpya kwa amani au kuruhusu demokrasia ya uchaguzi ya kweli kwenye nchi zao ndio msingi wa mtoa hoja baada ya utafiti na hata CCM wanavojivuta kuandika katiba mpya utaona dalili zilezile za kutaka kuharibu amani ya nchi, wanasingizia wanajenga uchumi lakini kimsingi hawajengi uchumi wowote wa nchi maana Taifa bado maskini na halina uelekeo wa kujikomboa maana tumekua tegemezi toka uhuru hadi leo tunaendelea kutegemea ajabu sana ,
 
Kaka Pascal Mayalla una akili sana nadhani kwa vile tunakuona kwa maandishi au kwa jinsi ya nje huenda ndio sababu wakati fulani tunakudhihaki. Lakini nafsi yangu inaniambia viatu vyako ni vikubwa sana, vita vyako sio vya kawaida. Tusamehe sana mkuu wangu, vile ambavyo tunakujudge vibaya kwa sababu ya yale tunayoyaona kwa nje. Mungu akulinde kaka mkubwa

Zaburi 32 : 7-8,10
Ndiwe sitara yangu, utanihifadhi na mateso, Utanizungusha nyimbo za wokovu. Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama. Naye mtu mwovu ana mapigo mengi, Bali amtumainiye BWANA fadhili zitamzunguka.
 
Unaamini kabisa katika uliyoyaandika?😂😂😂😂
 
Andiko zuri kabisa, blah blah blah blah kawaida yetu wabongo, sijui kama tutaweza kubadirika
 
Vtu vingne husindikana kufanyika au uchelewa kufanyika kutokana na uhitaji wa mda uwo nazan katiba mpya inaweza ikawa inazungumziwa sana mitandaoni lakin sio kwa wananchi na kukutana na mijadala ya katiba mpya mtaani ni mara chache sana

Nazan kwa sasa uhitaji wa wananchi sio katiba mpya ila ni uongozi imara na utakao weza kujali maslai ya wananchi na nchi kwa ujumla

Tutatukanana na kuzalauliana sisi ambao tuko mitandaoni ila ukweli ni kwamba wananchi weng bado hawajawa tayari kwa katina mpya na akili yao haioko kwenye katiba na wananchi weng badi wanaamini mattzo yao hayatotatuliwa na katiba mpya

Kuna kitu kimoja wabongo tunashindwa kuelewa asilimia karibu 80% ya watanzania hawako mtandaoni wala hawana acces ya kupata habari muhimu au izo za katiba mpya

Tuache ku ignore ukwel wachache ndo wanajua na kufuatilia na habari za katiba mpya au ata mambo ya muhimu yanayoendelea nchini ila watanzania weng hawajui wala sio wafuatiliaji na apo ndo ugumu unapo anzia

Ntakupa mfano juzi limefunguliwa bwawa la nyerere ila watanzania weng hawajui km limekamilika kwa asilimia 78% weng wanajua ni 100% limekamilika
Watz weng hawajui litazalisha umeme kiasi gan na litatumia mga gan kujaa maji na linabeba lita gap za maji na kuanza uzalishaji wa umeme watz weng hawajui na wala hawajafuatilia kujua

Km kwel tunataka katiba mpya basi wale wenye uwelewa ni muda sasa kutoka mitandaoni na kuingia mtaani na vijijini kutoa elimu kwa wananchi, tuachane na hawa wananchi wa mitandaoni ni wacache na weng habari za katiba mpya wanzazo ila wanachi wa mtaani na vijijini hao hawana

Kutegemea wasomi kupata katiba mpya itakua ni ngumu sabu wasomi weng wa Tanzania ni maskini wa kipato hawana pesa na km huna pesa huwez kua na ushawishi wala huwezi kua na msimamo
 

Bila machafuko hakuna katiba mpya ya utashi wa wananchi hasa ukizingatia chama kinachohodhi huo mchakato hakitaki katiba mpya. Kenya hapo wana katiba nzuri baada ya machafuko. Ww endelea kupiga porojo za dialogue, sijui advocacy ambayo ndio imetufikisha hapa kwenye hizi danadana.
 
Ujumbe wako umejikita kwenye "watu wa mitandaoni"!Ngoja nikuulize.Hao wa mitandaoni wanaishi nchi gani?Ina maana watu wa mitandaoni wapo mbali sana na wanaoishi kule nchini Tanzania kiasi cha kwamba wameombwa wawasemee au wanajisemea vitu vya nchi isiyowahusu?Weye unaishi mitandaoni au ni ileile nchi wanayoitaka katiba mpya?Hesabu ya wananchi wanaoishi nchini wasioitaka katiba mpya na wanaoishi mitandaoni uliipata kwa njia ipi?
 

Kwahiyo jambo linafanyika baada ya watu wengi kulijadili? Nijuavyo jambo linafanyika kutokana na umuhimu wake na sio kwasababu watu wengi wamelijadili. Mfano maVX/R yananunuliwa sana na serikali, je wananchi wote unawakuta wakiyajadili umuhimu wake? Kwa maneno marahisi wananchi watachukia sana iwapo katiba mpya itapatikana wakati hawajawa tayari? Acheni upotoshaji wa kijinga.
 
Kisha utaibuka tena kwa ticket ya CCM kuomba ridhaa ya uteuzi kugombea ubunge🤣🤣🤣 na watu wakuamini kuwa uko independent kifikra na kitaaluma hasa katika sekta ya habari na udunduizi!!!?
 
Kaka Pascal hebu jaribu ukipata audience na Rais HASSAN, Samia muulize swali kama ulilomuuliza Ndugu Dr.Magufuli uone utakavo shambuliwa kama Sukuma Gang, kwanza atakavyo kushambulia ni kama umerusha nyuklia
 
Katiba ni mpaka pale mwenyekiti wetu atakapotaka bwashee
 
P,kwanza nikupongeze kwa kukaribia kuuaga mwaka na kukaribia kuukaribisha mwaka mpya,pia nikupe pole kwa kuchelewa kubaini kama wabongo ni watu wa maneno mingi mingi na vitendo 0.kukusaidia tu, Watanzania ni walking dead,Taifa langu ni walking dead kwa Tabia za mazoea na janja janja.
 
Katiba MPYA itapatikana siku wananchi wenyewee watakapoitaka. Mchakato wakati a umeathiliwa na migongo ya matakwa ya vyama vya siasa ndio MAANA halina mvuto wowotee. Vyama siasa vikazanie katiba za vyama vyao na siokatiba ya wananchi ambao wengine sio wanavyama vya siasa. Katiba ya wananchi itafutwe na wananchi wenyewee wasio na mgongo wa chama chochote Cha kisiasa, ili tupate katiba itakayosimamia vyama vyote vyasiasa Kwa maslahi mapana ya Taifa.
 
Mkuu nashindwa kuamini kauli zako. Hivi inawezekana vipi katiba inayokupa ulaji uje kuichallange.
Anyway, paragraph ya mwisho imeeleweka.
 
Ahsante mtoa mada
Kwa hali ya nchi yetu Dola ina nguvu sana na wabongo are very docile.
Kila mtu anapaswa kuwa mwl wa jirani yake kuhusu umuhimu wa katiba mpya ili tupate mass response na kuweza kushinikiza wenzetu ambao wanasema katiba sio kipaumbele waone urgency of it's accomplishment
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…