Watanzania ni wanafiki Vs Diamond Platinumz

Nedago

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2018
Posts
908
Reaction score
1,350
Salaam Wakuu.

Tukiachana na ishu ya lowassa kurudi ccm,maana si mwanaharakati na ameshindwa mikikimikiki ya kule,maana kazeeka tayari kule kuna hitaji damu ya moto inayotembea kwa speed Sana sio yeye,kwaio kashindwa kaona arudi kwa wazee wenzie kwenye maisha simple.

Wakati tukiendelea na maombolezo ya ndugu yetu boss ruge,kuna mengi yametukia na ya kushangaza Sana,

1.Clouds media wameonesha nguvu yao katika promo na kufikia kuonesha kuwa msiba huu ni wa kitaifa,na kulazimisha kila mtu aonekane kaguswa,msiba uko very over rated.

2.Tumeona wasanii na watu wengi wakijifanya kuguswa na kifo cha marehemu na kuposti kwenye social medias lakini hadi sasa hawajagusa msibani kwa Ruge,wengine wapo dar hapohapo,Why?

3.Lakini tumeona wasanii,wanasiasa,wadau na hata wananchi wa kawaida wakimnyooshea Sana vidole diamond platnumz Pekee,kwamba kwanini hajaposti neno R.I.P ruge tangu first day, wakati wengine wamefanya hivyo,na wamesahau kuwa msiba haujaisha.why diamond na sio wengine mfano jide?

4.watanzania ni wanafiki Sana,wakati Cloud's media kupitia ruge wakifungia nyimbo za diamond na Kuanzisha vita na wasafi walikuwa wapi kuzima bifu lile na kumshauri ruge na media ile,kuacha ile tabia ya Kuanzisha bifu na diamond?

5.Endapo nguvu hii ya kumuita diamond msibani ingetumika kuwakemea Cloud's fm zidi ya chuki zao,inawezekana Leo diamond angekuwa kisha posti R.I.P, au watanzania hawa hawa walikuwa hawajui hayo? Au ni kwamba clouds wanahaki sana kufanya wanachojisikia na kuachwa na si diamond na wasafi kiujumla?

6.wadau wajifunze kukemea uovu na vita Kama Hivi,maana nguvu hii iliyotumika ingetosha kuwaogopesha Cloud's na wangepatana na diamond,lakini walikaa kimya utazani hawapo au diamond alikuwa hana haki ni clouds tu wanapaswa kuabudiwa na wote? Au ruge R.I.P na Cloud's wanaogopwa kusemwa Au social media hazikuwepo?.Na kuna baadhi ya wasanii walifurahia ban ile kwa wasafi wakijua jamaa atapotezwa wabaki wao,maana anawatesa kawaacha mbali.

Watanzania ni vema wakakaa kimya juu ya hili maana walishindwa kuwapatanisha marehemu akiwa hai,diamond aachwe afanye kadri atakavyoguswa.

The Future is in Our Brain,Tongue's&Hand's.
 
Ruge licha ya kunyanyasa wasanii wa kike kingono ila jamaa alijitahidi sana kuua vipaji vya wasanii wengi hapa nchini, nashangaa leo amekufa watanzania wanajifanya wana huzuni na kumfananisha na hero wa nchi wakati he is none of that. Huu ni unafiki wa hali ya juu sana.
 
Watu mbona mnakuwa wajinga!?? Huwezi kulinganisha huyo fala unayemtetea mwenye bifu na Baba yake mzazi unamlinganisha na Jide!??. We umeona hapa tu,subiri hata siku akifa Baba yake na siku akifa yy ndo utajua km watanzania ni wanafiki au hapana.

Jide alishasema msimamo wake kuhusu Ruge rip na Jose kusaga. Na alitoa msimamo huo tangu 2013 na thread yake ipo hapa jf. Na alishasema hata yy akifa,mbali na kutohudhuria msiba wake,hata nyimbo zake tu,clouds wasipige kabisaa wakati wa msiba wake. Na ameturuhusu tukimuona Jose kusaga au Ruge R.I.P. kwenye msiba wake tuwapopoe mawe.

Hebu tuonyeshe hapa msimamo wa diamond kuhusu Ruge...na Jose kusaga. Diamond ndo mnafiki,anamchukia Ruge wakati anashirikiana na kusaga,hv Ruge kuna kitu alikuwa anafanya bila kusaga kujua!?? Ndo maana jide kawataja wote tena kwa majina. Usimlinganishe Jide na vitu vya kijinga bhaana!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwaiyo unataka diamond apost mtandaon msimamo wake? Au akufate wewe akwambie mambo yake?? Kwan lazm? Kufanya hivo... Hii inaonyesha diamond ni mkubwa kuliko ruge

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza nani aliyesemamisiba iko mitandaoni kwa kupost R.I.P?
Hili anafanya yeyote hata kwa ushabiki tu,ili mradi naye amepost na kuonesha yupo current na haina maana ameguswa

Pamoja na hayo,kama akiamua kumaliza chuki iliyokuwepo(ikiwa mwenzake katangulia mbele za haki) ni busara kwake na kuonesha ukomavu kifikra.

Pia kutopost kwake hakuathiri lolote kwake wala kwa marehemu labda jamaa zao.

NB.Wakati mwinginetujifunza kufanya mapatano na kuishi kiungwana kabla ya story za maisha yetu kubadilika na kuwa tayari tumechelewa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwani uyo diamond asipo post RIP ndio kwamba uyo ruge hata enda mbinguni kwan diamond ni mungu acheni mada za diamond kila time maana huyo diamond hana tofaut na binadamu wengine

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo ruge aliejifanya mungu mtu mwisho wa siku yuko wapi? alifanya yake kwa wenzie enzi za uhai wake,,acha na upande ulioumia ufanye yao punguza povu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uko sawa mkuu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaweza ukapost instagram na ukaenda kuzika,lakini kama moyoni mwako bado una kinyongo ni kazi bure mbele za mungu,ila kwa wanadamu utaonekana wa maana,Usikute kuna watu wamepost na msibani wameenda lkn bado moyoni mwao wana vinyongo.
 
Umeona mkuu.

The Future is in Our Brain,Tongue's&Hand's.
 
Ishu ya baba yake ni la kifamilia zaidi.

The Future is in Our Brain,Tongue's&Hand's.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…