Maybe he mean't to say wamealikwa lakini hawajatokea.Or wamealikwa,wamekwenda(na kula pesa za kujikimu) LAKINI hawana muda wa kuonyesha chochote kwenye banda lao.
Jamani...labda tuangalie kidogo mpangilo wa hii mikutano.
Mikutano hii ya kimataifa, siyo kama mkutano wa wanachama wa club ya...... mpangilio wake ni tofauti sana.Inakuwa kama hivi:
1.
Plenary - hili ni jumuiko kubwa la waliohudhuria mkutano na wanaweza kuwa kwa mamia kama siyo maelfu.Kwa kawaida hapa ndio utaona watu kama viongozi wa msafara ( mawaziri au viongozi wengine wa taasisi mbalimbali including NGOs), wataalamu wengine nk wakitoa speech zao, na statements na kutoa mada zilizopangwa kwenye ratiba
2.
Side meetings/Caucuses/workshops - hii ni mikutano inayoendeshwa sambamba na mkutano mkuu. Mara nyingi hii huwa na themes mbalimbali na watu huchagua wanataka kuhudhuria ipi.
3.
Maonyesho/exhibitions - haya maonyesho hufanywa na washiriki kuonyesha mambo mbalimbali ikiwemo machapisho, n.k.
NB: Ni vigumu sana kuweza kujua kama Tanzania tumeshiriki vipi katika kila level maana hii hutegemeana na ukubwa wa delegation iliyoenda huko.Ninafahamu kwa mfano Tanzania tuna washiriki kutoka Serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali ya ndani na nje ya nchi.Na najua baadhi wako kwenye ratiba ya kutoa mada katika maeneo mbalimbali.
Kuhusu kufanya shopping wakati mkutano unaendelea, hili siyo tatizo la watanzania peke yao. Hata washiriki kutoka nchi nyingine na siyo za kiafrika tu hapa za ulaya hufanya hivi japo wazungu siyo sana kama waafrika. Mjue kuna kitu kinaitwa " conference tourism' hii ni fursa mtu huipata kuona nchi nyingine akiwa anahudhuria mkutano ughaibuni na kwa wale walioko kwenye tasnia ya utalii watanielewa naongelea nini. Ni kama WC ilipokuwa inaendelea ( japo havifanani sana) mtu anaenda kuona mechi lakini hapo hapo anachukua fursa ya kuwepo huko kuona vivutio vingine ikiwemo kufanya shopping.
Huko Vienna ni zaidi ya AIDS CONFERENCE 2010 - NI BIASHARA KUBWA inaendelea - madukani, mahotelini nk na ndio maana nchi hugombea ku host mikutano maana ni njia moja wapo ya kufanya biashara na kuingiza pato.