Watanzania ogopeni dhambi za sirini

Watanzania ogopeni dhambi za sirini

Yesu Anakuja

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2019
Posts
12,675
Reaction score
25,924
Luka 12:2 Lakini hakuna neno lililositirika ambalo halitafunuliwa, wala lililofichwa ambalo halitajulikana.

Mnadhulumu haki za watu, mnauwa kwa ujambazi, kwa visirani, ugomvi wa kisiasa na sababu mbalimbali. Jueni hakika kwamba, yupo Mungu aonaye sirini, mnafanya mkiwa mmejificha, mnafikiri hamuonwi, Mungu anawaona, na hapendi mnachofanya. sio lazima iwe ni siku ya mwisho ya hukumu, hata kabla ya hapo, machozi ya victims na damu zao zinalia mbele za Mungu, naye Mungu atashuka kuwatetea, na hakika atawatetea, hakuna chozi liliwahi kufika kwa Mungu asishuke kutoa haki. MWOGOPENI MUNGU.

Kwenu ninyi mnaojifanya mnasali, fanyeni vitu toka moyoni, Yesu alikataza unafiki, msiwe wanafiki wa kujificha kwenye dini, Mungu anaona moyo, anaona zaidi ya mavazi yenu ya dini, simameni upande wa haki, huo ndio upande wa Mungu kwa sababu Mungu ni wa haki na haki yakaa ndani yake.

Dhambi za sirini zitawakosesha wengi uzima wa milele,na watu wengi hasa tuliokoka tunajitahidi sana kuwaficha wanadamu maovu hayo ya sirini tukiwaza kwamba tunapowaficha wao tupo salama pasipo kujua tunajiweka katika hatari kubwa na hasara ya milele.

Ndugu lazima ujue ni kweli utajitahidi kumficha huyo mwanadamu uwenda ni baba/mama/mchungaji/ndugu zako wa kiroho ila ujue fika hao unao jitahidi kuwaficha hawana mbingu ya kukupeleka maana hata wao watasimama mbele ya kiti cha hukumu kutoa hesabu ya maisha yao siku ile.

Kila jambo lolote la siri liwe ovu au jema Mungu atalileta hukumuni siku ile kwa wazi kabisa na ndipo sasa itakuwa aibu na kudharauliwa milele na kilio cha milele. Tunapaswa kuutimiza wokovu wetu wa kumuogopa Mungu na si wanadamu, tumuogope Mungu ambae huyo ana uwezo wa kuangamiza mwili na Roho katika Jehanamu ya moto....

Unapojikuta umemkosea Mungu fanya haraka sana kurekebisha na Mungu na usitumie njia yoyote kuficha uovu wako kwa wanadamu na kuendelea kulea dhambi uwe uhakika dhambi hizo unazoelea huko sirini jua moja zitakutenga na Mungu milele.

Baaada ya kuanza mahusiano yasiyo rasmi na huyo kaka ndani ya kanisa la Mungu huku mkisema mmeokoka, mkaanguka katika uasherati wenu, hadi mimba ikatokea matokeo yake mkaona isiwe kesi dawa ni kutoa mimba ili mbaki kuitwa kaka sayuni na dada sayuni kweli mkafanikiwa uovu wenu ni kweli mmefanikiwa kuwaficha wanadamu ila Mungu wetu aonae sirini yeye afichwi jambo, badala kumgekia Mungu kwa toba ya machozi na kuvunja hayo mahusiano yenu bado mmezidi kudumu katika uovu wenu mkijifariji ilitokea bahati mbaya, Pasipo kujua ni wema wa Mungu tu unawavuta mpate kutubu, lasivyo mngekwisha katiliwa mbali ni huruma za Mungu tu.

Kwenu ninyi mliookoka, ogopeni dhambi za siri, ukitenda dhambi kimbia katubu haraka kabla haijakutafuna.

Wokovu wetu tulioupata ni wa thamani kubwa sana, ni lazima tuutimize kwa kumuogopa Mungu wetu, na si habari ya kuwaza juu ya mtu fulani akijua itakuaje, tuwaze juu ya Mungu kwanza, ambae ndie mwenye mbingu ya kutupeleka.

Tuache kuishi maisha ya pande mbili nuruni tuko kwa Mungu ila sirini tunayofanya yanatisha ni afadhali hata na mpagani asiye mjua Mungu, neno moja ni hili vuguvugu wote watatapikwa,amua leo kuwa baridi au moto, kama umeamua kuokoka, okoka kwelikweli simama imara acha dhambi zote sirini na hadharani usije kulia kilio cha kusaga meno siku ile watu wanakuona umeokoka leo ila siku ile unakataliwa nakuhesabiwa miongoni mwa waovu inatisha kama nini!!!!!!!!
 
Haya mambo si Mungu tuu hapendi hata Wanadamu wengi hawapendi na Bahati Nzuri serikali na Sheria zake pia hawapendi haya yatendekayo,ila wapo wayatendao wakiwa serikalini huku wakila viapo vya dini zao na kumtajaMungu na kutenda kinyume chake!
 
Back
Top Bottom