Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
TRL sasa kuongozwa na Watanzania asilimia 100
• Waziri mpya wa uchukuzi aponda menejimenti ya Rites
na Betty Kangonga
WAZIRI wa Uchukuzi, Omary Nundu, ameahidi kuishauri serikali kufanya haraka mchakato wa kulirejesha Shirika la Reli Nchini (TRL) chini uongozi wa wazalendo ili waweze kulifufua.
Shirika hilo lilikuwa likiongozwa kwa ubia na menejimenti ya kampuni ya Rites ya India iliyokuwa na hisa ya asilimia 51 na serikali ya Tanzania iliyokuwa na hisa ya asilimia 49.
Akizungumza na wafanyakazi wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana, Nundu alisema inasikitisha kuona shirika hilo linazidi kudorora kila kukicha huku likionekana kama halipo.
"Mmekuwa wavumilivu na wachapakazi hata kwa mazingira yaliyopo maana kwa muonekano wa wazi shirika kama halipo maaana hatuwezi kuwa na safari moja tu kwa wiki kwa shirika kama hili!" alishangaa.
Alisema makubaliano ya kuvunjwa kwa mkataba yalikwishafanyika na serikali inaendelea kuweka mikakati ya kumalizana na wabia ambapo muda si mrefu kampuni itaendeshwa na Watanzania kwa asilimia 100.
Waziri Nundu alisikitishwa na hatua inayofanywa na menejimenti ya Rites ya kuendelea kukusanya mapato huku serikali ikiambulia patupu.
"Ninashangaa kama kweli jambo hili linafanywa na kuwa kimya, sisi ni wazalendo….hii ni nchi yetu tuwe wazi na kueleza yale yanayotendeka," alisema.
Alisema ni muhimu kuangalia mikataba inayofanywa na serikali na kuichunguza kwa upana ili ikitokea mwaka wa kwanza kampuni iliyoingia ubia inazalisha kwa hasara basi kuwepo na njia nyepesi na za haraka za kuchukua.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Reli (TRAWU), Sylvester Rwegasira, alisema kuwa alichokifanya Waziri Nundu ni kutoa ahadi na yatathibitishwa hayo baada ya kero hizo kuondolewa.
"Tutaendelea kupiga kelele na muelewe kuwa kila tunapoamka shirika hili linaendelea kufa hasa ukiangalia suala hili la fedha ambazo wenzetu wanazikusanya na zinaingia katika mifuko yao. Tunaomba serikali ichukue hatua za haraka sana," alisema.
Hata hivyo, wakitoa maswali yao kwa Waziri Nundu, Elizabeth Msemo wa Idara ya Masoko alisema hali ya mabehewa inatisha jambo linaloonyesha kuwa Watanzania wako katika kipindi cha ukoloni maana abiria wamefikia hatua ya kufa ndani ya mabehewa kutokana na kukosa hewa.
Aidha, waziri huyo alikaribishwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali likiwemo la "Hapa kama Ivory Coast, menejimenti 2 moja ya Rites na nyingine ya serikali je hii sawa?"