Watanzania: Shikamooni Wakenya, nyie ni wakubwa.

PowerWithin

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2014
Posts
646
Reaction score
501
Wakenya Shikamooni!

Tukiacha hizi ligi zetu za jadi, wenzetu hawa wapo mbali sana na sisi walau kwa maeneo matatu muhimu na makubwa sana kwa mustakabali wa Taifa. Kama eneo la elimu, uchumi na siasa. Maeneo hayo yanaleta kitu kinaitwa 'multiplier effect' kwenye Taifa lao. Japo leo tunawapongeza kwa upande wa siasa.

Angalia namna wanavyodili na changamoto za general election yao. Wapo open, wapo humble, wapo pure honest ukiachilia mbalil changamoto za kawaida za ushindani wa kiuchaguzi.

Kuna baadhi wanang'ang'ania suala la kuawawa IT manager wa IEBC. Hili limeleta dosari kwa namna fulani, lkn kupitia forms 34A na 34B naona hili wanalitatua bila matatizo. Ustaarabu huu katika medani ya kisiasa si ya kawaida sana katika Africa hasa Tanzania yetu ambapo Chama pinzani na wana harakati hawaruhusiwi kuwa na Tallying Centres mbali ya kufanya siasa tu za majukwaani.

Nini kilichowafanya hawa jamaa watuzidi? Kwa mtazamo wangu ni mfumo wao wa elimu. Nadhani ukilinganisha mfumo wetu wa elimu na wa kwao wa kwetu umekaa kibabaishaji zaidi yaani mfumo usiokuwa na real vision.

Jambo hili ndilo lililowapelekea kudai tume huru na katiba mpya, wakati huku kwetu wananchi wanaomba kutoka chama tawala wapewe katiba mpya na tume huru. Kenya ni tofauti sana na sisi. Tumewakubali sana.

Leo hawa jamaa soon and very soon watakuwa level moja na South Africa both Kisiasa, Kielimu na Kiuchumi. Sioni kitakachowakwamisha maana hata manyang'au wachache mfumo wao unawathibiti. Sisi tunawatakieni mema.

Wana changamoto moja eneo la usalama. Lakini juhudi wanazozifanya are quiet promising. And we wish them good luck.

Nionavyo, sisi kufikia level ya sasa ya wakenya sijui lini kwa mwendo huu tunaoenda nao sasa.

Again, shikamooni wakenya.
 
Kuna uhsiano mkubwa wa IQ ya binadamu na eneo analopatikana binadamu husika.

In other words,Human Intelligence Quotient is a function of the Region where that particular human being is or can be found.

Kadri unavyo-move kwenda kaskazini mwa bara letu ndivyo IQ ya binadamu invyoongezeka, maarifa,uwezo wa kufikiri,uzalendo,n.k ingawa kuna some exceptions kidogo.

Ndio maana wamisri na wanaigeria huwezi kuwalinganisha kimandeleo na watu wanaoishi kusini mwa jangwa la sahara


Ni sababu hiyo hiyo inayowafanya wamisri, wamorocco,waalgeria,n.k wawe na maendeleo yanayofanana na watu wa mataia ya Ulaya wanayopakana nayo as you move futher north.
 
Usisahau na wizi pia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Elimu yao ni ya kawaida sana kama uliwahi soma shule za st.mary's ,ndo utanielewa mpaka vitabu ni vya kenya hata walimu ni toka kenya, jamaa wapo hivyo sababu ya hali yao ya maisha ni ya kibepari ndo mana jamaa ni aggressive kwenye kila kitu
 
That is stupid analog.. and if that is the case, you're a case control kwa upande wa watu wa kusini mwa jangwa
 
Mbona South Africa, Mozambique, Zimbabwe, Namibia na Angola walioko kusini wako juu tu kimaendeleo mkuu kutuzidi sisi 'wapumbavu wa ccm' tulio kaskazini kuliko wao?
 
Mleta mada umechambua vizuri sana juu ya hao jamaa na mafanikio yao.

Ulipokosea ni kuwaamkua SHIKAMOO. hapo HAPANA kabisa!!
Labda uwe hujui maana ya hilo neno, kama unajua basi usitujumuishe Watanzania wote, wasujudie kivyako na endelea kukaa chini ya miguu yao.
 
Walikuwa kama sisi before 2007 ila baada ya pale kila mtu alijua kushika adabu.
Sisem itokee kama ile hapana ila we can have better ways kama ilivyotokea Ghana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…