Watanzania sijui nani katuroga

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Kwa matukio kama haya ambayo nitayaorodhesha hapa acheni tu Watanzania tuchekwe kuwa tuna mapungufu makubwa ya Kufikiri na kwamba kupata Maendeleo itakuwa ni ndoto na labda inabidi tukae chini tutafakari ni nani ametoroga....
  1. Zanzibar imefutiwa Uanachama wake CAF badala ya kulaumiwa Viongozi wa ZFA au Sisi Watanzania wenyewe kwa wenyewe sasa lawama zetu zote tumezihamishia kwa Rais wa CAF Bwana Ahmad Ahmad.
  2. Klabu ya Simba inasajili Wachezaji kwakuwa tu wamecheza vizuri ndani ya mechi moja na kupata Tuzo.
  3. Klabu ya Yanga inasajili Mchezaji kwa Kigezo tu katika mechi moja huyo mchezaji aliweza tu kung'aa na kumpiga chenga nyingi Himid Mao na Salum Abubakar ' Sure Boy '.
  4. Singida United wanasajili si kwa kuweza kufanya vizuri katika Ligi Kuu ijayo ya VPL bali kwa kuja tu kuzifunga Simba na Yanga.
  5. Klabu ya Kagera Sugar ina uwanja wake wa Nyasi bandia wa Kaitaba ambao unafanana kwa kila kitu na huu wa Karume lakini wametoka Mkoani Kagera kuja kufanya mazoezi Mkoani Dar es Salaam.
  6. Klabu ya Ndanda ya Mtwara hadi hivi sasa inajipanga kuanza Pre Season yake lakini haijui Kocha wake aliyewasaidia kuepuka kushuka daraja yupo wapi.
  7. Msemaji wa Mtibwa Sugar anasema kuwa wao Mtibwa furaha yao ni kubaki tu katika Ligi Kuu ya VPL lakini hawana hata haja ya Ubingwa.

Kwa upuuzi / upupu huo wa hapo juu ndiyo maana sasa nataka kuachana tu rasmi kushabikia mpira wa Bongo ( Tanzania ) na nibaki tu kushabikia Timu zangu zinazojielewa Liverpool FC ya Uingereza, Borrusia Dortmund ya Ujerumani, FC Barcelona ya Hispania, AC Milan ya Italia, Paris Saint Germain ( PSG ) ya Ufaransa, River Plate FC ya Argentina, Corinthians FC ya Brazil na Kaizer Chiefs ya Afrika ya Kusini.

Nawasilisha.
 
Jamaa una timu nyingi za kushabikia, yaani huna stress kabisa weee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hatuwezi Mpira..Tutafute wachezaji wa nje tuwape uraia...Samatta peke yake ndio anafaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…