Watanzania siku zingine ‘ Wagonjwa ‘ kama hawa ‘ Wabishi ‘ na ‘ Viburi ‘ ni wa kuwaacha tu ‘ Wafe ‘ ili wengine wajifunze

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Wewe tumekuambia mapema sana kuwa tibiwa Hospitali ya Muhimbili Mkoani Dar es Salaam utapona haraka dhidi ya Ugonjwa wako wa ‘ Pyramid Mwarabu Fever ‘ ukatuona wenye Akili akina GENTAMYCINE ni ‘ Mapopoma ‘ na ukasema kuwa unataka kwenda Kutibiwa Hospitali ya Bugando Mkoani Mwanza ambapo sasa badala ya Kupona ndiyo Kwanza Ugonjwa wako umeongezeka mara Mbili nzima na kusababisha tatizo kuwa Kubwa na Kutuongezea Gharama za Matibabu.

Kwa Ubishi na Kiburi chako sasa Madaktari wa Hospitali ya Bugando uliowaamini sana na Kuwatukuza huku ukisema kwakuwa Mwanza ni Kwenu watakuponesha na ukawadharau Madaktari Bingwa wa Muhimbili wameushindwa Ugonjwa wako huo ‘ Sugu ‘ wa ‘ Pyramid Mwarabu Fever ‘ ambapo sasa umetuongezea Watanzania gharama za kwenda Kutibiwa huo Ugonjwa wako Cairo nchini Misri ambapo kwa jinsi Ugonjwa wako ulivyofikia hatua za mwisho tuna uhakika hiyo Siku yako ya ‘ Oparesheni ‘ tarehe 3 November 2019 ‘ utakufa ‘ tu hivyo kuanzia sasa Watanzania tunaanza Kuandaa ‘ Mazishi ‘ yako rasmi.

Kuna Watu ‘ Mapopoma ‘ kweli hapa duniani. Yaani Wewe kabisa madai yako eti unamkomoa ‘ Mwarabu ‘ kwa Kumtoa Dar es Salaam na Kumpeleka Mwanza katika Uwanja wasiouzoea na ulioko mbali na Kwako hapa na Wao kwa Kukuonyesha dharau na jeuri wamekuja na Ndege yao ‘ Maalum ‘ wakatua zao tu Dar es Salaam kuweka Mafuta na wakakufuata hadi Mwanza huku ndani ya Ndege yao muda wote Wachezaji wakiwa wanacheza zao tu Karata na Wewe ukiwa CCM Kirumba muda mwingi ‘ Unaroga ‘ na Kuvunja Nazi njia panda huku ukifanya ‘ Mikafara ‘ ya Ajabu na ya Kufa Mtu na bado Mwarabu ‘ amekubikiri ‘ hapo hapo CCM Kirumba.

Tukiwa tunawaambieni kuwa Mwinyi Zahera siyo Kocha bali ni ‘ Samjo Samjo / Tapeli Tapeli ‘ hivi mnadhani huwa tunatania au kwakuwa Sisi ni wana Msimbazi basi tunachuki na nyie wakati ukweli ni kwamba wakati mwingine huwa tunaweka Utani pembeni na Kuongelea mambo ya Kiufundi. au mnadhani na akina GENTAMYCINE hawakucheza Mpira miaka yao? Tena huenda wengine tungeendelea Kucheza Mpira leo tungekuwa hata Liverpool FC huko au Barcelona sema tu Wazazi wetu wengine walikuwa ni ‘ Wakoloni ‘ na waliweka mbele Taaluma huku wakitupiga mno ‘ Mikwara ‘ ya Kutulaani kama tutaacha Masomo ( Shule ) na Kucheza Mpira ambao kwa miaka hiyo ulikuwa haulipi nchini.

Kocha yoyote mwenye Akili timamu kamwe hawezi Kumuanzisha Abdallah Makame na Feisal Salum katika Kiungo wakati nje ana Watu kama akina Sibomana na Banka ambao kwa Mechi yenu ilivyokuwa wangeweza ‘ Kukichafua ‘ vizuri mno pale katikati na ‘ Waarabu ‘ wasingefurukuta kabisa. Yaani Mechi muhimu kama hii unawezaje kuwa na ‘ Lone Striker ‘ kama Sidney wakati una Uwezo wa Kuchezesha ‘ Double Strikers ‘ Balinya na Sidney huku ‘ Fundi ‘ Sibomana akiwa ‘ anawalisha ‘ tu vyema na huenda hata matokea yasingekuwa kama haya mliyoyapata kwa Kujitakia na kwa ‘ Upopoma Uliotukuka ‘ wa Kocha wenu ambaye ‘ anawagharimu ‘ na bado tu mnang’ang’ania utadhani ‘ amewarogeni ‘ hizo Akili zenu.

Na mtazidi ‘ Kuchanganyikiwa ‘ zaidi kwani wakati mkijiandaa kwenda Kupokea Kapu lenu la Magoli huko Kwao nchini Misri huku katika Ligi Kuu ya Vodacom ‘ Mume Wenu ‘ Simba Sports Club Yeye ndiyo Kwanza anazidi tu ‘ Kuziokota ‘ alama zake na kuziweka ‘ Kibindoni ‘ na mpaka Wewe ukirudi na Kujikita katika Ligi Kuu hii huku ukiwa ‘ umeshajichanganya ‘ kwa Kutolewa huko Shirikisho na ‘ Mgogoro ‘ mkubwa ukiibuka hapo Jangwani mtashtukia tu Simba Sports Club ‘ anatawazwa ‘ kwa mara ya Tatu kuwa Bingwa wa Vodacom Premier League kwa Msimu huu wa 2019 / 2020 huku mkibaki ‘ Kujifariji ‘ na Kauli zenu zile kuwa Simba Sports Club ‘ inabebwa ‘ na TFF kwakuwa TFF hii imejaa wana Simba watupu.

Wewe eti mpaka Profesa Lipumba ( tena akiwa kavalia Tshirt Form Six ambayo ni Oversize kabisa ) nae Siku zote hajawahi Kuingia Uwanjani Kuishangilia Yanga SC pamoja na Yule Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama fulani hivi ( ambacho hakichoki Kutawala ) huku Msanii Asley nae akiwemo tena akiwa amevalia ‘ Hereni ‘ Sikio lake la Kushoto huku Mashabiki wenu wengine wakivalia ki Kike Kikewakati ni Wanaume kabisa leo nao wakiwa ni sehemu ya Watu walikuja Kuwashangilieni pale CCM Kirumba mnadhani kwanini msifungwe? Nuksi mmeitafuta wenyewe na wala msimlaumu Mtu au msitafute sijui Mchawi.

Ahsante sana Mwarabu Pyramids FC leo Watanzania wenye Akili tunalala kwa Amani na Mji umetulia tuli wengine wakilia tu.
 
kuandika mada ndefu halafu pumba zote, ni ujinga.
 
Pamoja na muandiko wakukera wamauzi Kuna ka ukweli ukweli furani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…