mpimamstaafu
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 4,445
- 4,707
Hakika inaonekana Watanzania tulio wengi hatukuelimishwa vya kutosha Majukumu ya mfumo wa siasa vya vyama vya upinzani wakati vinaanzishwa.Nadiriki kusema hivyo kutokana na watu wengi wanalaumu uwepo wa vyama vya upinzani na kuvilaumu eti vinapinga kila kifanyacho na chama tawala.Kibaya zaidi kundi kubwa linalovilaumu vyama vya upinzani ni wasomi wetu ambao binafsi naamini kwa upeo wao wa elimu wasingeshangaa vyama vya upinzani kukipinga chama tawala.Hata huko Marekani kwenye demokrasia chama cha Upinzani cha Demokrasi kinapinga yote yafanywayo na Republican iweje leo vyama vya upinzani kuipinga ccm kionekane kitu cha ajabu.Kama kuna chama cha upinzani kinaunga mkono chama tawala basi hicho chama hakina nia ya kutawala.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app