SoC03 Watanzania tuache kupotoshana kuhusu Serikali yetu

Stories of Change - 2023 Competition

hassan yahaya

Member
Joined
Aug 27, 2022
Posts
35
Reaction score
37
Kupotosha ni kitendo cha mtu kutoa taarifa au kuzungumza kitu katika hali isiyo sahihi na kupelekea wanaomsikiliza kukosa uhalisia wa jambo. Leo hii nchini Tanzania kumezuka tabia hii ya upotoshaji katika mambo mbalimbali ikiwemo mambo ya utawala wa serikali.

Kutokana na kuwepo kwa upinzani mkubwa kati ya vyama vikubwa viwili ambavyo ni chama cha Mapinduzi ( CCM ) na chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) mambo mengi ya serikali yanayopingwa au kuzunguzwa vibaya inaonekana kuwa CHADEMA ndio wahusika ila ukweli ni kwamba nchini kwetu kila mtu anajioa uhuru wa kuongea na anaongea apendavyo. Mfano leo hii ukiangalia taarifa mbalimbali kuhusu teuzi za serikali au mikataba ya serikali sehemu ya maoni wapo wanaopinga na wapo wanaounga mkono.

Kupinga na kuunga mkono sio kosa ila kosa linakuja mtu kutoa taarifa au ufafanuzi usiokuwa sahihi mfano katika mkataba huu wa hivi karibuni kuhusu bandari kuna mtu katoa maoni yake kwamba kutoka na kukubaliana na mkataba huo basi nchi yetu itarudi katika kutawaliwa yaani biashara ya watumwa itarudi tena, jambo ambalo si kweli kwani serikali yetu ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania inafanya mambo kwaajili ya maendeleo ya taifa na sio kuikandamiza nchi au kuwakandamiza wananchi.

Sote tunatambua kuwa nchini kwetu wapo watu wanaofatilia maswala ya kisiasa na utawala na wasiofatilia lakini pia wapo ambao wanaelimu kubwa na wenye elimu ndogo hivyo kama mpotoshaji atakuwa ni mtu mkubwa serikalini basi ataketa mkanganyiko mkubwa kwa wananchi na kufanya wananchi kupoteza imani kwa serikali.

Kwa mfano kipindi cha raisi wa awamu ya tano Dkt John Pombe Magufuli wapo watu walipotosha sana jamii mfano kuhusiana na suala la kununua ndege, hata ilipofika kipindi cha janga la uviko 19 pia wapotoshaji walikuwepo, hata kifo chake Magufuli wapo waliozusha kuwa amefariki kwa uviko 19 japokuwa aliyekuwa makamu wa rais Dkt Samia Suluhu Hassan aliweka bayana juu ya kifo cha raisi wetu.

Watanzania kwanini tunafika huko? Sisi sote ni wamoja hakuna mwenye nia mbaya na mwenzie basi tuaminiane. Viongozi wetu wanatupenda, wanapotekeleza mambo tuwape muda tuone wanafanya nini.

Maendeleo hayawezi kuja kama hatutakuwa kutu kimoja, tunapaswa kuwa wamoja kuunga mkono jamba linalo anzishwa ili kulipa nguvu ya kukamilika kwake. Kuongoza nchi kubwa kama Tanzania sio kazi rahisi.
Lakini pia tunatakiwa kujua kuwa sisi ni binadamu na hakuna binadamu asiye kosea hivyo ndivyo tulivyo umbwa, wapo watu kwaajili ya kuongea na kurekebishana katika ngazi za juu za serikali hivyo tusiwe tunaongea mambo tusiokuwa na uelewa nayo.

Kusema hivyo haina maana kwamba tusihoji au tusiulize au tusilalamike nchi yetu ni ya kidemokrasia hivyo tufanye kama demokrasia inavyotaka ila tusitoe taarifa za uongo. Kutoka na taarifa hizi za uongo inapelekea wananchi kufanya mambo kwa mihemko kama vile kuchukia watu wa chama fulani, kutotoa ushirikiano katika maswala ya kimaendeleo kwasababu kiongozi ni wachama pinzani, kuchochea kukwamisha shughuli fulani.

Lakini pia watanzania tuache kulalamikia mambo madogo kwani kila kitu kina muda wake.

NINI TUNAPASWA KUFANYA WATANZANIA?

Tunapaswa kubadilika kwa kuleta mfumo mzuri wa kisiasa na kuupa jina la MABADILIKO YA KISIASA. Mfumo huu utalenga kuwaunganisha watanzania wa vyama vyote na kuwa kitu kimoja yaani mtu wa chama fulani kuweza kuungamkono jambo linalofanya na chama kingine, kutoingia kati migogoro ya kisiasa.

Mabadiliko haya ya kisiasa yatasaidia kuungana kwa wananchi kwa kuwa kitu kimoja bila kubaguana. Kama tulivyoweza kuondoa ukabila nchini kwetu ndio hivyo tunatakiwa kuondoa uchama, kila mtu awe na mwanachama wa chama fulani lakini tuwe tunapendana na kushirikiana ifika hatua mbaka kuombana ushauri juu ya maamuzi fulani ila kupiga hatua za kimaendeleo. Itapendeza sana kama nchi yetu tukiwa kama familia, shida ikiikumba chama fulani basi chama kingine kiguswe pia, kiweze kutoa msaada bila unafki.

Tukifanya hivyo naamini tutapiga hatua kubwa sana na hata kuwa mfano wa kuigwa na mataifa mengine duniani.

Tukipeana taarifa sahihi bila kupotoshana basi tutapendana kwani mapenzi hutoweka baada ya kuambiwa kuwa wanajenga miradi kwa manufaa yao binafsi hapo ndipo wananchi wanaingiwa na wasiwasi na kutoiunga mkono katika mambo hayo. Lakini pia kuna kundi la wasanii ambalo limebeba watu wengi sana na wasanii hao wanamashabiki wengi sana, wasanii wakiipotosha jamii basi ni rahisi sana watu kuwaamini.

Hivyo wasanii wanapaswa kutoa burudani na mafunzo kupitia nyimbo zao na sio kupotosha watu, wasiwe wanaimba nyimbo zao kwa kuzungumzia vibaya watu kwa nyuma yao kuna kundi kubwa ambalo linayumbishwa na wao. Tudumishe upendo na amani ili kuleta maendeleo.
 
Upvote 6

Nimeshindwa kusoma bandiko lako lkn nimedondosha kura yangu kwa sabab nimevutiwa mno na heading
 
Back
Top Bottom