Watanzania tuache sifa za kuomba upendeleo

Watanzania tuache sifa za kuomba upendeleo

Koryo2

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2016
Posts
2,056
Reaction score
2,519
Imekuwa kawaida kila Mhe. Waziri, Mhe. Mbunge, Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa wilaya na hata Mkurugugenzi na mtu wa kawaida kusifu hata asijue anasifia nini.

Kuna mapungufu sana katika sekta zinazohudumia watu lakini haya hayasemwi isipokuwa sifa.

Mfano hai ni sekta ya afya. Hakuna matibabu ya bure na kila ukifika kwenye zahanati, Kituo cha Afya kumuona daktari unalipia fedha baadaye unaambiwa ukanunue madawa kutoka maduka ya ya watu binafsi.

Haya mapungufu hayasemwi lakini kila kukicha na sifa. Sehemu nyingi nyingi hakuna maji, umeme unakatika kila kukicha lakini mwisho wa yote ni sifa.

Watanzania tujitambue acheni sifa za kuomba au kupata cheo, upendeleo n.k.
 
Hiki kizazi kishaharibika, labda tuanze upya na hawa watoto wanaozaliwa sasa hv, tuwajenge kuwa wazalendo na waipende nchi yao. Wasiwe na nidhamu za woga na waache kujipendekeza kwa wenye mamlaka, palipo na dosari waseme bila woga
 
Back
Top Bottom