Kumezuka tabia ya kuendekeza starehe na sherehe kubwa za harusi kwa kutegemea michango ya watu, tatizo linakuja unapotaka kila mtu akuchangie ilimradi unamfahamu au Mtumishi katika taasisi moja, inakera sana michango inakuwa nongwa, msg mara simu mara nini nini? Mara umeadiwa kwenye group bila ridhaa. Kiukweli binafsi sipendagi hii tabia.
Halafu usipochangia unakasirikiwa kabisa kana kwamba lazima. Hebu nipate experience wezangu wenye mtazamo kama wangu wakutopenda kuchangia na wala huwa hawaombi michango?
samahani kwa kuvamia uzi , maana 'mimi si mwenzako mwenye mtazamo wa kutopenda kuchangia, na huwa ninatoa michango.
Ila nimeguswa niseme kitu.
Tabia ya kuchangishana haijazuka kama wewe usemavyo, imekuwapo toka enzi kabla wewe hujazaliwa. Toka enzi za ujima watu walikuwa wakichangishana hata mazao, mafano mchele, maharage, mahindi nk. kwa kwa ajili ya kufanikisha sherehe. Ikafika mahali mazao au vitu vikawa adimu kuliko pesa, hapo watu wakaanza kuchangishana pesa.
Wote waliochangia walifanya kwa furaha na kwa moyo wa kupenda. Hata ikitokea mtu hajaombwa mchango na ndugu, jamaa au rafiki alijisikia vibaya kwa kujihisi kwamba ameonwa vipi, wakati mwingine hata kukasirika kwamba amedharauliwa. Kutokana na hili , mleta mada usifikiri kwamba kila akuombaye mchango ana shida na pesa yako, wengine wanatimiza wajibu tu ili usije ukalaumu.
Imefika mahali pesa nayo imekuwa adimu. Sasa kumezuka SASA kumezuka tabia ya watu kutopenda kuchangia sherehe za wenzao hata kuwashushia heshima hao wanaamba michango.
Napenda kuwaambia mleta mada na washiriksa wake kwamba tatizo walionalo si la hao wawaombao michango, bali ni la jamii, maana jamii imejengeka hivo. Inahitaji ujasiri wa aina yake kuipinga jamii inapotaka uombe michango kwa watu, ushawishi huwa ni mkubwa sana kwamba sherehe ni yako lakini haujifanyii mwenyewe, wafanyiwa na wanajamii, ingawa mwisho wa siku unatwikwa zigo la kuomba michango huku ukisaidiwa kwa mbaaali, ili kina bitcoinbase wakuone kimeo.
Mawazo ya mleta mada ni mazuri nayeye pamoja wachangiaji wanaomsapoti wanaonesha kuwa jamii imeanza kubadilika taratibu, angalau sasa kuna watu wenye ujasiri wa kuiambia jamii kwamba ndoa na maisha ya ndoa ni bora kuliko sherehe ya ndoa .
Nakushukuru mleta mada, natamani jamii ibadilike, wasitarajie sana sherehe toka kwa vijana wanaooa maana wakati mwingine hata wamewakwamisha vijana kufanya maamuzi hayo kwa kufikiria gharama za sherehe za harusi. Bali wawe radhi kulingana na uwezo wa kijana ama familia yake, kuamua kwamba kutakuwa na sherehe au la , au sherehe kubwa au ndogo.