Sinkala
JF-Expert Member
- Dec 22, 2008
- 1,773
- 688
Kuna kozi zinaendelea kutolewa kupitia LIVE VIDEOCONFERENCE katika centre ya Tanzania iliyopo UDSM. Project hii ipo katika nchi 53 za Africa na watu wanasoma huku wakimuona mwalimu LIVE katika big plasma screen + projector screen. Unaweza kuuliza swali kwa kunyoosha kidole na mwalimu anaweza kuuliza swali direct kwa kumchagua mwanafunzi anayemtaka. Hii ni tofauti na online learning, hii ni Tele-Education system ambapo wote (mwalimu na mwanafunzi) lazima muwepo darasani muda wa lecture. Kuna posibility pia ya kudownload video ya lecture iliyopita for your revision. Wanafunzi wa centre ya Tanzania wana uwezo pia wa kuwaona wenzao wa centre nyingine. Kuna centre zina wanafunzi hadi 200 (km Uganda) lakini watanzania tunachechemea. Project hii inatambuliwa na Serikali ya JMT kwani ni mkataba btn countries na sio Universities, na UDSM is just a centre, lakini Wizara ya Sayansi na Teknolojia ingeweza kuweka centre popote pale nchini kama ingetaka. Kwa maelezo zaidi soma hapo chini na ukimbie kuapply kabla pazia halijafungwa: