Watanzania tuchangie kuboresha katiba yetu

Watanzania tuchangie kuboresha katiba yetu

John Mtui

Member
Joined
Nov 29, 2012
Posts
5
Reaction score
2
Ndugu zangu Watanzania Tunajua kabisa kuwa hii ni nchi yetu na ni vizuri tukasema tunavyotaka iwe vinginevyo watu wachache watatusemea wanavyotaka iwe, mwisho wa siku tutakuwa tunalamika tu kuwa hatukutaka iwe hivi. Tunamshukuru Rais wetu Mh Dr Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutupa nafasi hii ya kuamua mustakabali wan chi yetu kwa kutunga katiba mpya; nafasi ambayo ni adimu sana kwa nchi nyingi duniani. Ahsante sana Mheshimiwa Rais Tunajua kuwa wenzetu wa visiwani wanaichangamkia nafasi hii kwa nguvu zao zote ili kuboresha maslahi yao katika muungano. Wamehamasishana na wamejitokeza kwa wingi sana kuhakikisha wanapata the best steak katika muungano huu mwema. Ukaaji wetu kimya utatufanya tuishie kuachiwa mifupa mwisho tulalamike. Nawaomba Watanzania tuchangie uaandaaji wa katiba mpya, hasa kwenye eneo la Muungano; Yaliyo hapa chini ni mawazo yangu mimi mwenyewe, simshawishi mtu kuyaafiki, ila kama unaona na wewe una mawazo kama ya kwangu, just copy and paste it on this links wanaoishi Ndani ya nchi Muundo wa Muungano 1 Pendekezo langu la kwanza (Serikali moja tu) Nashauri kuwa na seikali moja tu – Serikali ya Jamhuri ya Muungano ambapo Zanzibar ni Mkoa na Pemba ni mkoa katika serikali hiyo. Hii inatokana na ukweli kwamba kama kweli tumeungana kama nchi moja, hakuna haja ya kuwa na nchi ndani ya nchi nyingine. Zanzibar imekuwa kama nchi kamili ndani ya Tanzania kitu ambacho si sahihi. Wana Rais wao, Makamu wawili wa Rais, baraza la mawaziri na bunge (baraza tukufu la wawakilishi). Wana bendera yao, wana katiba yao, wana tassisi zao na kila kitu kinachoifanya iwe serikali kamili isipokuwa tu vyombo vya dola. Na bado wanataka mengine ikiwemo kutaka kuwa part ya taasisi za Muungano huku wao wakiwa na taasisi zao wenyewe mfano ZACP agaist NACP, ZFA against TFF, ZMCP against NMCP na mengineyo mengi. Hii ni unfair kwa sababu zifuatazo - Wao wana serikali yao ambayo sisi hatushiriki hata kidogo na hatuna uwezo wa kuinfluence kitu chochote huko lakini sisi hatuna serikali yetu ambayo wao hawana influence. Wao wanatuamulia (kupitia uwakilishi wao kwenye bunge la Jamhuri na Baraza la Mwaziri) lakini sisi hatuna uwakilishi kwenye serikali yao ili kujitetea wanapofanya maamuzi kandamizi. Hii ni uoneveu kwa wa Watanzania bara. Kumbukeni siku baraza la wawakilishi walipokuwa wanajadili suala la mafuta. Hakukuwa na mtu wa kuitetea Tanzania bara. - Wao wanakuwa treated kama serikali kamili na tassisi kamili, na mapato yanayoingia kwenye maeneo hayo hayawanufainishi Watanzania wote, yanawanufaisha wao tu. Lakini mapato yanayokuja kwa jina la Muungano, wao wana sehemu yao. This is double allocation and unfair - Sheria zote za Tanzania zinawatambua watu wote wanaoishi Tanzania (bara na visiwani) kama Watanzania, ila Zanzibar kuna sheria ambazo zinamtreat Mtanzania bara kama foreigner (Mfano sheria ya Ardhi). Ndio maana Wazanzibari wengi sana wana Ardhi huku bara ukilinganisha na walio na ardhi huko Zanzibar. Tukiwa nchi moja, mambo haya yatafutika - Kwa mtizamo wangu, kwa nchi maskini kama Tanzania kuwa na serikali mbili ni kuwaongezea walipa kodi gharama za uendeshaji. Naamini kabisa gharama zinazotumika kuhudumia uongozi wa serikali ya Zanzibar (Mheshimiwa Raisi, Watendaji wake na Baraza la Wawakilishi) ni kubwa sana ukilinganisha na ambavyo tungehudumia Mkuu wa Mkoa wa Unguja na Mkuu wa Mkoa wa Pemba) Na kwa vile Mapato ya Zanzibar sio makubwa sana, mzigo huu unawaegemea hata watu wa Bara. Naomba tujiulize, watu milioni moja wana mapato gani ya kuwekeza kuendesha serikali ile, ukichukulia kuwa hata kodi wanayotozwa ni ndogo kuliko bara. Hii inaonyesha kuwa sehemu kubwa ya gharama ya kuiendedsha serikali ya Zanzibar inatokwa kwa walipa kodi wa Tanzania bara.
- Wazanzibar wamekuwa wanadai kuwa treated as special part of the population na wamekuwa treated hivyo. Ile ni sehemu wanakoishi 0.03% ya Watanzania (1,070,000/40,000,000) lakini wamekuwa wakidai uwakilishi wa mkubwa sana mara nyingine 50/50 kwenye mambo ya Muungano mfano
o Tume ya Marekebisho ya Katiba ina wajumbe nusu kwa nusu kati ya Wazanzibari na Wabara. o Uwakilishi wa wananchi bungeni umekuwa si usawa. Sababu ni kwamba kuna majimbo ya Zanzibar yenye wapiga kura 3000 na wakati bara kuna majimbo yenye wapiga kura 300,000. Hii ni sawa na kusema kuwa wakati Watagnyika 300,000 wana kura moja bungeni, Wazanzibar 300,000 wana kura 100 bungeni. Hii sio sawa kwa sababu watu 3000 hawawezi kumhudumia wabunge kutokana na kodi wanazolipa kwa serikali. Kwa hiyo utaona watu laki tatu ndio wanaowalipa mishahara, posho na stahili nyingine hawa wabunge wa Zanzibar lakini linapokuja suala la kupiga kura, wanaofaidika ni Wazanzibar. Ndio wanaowaamulia Watanganyika. Hii si sawa o Tofauti ya kodi. Wenzetu wa Zanzibar kodi wanazotozwa ziko chini zaidi ya zinazotozwa bara. Sasa wanatumia kigezo hicho kuishi maisha yenye nafuu kuliko Wanzania wa bara huku bara tukilipa kodi kubwa kuwahudumia wao. Mifano michache ya matumizi mabaya ya tofauti hii ya kodi. - Wazanzibar wanaagiza mali nyingi kupitia Zanzibar zikiwemo bidhaa za kwenye super market. Baadae wanzipakia kwenye majahazi kuziingiza bara na kuzishusha kweny bandari bubu (Tanga, Bagamoyo, Rufiji, Kilwa etc) na baadae kuzileta Dar es Salaam. Hapa wanakuwa wamekwepa ushuru. Wakifika huku wanziweka kwenye super market zao na kuanza kuziuza. Kwa vile wanakuwa wamekwepa kodi, hata bei ya bidhaa inakuwa chini, kwa hiyo mtu wa bara huwezi kushindana nao kibiashara kwani wakati sisi tunafanya biashara halali na kulipa kodi kwa kiwango cha bara, wao wana ahueni ya kodi. Ndio maana biashara ya supermarket kwa kiwango kikubwa imetekwa na Wazanzibar kutoka Pemba. Hii ni kuwaumiza wabara kibiashara na mwisho waje kuwa omba omba kwenye nchi yao wenyewe. - Tulipobadili mfumo wa namba za magari kutoka TZ kwenda T…. XXX, wazanzibar waliokuwa wanaleta magari huku ilibidi walipe difference ya kodi ili kusajili gari lake. Katika kukwepa hilo, ilibidi nao kuanzisha mfumo wao wa namba ambao unatumika kote kitu ambacho kinawasaidia kutolipa kodi ya magari yanayoletwa bara o mmm - Na mambo mengine mengi yasiyo ya haki. Kibaya zaidi ni kuwa Wenzetu wanaendelea kutaka zaidi na kinapotokea kitu kizuri upande wa Zanzibar wanakitungia sheria ya kuwatenga Watanganyika. Mfano mzuri ni pale walipohisi kuwa mafuta yamegunduliwa wakaanza kutunga sheria ya kuwatenga Watu wa bara kwa kuyaondoa mafuta kwenye mambo ya Muungano Haya ni baadhi tu ya mambo yaniyofanya nione huu Muungano kama vile ushirkianao ambao terms zake ni kama ‘Zanzibar ni kwa ajili ya Wazanzibari tu, lakini Tanganyika ni kwa ajili ya wote (bara na visiwani. Hii sio fair. Kwa vile si vizuri kutengana, nashauri tuungane katika terms ambazo ni fair kwa kila mtu. 2 Pendekezo la pili – Kutengana kabisa Kama itashindikana kuwa na nchi moja kama nilivyotaja hapo juu, ni afadhali tutengane kabisa. Zanzibar iwe nchi kamili isiyo ndani ya nchi nyingine, na Tanganyika iwe nchi kamili. Yaani Tanganyika na Zanzibar ziwe kama ilivyo Kenya na Uganda au Tanzania na Kenya. Tutabakia kuwa ndugu kial mtu akiwa kwake na kuondoa manunguniko ya Muungano yaliyopo. Nasema hivi kwa sababu; - Sababu za kiusalama zilizoifanya Tanganyika na Zanzibar kuungana hazipo tena. Sultani hawezi kurudi tena na sioni Zanzibar kama nchi kuwa na any added security concern kwa sasa. Wazanzibar wamekuwa wanalalmika wazi kuhusu Muungano. Hii inatokana na Uhuru walionao katika kujadili Muungano tofauti na Bara ambako kujadili Muungano inaonekana kama kosa. Mimi siajwahi kukuatana na Mtanganyiak yoyote ambae sio kiongozi anayeutaka Muungano. Hata viongozi niliowahi wakiwa kwenye mazingira yasiyo ya kikazi huwa wanasema huu Muungano haufai. Naamini kabisa ni Muungano ni miongoni mwa mambo yanayowasononesha 99% ya Watanganyika. Ni muda muafaka sasa kuwaondolea Watanganyika sononeko hili. Nashauri serikali iitishe kura ya Maoni pande zote mbili za Muungano, ili kila Mtanzania apige kura kuhusu Muungano (Serikali moja, serikali mbili au kutenagana kabisa) Naamini Watanganyika walio wengi wanataka kutengana ila Wazanzibar watataka hizi hizi serikali mbili ambazo kwao ni faida zaidi - Kitendo cha Wazanzibar kunzisha kuboresha (kuboldi) mstari uliopo kati ya serikali ya Tanganyika na Zanzibar (bendera yao, katiba yao, taasisi zao etc) wakati huo huo wakiongeza ukubwa wa tobo la njia moja la kuitumia bara (kuendelea kudai mafao zaidi kwenye Muungano) ni dalili tosha kabisa kuwa wanahitaji kukaa kwao. Kwa muono wangu, Mh Raisi akitoka bara, automatically, Mh Rais wa Zanzibar angekuwa makamu wa Raisi. Hali ilivyo sasa inawapa Wazazibar nguvu kubwa sana katika ngazi za juu za maamuzi. Wakati uongozi wa juu wa serikali yao ikiwa inaongozwa na Wazanzibar wazalendo, (Rais na Makamu wawili wa raisi), Uongozi wa juu wa Muungano una Mzabari. Kwa hiyo katika viongozi wakuu watano wan chi (Wah. Marais wawili na makamu watatu wa Mhe Rais,) Wanne wanatoka Visiwani, jambo ambalo linaipa nguve sana Zanzibar kuhusu bara. Ni jambo la kawaida sana kumuona Makamu wa Rais wa Zanzibar akija kufanya ziara za kikazi huku bara. Mimi sijui zaidi ya Mh Rais, ni nani anaenda kuangalia wanachofanya wenzetu. Ni mgawanyo usio walazima wa madaraka, aambao hauko fair na ambao unaongeza matumizi ya serikali ambayo kwa kiwango kikubwa yanatoka bara na anayefaidika ni Zanzibar. Hii si sawa. 3 Pendekezo la tatu – Serikali tatu Kama hayo mawili hapo juu hayawezekani, basi kuwa na serikali tatu, yaani - Serikali ya Muungano yenye Rais wake, baraza la mawaziri na bunge - Serikali ya Mapinduzi Zanzibar - Serikali ya Tanganyika yenye Rais wake, baraza la mawaziri na bunge

Ikumbukwe kuwa hata Wazanzibari wenyewe hawataki Muungano. Angalia picha za mabango yaliyoko kwenye baadhi ya miji ya Zanzibar

IMG-20121212-00238.jpg

IMG-20121212-00239.jpg
Mungu ibariki Tanzania, Mungu mmbariki Mh Dr. Jakaya Mrisho Kikwete
 
Back
Top Bottom