Mbunge Wakimataifa
Member
- Jan 3, 2024
- 26
- 25
Ili Tanzania ya sasa na ijayo iweze kukabiliana na kuondoa tatizo la kuporomoka kwa thamani ya shilingi na uchumi kwa ujumla pamoja uhaba wa fedha za kigeni, ni vema sisi kama Tanzania tuchague sekta ambazo sisi kama watanzania tunazimudu katika kuzianzisha na kuziendeleza kulingana na uwezo wetu kiuchumi na kiteknolojia. Ili kupitia sekta hizo tanzania ijulikane kama ndiye kinara au miongoni mwa wazalishaji wa aina fulani ya bidhaa ulimwenguni.
Kupitia hilo tutakuwa tumelifanya jicho la ulimwengu liitazame Tanzania kama sehemu muhimu ya upatikanaji wa bidhaa fulani ili kupitia bidhaa hiyo/hizo Tanzania iweze kujipatia fedha za kigeni kiurahisi kuliko ilivyo sasa hivi ambapo tunategemea zaidi madini na mazao kwa kiwango kidogo.
Ili uchumi uweze kutengamaa ni lazima kuwe na mzani sawa kati ya tunachokitoa na tunachokiingiza. Kwa hali ilivyo sasa Tanzania tuna maeneo mengi ya kutoa pesa zetu nje kuliko maeneo yanayotuingizia pesa kutoka nje. Katika kutekeleza hilo naishauri serikali iweke mkazo mkubwa katika sekta zifuatazo ambazo hizi sisi watanzania tunazimudu;
1. KILIMO; tuweke mkazo mkubwa katika kilimo cha mazao ya aina zote yaani chakula na biashara. Naamini katika kilimo tunaweza kufanikiwa kwasababu tuna ardhi ya kutosha. Nchi nyingi za africa hukumbwa na majanga ya njaa mara kwa mara hivyo basi sisi kama Tanzania tunaweza kuwa sehemu ya utatuzi wa matatizo kama hayo kwa kuwa mzalishaji na msambazaji mkubwa wa chakula barani afrika kisha kujipatia pesa za kigeni. Tuna korosho,chai,kahawa na tumbaku ni mazao tunayoweza kuuza kokote duniani. Mfano mzuri nchi ya Ukrane yenyewe imejidhatiti katika uzalishaji wa ngano, anakula hela ya mtu yeyote ulimwenguni kupitia ngano.
2. MADINI; Tanzania imebahatika kuwa na madini mengi sana, tujikite katika utafiti ili tuweze kugundua vyanzo vingine vingi vya madini, tuyatengenezee mfumo mzuri wa kuyavuna bila kuruhusu uuzaji holela na kwa vile madini ni bidhaa inayohitajika sana ulimwenguni hii itaifanya Tanzania iweze kujiongezea idadi kubwa ya pesa za kigeni kuliko ilivyo hivi sasa ambapo dola huadimika mara kwa mara lakini pia tumekuwa tukitoa zaidi pesa zetu nje bila kuwa na njia mbadala ya kuzirudisha.
3. BANDARI; Kuna nchi nyingi zinategemea tanzania kama mlango wa kuingizia bidhaa nchini kwao. Tuboreshe bandari zetu ili ziweze kufanya vizuri zaidi na ikibidi hata kujenga bandari zingine mpya tuzijenge ili tupate watumiaji wengi wa bandari zetu kutoka nchi tofautitofauti ili tupate pesa zao kupitia bandari.
4. UJENZI; kwenye sekta ya ujenzi tupunguze idadi ya wakandarasi kutoka nje ya nchi, hawa nao ni kikwazo kwa uchumi wetu kwasababu wanalipwa pesa nyingi hivyo wamekuwa miongoni mwa sababu za kupungua kwa idadi ya fedha za kigeni nchini na kuyumba kwa uchumi wa nchi. Ni bora tutumie wakandarasi wa ndani ili pesa ibaki nchini kwetu. Tunakopa pesa nyingi kwa ajili ya miradi mbalimbli lakini pesa hizo zinaingia na kutoka, tunashindwa kuzibakisha kwasababu wanaokuja kuitekeleza miradi hiyo wengi woa ni wageni.
5. UTALII; tuna vivutio vingi nchini ambavyo vinatuingizia pesa za kigeni lakini tusiridhike na mazingira yaliyopo hivi sasa, tuendelee kuwa wabunifu kwenye sekta ya utalii. Tuboreshe sekta ya utalii kulingana na mazingira na wakati. Tutangaze vivutio vipya na vile vilivyopo tuviboreshe ili kuvutia watalii wengi zaidi nchini. Pesa za utalii ni pato la moja kwa moja halihitaji uwekezaji mkubwa sana kama ilivyo kwenye viwanda lakini ukiweka mazingira vizuri na usimamizi bora pato lake ni uhakika.
Kuna mambo mengi tunaweza kuyafanya na yakaleta tija kwenye uchumi wetu lakini haya niliyoyaelezea ni mambo ambayo nina uhakika sisi kama watanzania yamo ndani ya uwezo wetu tuyashupalie haya tunayoyaweza kwa asilimia kubwa kuliko kuhangaika na mambo mengi ambayo uwezo wetu haufiki hata nusu. Mfano kwenye suala la viwanda, ni kweli viwanda ndiyo nguzo kubwa ya uchumi wa nchi zilizoendelea lakini ni suala linaloenda pamoja na teknolojia.
Sisi kama watanzania lazima tukubali teknolojia yetu kwa sas bado iko chini haifikii kiwango halisi kinachoendana na teknolojia ya viwandani. Hatuwezi kuipata hela ya watu wenye uchumi wa viwanda kirahisi kwasababu kiteknolojia wako mbele zaidi yetu.
Sisi tuwatafutie na kuwauzia vitu ambavyo wao hawana na havipatikani kwa kutengenezwa viwandani kama vile madini na mazao ambayo ni mali ghafi ya viwanda vyao.
Ili tunapoenda kuchukua bidhaa zao za viwandani na wao waje wachukue kwetu mali ghafi za viwanda vyao ili kila mmoja atoe na kupokea.
Huko kwenye viwanda twende taratibu kwa kadili tunavyoweza lakini yale yaliyo ndani ya uwezo wetu tuyazingatie na kuyatekeleza kwa asilimia 100 au hata 95.
Maendeleo ni hatua kwa hatua, hata mapinduzi ya viwanda ulaya yalianza na kilimo.

Upvote
5