Godfrey Protas
New Member
- Jan 17, 2017
- 1
- 2
Kabla ya kuendelea na mada husika ningependa kwanza tuelewe maana ya ujuzi. UJUZI ni maarifa aliyonayo mtu katika kubuni, kufikiri, kuunda na kutenda jambo au kitu kitakachomsaidia yeye mwenyewe au jamii yake inayomzunguka katika maisha yake ya kila siku. UJUZI WA KUTENDA ni ujuzi ambao humwezesha mtu kuwa na uwezo wa kutenda kazi itakayomwezesha kujipatia kipato chake na kujiajiri pasi na kusubiri kuajiriwa na mtu mwingine au taasisi fulani. mtutu mwenye ujuzi wa kutenda huwa na uwezo wa kufanya kazi kubwa ya kubadilisha hali ya uchumi wake binafsi na uchumi wa nchi kwa ujumla.
Katika kujenga ile tanzania tunayoitaka au tuipendayo ni vizuri watu wotw na mamlaka zote nchini zikachkua jukumu la kuwekeza katika elimu ya kazi na maarifa ya kazi itakayopelekea kuzalisha watendaji wengi watakaoweza kuchukua hatua madhubuti katika kuijenga tanzania mpya ambayo ina watu wenya maarifa na ujuzi wa kutosha wa kazi katika fani mbalimbali. kwa kusema hii haimaanishi kwamba nakosoa mfumo wetu wa maarifa yanayotolewa kwa sasa na taasisi na mamlaka zetu za kielimu, ila najaribu kutoa rai na kuona jinsi ya kuweza kuleta mfumo wa elimu ambao utazalisha watendaji zaidi wa kazi kuliko kuzalishwa wasimamizi tu peke, ambao hawana uthubutu wa kujiajiri na kutengeneza taasisi zao za fani zao.
hii itasaidia kuponguza wimbi kubwa la vijana ambao tumehitimu vyuo mbalimbali na tumerudi kwa wazazi kuendelea kusubiri ajira badala ya kutengeneza ajira. hapa tunahitaji kuimarisha vyuo vya VETA na Kujenga shule nyingi za UFUNDI ili kufikia tanzania ya viwanda kwa maendeleo stahimilivu

Upvote
2