Heshima mbele mkulu,kwa vile uchaguzi mkuu ndo huooo unakaribia mi nadhani ni vema vyama(hasa vyama vya upinzani) vikatumia muda uliobaki kwa ajili ya kufanya maandalizi ya uchaguzi wa mwakani(mikakati ya ushindi) badala ya kusubiri mwaka 2010 ufike na kufanya maandalizi ya zimamoto...Huu ni wakati wa kuanza kuangalia ni nani atagombea na kushinda kihalali(kukubalika kwa wananchi) na si wakati wa kuanza kukusanya hela za kutoa rushwa ili ushinde katika uchaguzi huo mkuu...Huu ni wakati wa vyama vyote vyenye nia ya kushiriki katika uchaguzi huo mkuu kufanyia kazi/kusahihisha makosa yote yaliyopelekea vishindwe katika chaguzi zilizopita...Vilevile huu ni wakati kwa CHADEMA kujiimarisha katika ngazi za mikoa,wilaya,tarafa,kata,vijiji na shina(kama ilivyo katika chama tawala CCM) ili kuleta upinzani na ushindani wenye uwiano tofauti na ilivyo sasa(Hii ni pamoja na kuandaa bajeti ambayo kipaumbele chake kitakuwa ni kuimarisha kama sio kuanzisha matawi ya wilayani na vijijini ambako ndiko wapiga kura wengi wapo) ,Pia ni wakati wa CUF kujiimarisha zaidi Tanzania bara kama ilivyojiimarsha PEMBA,lengo kama nilivyosema hapo awali ni kuwa na upinzani wa kisiasa wenye uwiano hasa bungeni na katika halmashauri za wilaya,miji,manispaa na majiji(maendeleo yatakuja kwa kasi ya ajabu mno)...Aidha ni wakati wa chama tawala CCM kukaa na kujisafisha ili kiwe safi(japo kiasi) kinapoingia katika uchaguzi mkuu wa mwakani,hapa nina maana kwamba CCM kiandae wagombea walio wasafi,wanaokubalika kwa wananchi na si wanaoingia madarakani kwa kutoa rushwa ama wale ambao wanasifika kwa kuwa na sifa maarufu ya UFISADI...Mwisho ni wakati kwa Tume ya Taifa ya uchaguzi(NEC) na pia Bunge kukaa chini na kuifanyia marekebisho sheria ya uchaguzi ili kuepukana na malalamiko ya mara kwa mara ambayo ni matokeo ya mapungufu ya sheria hiyo(kama ilivyotokea katika uchaguzi mdogo wa Mbeya vijijini).Ni ushauri tu....Naomba kuwasilisha wakulu..Mbarikiwe sana