BilioneaPATIGOO
JF-Expert Member
- Jun 23, 2012
- 12,320
- 11,327
Ni kilio kilio cha tozo, makato, kila mahali.
Ila watanzania wenzangu tukiendelea kusikilizia maumivu haya makali kabisa, embu kwa pamoja tujiulize maswali tafakuri yafuatayo
Je, makato na tozi za zamani katika miamala ya simu, vilienda wapi? Je, tulishawahi kufanyiwa press conference ya kuambiwa makusanyo yote ya tozo hizo katika miamala ya simu vilienda wapi au vilitumikaje?
Na je, makato na tozo hizo, zilikua hazitoshi katika kufanya miradi ya maendeleo nchini? Ni kweli kabisa kwamba zilikua hazitoshi kiasi kwamba wakati huu wame double kama sio ku triple tozo na makato haya ya sasa?
Tunakumbuka ripoti ya CAG iliyopita madudu yaliyofanyika na ufisadi wa kutisha, mwendo wa bilioni tu, naomba tukumbushane haswa idara labda ya TRA, mawsiliano, Tanesco, na idara zote zinazohusika katika hili la miamala+tozo, je ripoti ya CAG ilikua inasemaje, naomba ambaye atapata upande huo atuwekee tuone na tusome.
Tutakiane heri katika uvumilivu huu wa mateso makali ya tozo na makato.
Asanteni na tupeane pole sote tunaokumbwa na mateso haya.