SoC01 Watanzania tunaweza kuyashinda Maradhi ya Kisukari

SoC01 Watanzania tunaweza kuyashinda Maradhi ya Kisukari

Stories of Change - 2021 Competition

ALI MOHAMMED

Member
Joined
Jul 16, 2021
Posts
32
Reaction score
61
Nikiwa muathirika wa ugonjwa huu tangu mwaka 2016, licha ya kuwa na ugonjwa wa kisukari kwa kuwa nafuata maelekezo na masharti yote ya kiafya kutoka kwa wataalamu, basi waweza usiamini Kamba mimi ni muhanga wa gonjwa hilo, lakini vyoyote itakavyokuwa mimi siwezi epuka kusema eti sina ugonjwa huo, kinyume chake ugonjwa huo ninao lakini naishi nao kwa amani kabisa, ndipo nikaona niwape Watanzania wenzangu dondoo mbili tatu ili kuwapa tahadhari ya ugonjwa huu wale ambao hawajapata na kwa wale waliopata basi angalau wapate moyo na nasaha za ugonjwa huu.

Tanzani ni miongoni mwa nchi za Afrika silizokugubikwa na maradhi sugu ambayo huchangia kupoteza nguvu kazi ya taifa kwa kiwango kikubwa sana, watu wengi hawana mazingatio ya kutosha juu ya magonjwa haya sambamba na kukosekana kwa kampeni endelevu juu ya magonjwa haya, mfano wa magonjwa haya ni Presha na Kisukari, ambapo magonjwa haya kikawaida huwa hayakai mbali mbali bali mara nyingi hufuatana, muda mwengine mtu anaweza kuanza kuuguwa Presha na Baadae Kisukari kikafuatia, au kinyume chake pia yawezekana.

Leo ningependa kuzungumzia zaidi namna gani Watanzania kama taifa tunaweza kulidhibiti taifa letu ili lisidhurike na ugonjwa huu wa kisukari ambapo kitaalamu wanaita “Diabetic”. Maradhi haya ya Kisukari ni khatari mno, ingawa hakuna maradhi yalio salama, lakini naweza sema kama utafiti utafanywa wa kuyajua magonjwa yanayoongoza kwa uharati nchini Tanzania, basi Kisukari hautakuwa wa mwisho, bali utakuwa miongoni mwa magonjwa ya mwanzo yalio hatari.

NINI UGONJWA WA KISUKARI?

Ugonjwa wa kisukari (Diabetic) ni ugonjwa ambao husababishwa na ufanyaji kazi wa mwili ambapo mtu anakuwa na kiwango kikubwa cha sukari aina ya glucose katika mwili ambapo mwili wake hukosa uwezo wa kutengeneza insulin ya kutosha au seli za mwili wake haziwezi kutumia insulin iliyopo au pia mwili kuwa na matatizo yote mawili kwa pamoja, yaani kiwango kingi cha sukari na insulin dhaifu.

NINI HASA SABABU YA UGONJWA WA KISUKARI?

Kisukari (diabetes) ni ugonjwa unaotokana na tatizo la matumizi ya chakula katika mwili. Mwili wa binadamu hutumia chakula kilichoyeyushwa ili kuuwezesha kuwa na nguvu na kukua. Chakula cha aina nyingi tukilacho huvunjwavunjwa na kupata glucose, aina ya sukari katika damu ambayo ndiyo chanzo kikuu cha nguvu katika mwili wa binadamu.

Chakula baada ya kuyeyushwa, glucose huingia katika mfumo wa damu. Seli za mwili hutumia glucose hiyo ili kupata nguvu na kukua. Lakini seli haziwezi kuchukua glucose hiyo bila uwepo wa insulini (Insulin), insulini ndiyo inayoziwezesha seli hizo kuchukua glucose.

Insulin ni homoni inayotengenezwa na kongosho. Baada ya kula, kongosho hutoa insulin ya kutosha kuwezesha seli kuchukua glucose iliyopo katika damu, na mara baada ya glucose hiyo kuchukuliwa na seli, kiwango cha sukari katika damu hushuka.

Mtu mwenye kisukari ni yule ambaye kiwango chake cha glucose katika damu ni kikubwa mno (hyperglycemia) kutokana na kwamba mwili wake hautengenezi insulini ya kutosha, hautengenezi insulin ya kutosha au seli kushindwa kuitumia insulin inayotengenezwa na kongosho. Matokeo yake yake ni kuongezeka kwa kiwango cha sukari katika damu ambayo baadaye hutolewa nje ya mwili kupitia mkojo. Mgonjwa wa kisukari huwa na glucose nying katika damu yake lakini mwili unashindwa kuitumia glucose hiyo kwa matumizi yake ili mwili upate nguvu na kukua.

ZIJUWE AINA ZA UGONJWA WA KISUKARI

Kama nilivyoeleza kwamba kisukari ni kundi la magonjwa yanayohusiana na ufanyaji kazi wa mwili ambapo mtu anakuwa na kiwango kikubwa cha sukari aina ya glucose katika mwili kutokana na huku mwili wake kukosa uwezo wa kutengeneza insulin ya kutosha au seli za mwili wake haziwezi kutumia insulin iliyopo au pengine mwili kuwa na matatizo yote mawili kwa pamoja. Mgonjwa wa kisukari hupata haja ndogo mara kwa mara (polyuria), kusikia kiu kila wakati (polydipsia) na njaa (polyphagia).

Kuna aina tatu za kisukari; Type 1 Diabetes, Type 2 Diabetes na Gestational Diabetes.

TYPE ONE DIABETES
Aina hii ya kisukari mwili wa mgonjwa wa aina hii ya kisukari huwa hautengenezi insulin kabisa. Kisukari cha aina hii mara nyingine huitwa insulin-dependent diabetes, juvenile diabetes, au early-onset diabetes. Watu huwa na kisukari aina hii wanapokuwa na umri wa chini ya miaka 40 na hasa katika miaka ya mwanzo kabisa ya ujana wao. Kisukari cha aina hii huwapata watu wachache ukilinganisha na aina nyingine za kisukari, karibu asilimia 10 tu ya wagonjwa wote wa kisukari huwa na aina hii ya kisukari.

Mgonjwa mwenye kisukari cha aina hii atapaswa kutumia sindano ya Insulin katika maisha yake yote na lazima kila wakati ahakikishe kuwa kiwango chake cha sukari mwilini kinakuwa sawa kwa kuchukua vipimo na kufuata mpango wa chakula maalum.

TYPES TWO DIABETES
Mwili hautengenezi insulin kwa kiwango cha kutosha au seli za mwili zinashindwa kuitumia insulin iliyopo (insulin resistance). Karibu asilimia 90 ya wagonjwa wa kisukari katika ulimwengu husumbuliwa na aina hii ya kisukari.

Watu wenye unene usio wa kawaida na wenye uzito mkubwa wapo kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata kisukari cha aina hii ukilinganish na wale wenye miili ya kawaida.

Kuwa na uzito mkubwa au unene usio wa kwaida husababisha mwili kutoa kemikali zinazovuruga mfumo wa namna ya mwili unavyotumia chakula kilichoyeyushwa ili kuupa mwili nguvu na kuuwezesha kukua.

GESTATIONAL DIABETES
Aina hii ya kisukari ni kile kisukari wanachopata wanawake wakati wanapokuwa wajawazito. Baadhi ya wanawake wanakuwa na viwango vikubwa sana vya glucose katika damu zao na miili yao haina uwezo wa kutengeneza insulin ya kutosha kuweza kusafirisha glucose hiyo hadi kwenye seli za miili yao hivyo kusababisha kuongezeka kwa kiwango cha sukari katika miili yao.

Kisukari hiki huweza kudhibitiwa vizuri kwa kula chakula kinachofaa na kufanya mazoezi, Ni asilimia ndogo kati yao ambao huhitaji kupewa dawa. Gestational diabetes isipodhibitiwa huweza kusababisha matatizo wakati wa uzazi au kufanya mtoto anayezaliwa kuwa mkubwa kuliko alivyostahili.

MADHARA YA UGONJWA WA KISUKARI
Kwa kuwa ni ugonjwa, basi kisukari kama yalivyo magonjwa mengine basi nao una madhara yake, tena nadiriki kusema madhara ya ugonjwa wa kisukari ni makubwa na hatari zaidi ya madhara ya magonjwa mengine endapo ugonjwa wa kisukari hautadhibitiwa ipasavyo, madhara makubwa huweza kutokea. Baadhi ya madhara ambayo yamehusishwa na ugonjwa huu ni haya yafuatayo:
  1. Matatizo ya macho :- Mgonjwa wa kisukari yupo katika hatari kubwa ya kupata ugonjwa wa macho ambao kitaalamu unaitwa glaucoma, cataracts na mengineyo.
  2. Kupoteza Viungo:- Mgonjwa wa Kisukari ambaye hatadhibiti sukari yake ipaswavyo husababisha seli zake hai kukosa nguvu za kuponesha vidonda kwa haraka vidonda, hali hio ikidumu kwa muda mrefu husababisha mgonjwa kukatwa viungo vyake, vidole au miguu.
  3. Matatizo ya moyo:- Mgonjwa wa kisukari halikadhalika yupo katika hatari ya kupata ugonjwa wa moyo.
  4. Kupata Ugonjwa wa Kiharusi:- Kwa kuwa glucose huwa nyingi katika mwili wa mgonjwa wa kisukari hali ambayo huweza kusababisha figo kushindwa kufanya kazi vizuri, matatizo ya macho, magonjwa ya moyo na kiharusi nayo hujitokeza.
  5. Matatizo ya kusikia:- Kisukari husababisho tatizo la kushindwa kusikia vizuri.
  6. Ugumba:- Mgonjwa wa kisukari hushindwa kabisa kufanya tendo la ndoa, hali ambayo humfanya awe mgumba
KINGA YA UGONJWA WA KISUKARI
Hadi muda huu hakuna maabara yoyote duniani iliyothibitisha kutengeneza chanjo au kinga ya ugonjwa huu hatari wa kisukari, lakini Washahili husema “Mungu hakupi Kilema akakukosesha mwendo”. Kauli hii ya Waswahili ina sadifisha kwamba, licha ya kutokuepo kwa kinga wala chanjo za ugonjwa huu lakini ipo chanjo mbadala ya kujikinga na kujilinda kutokana na maradhi haya.

Kama tulikuwa pamoja tangu awali hadi hapa katika sehemu hii ya mwisho ya Makala hii, utagundua kwamba kumbe ugonjwa huu unatokana na sumu zilizomo ndani ya chakula, basi niseme chakula hicho hicho kinacho zalisha sumu iletayo kisukari nacho ndio hicho hicho kiletacho kinga halikadhalika tiba kutokana na mpangilio wa vyakula na miiko yake.

PUNGUZA/ ACHA KABISA KULA VYAKULA VA SUKARI
Endapo utapunguza kula vyakula ambavyo ndani yake kuna sukari ya moja kwa moja basi kumbuka umejipunguzia kitisho cha kuugua kisukari, vyakula hivyo ni:
  • Sukari yenyewe
  • Vyakula vyenye uwanga mwingi
  • Ugali (sembe)
  • Wali
  • Unga wa ngano mweupe
  • Na mfano wa hivyo
  • Vyakula vyenye Mafuta mengi
  • Mafuta yenyewe
  • Ngozi za kuku
  • Nyama nyekundu (Ng’ombe, mbuzi, Kondoo, nguruwe kwa wanaokula)
Tukiachana na njia hio ya kuacha kula vyakula nilivyo viorodhesha, pia inashauriwa ili ujiweke katika mazingira ya kuepuka kupata kisukari au hata kama tayari umeshapa ugonjwa kupunguza kiwango cha sukari , pia inashauriwa kufanya yafuatayo:
  • Mazowezi ni jambo la msingi, japo nusu saa kwa siku sababu mazowezi husaidia kuimarisha insulini yako sambamba na kuhuisha seli hai.
  • Kula vyakula vyenye vyuzi (Fibre) za kutosha mfano:
  1. Dona (sembe lililokobolewa)
  2. Ngano ya Kahawaia (Brown wheat flower)
  3. Kuku
  4. Samaki
  5. Ndizi
  • Vyakula vya Mizizi
  1. Viazi (Mbatata)
  2. Muhogo
  3. Na vyakula vyote vyenye asili ya kuvunwa aridhini.
  4. Mboga mboga
Katika milo yako yote hakikisha hukosi kula mboga mboga za aina zote ni suluhu tosha ya kushusha kiwango cha sukari/Glucose katika mwili, hasahasa bamia na mboga ya mchicha na nyenginezo.

HITIMISHO

Nadiriki kusema jamii ya Watanzania bado haijafahamu kwa kina juu ya athari za ugonjwa wa huu, hivyo Asasi za kiaraia ikiwemo Jamii Forums ina dhima ya kuelemisha Umma juu ya magonjwa mbali mbali, ili tupate Tanzania yenye afya endelevu kwa maendeleo endelevu, kinyume chake tukisema tuliache jukumu hili kwa serikali pekee, basi ule wimbo tunaoimba wa maendeleo tunayo yataka tutaendelea kuimba na hatimai vizazi vyetu vije virithi nchi iliyojaa maradhi
 
Upvote 44
Ni kweli inafaa kuogopa lakini inabidi tuogope kwa vitendo zaidi, nako ni kpunguza milo inayochangia maradhi hayo na kuzidisha milo inayopunguza kupata gonjwa hio, hapo utakuwa umeogopa kwa vitendo
Ugonjwa huu husababishwa na kula milo ya hovyo pekee au kuna sababu nyingine pia?
 
Ugonjwa huu husababishwa na kula milo ya hovyo pekee au kuna sababu nyingine pia?
Sababu nyengine ni kuwa na msongo wa mawazo isiyokwisha, msongo wa mawazo unauwa kongosho (pancreas), kongosho ikidhoofika inashindwa kumeng'enya chakula hivyo Glugose husafirishwa moja kwa moja kwenda katika damu, ndio maana mazowezi yanashauriwa mno ili kama njia ya kuondoa msongo wa mawazo (Stress)
 
Duh nimeishiwa nguvu zote na mimi nilikuwa naandika kuhusu gonjwa hilo hilo kama vile umechukua maneno mdomoni kwangu kazi kweli kweli halafu nishafika zaidi ya maneno 1000.

Ila type 2 diabetes hapo kwenye insulin resistance kinachotokea ni kwamba cells azihifadhi glucose but also fat acids; ambazo zote hizo (glucose na fatty acids) kazi yake ni kuupa nguvu mwili na kuzipunguza kwenye cells inabidi uwe active.

Usipofanya mazoezi au unapokula sana vitu vya mafuta cells zinakuwa na more reserve of glucose and fat kwa sababu uzitumii, kwa ivyo insulin inapobeba glucose tena kutoka kwenye chakula inakuta cells aziwezi pokea kwa sababu kuna enough reserve already; over time inaharibu cells receptors na insulin inakuwa aina uwezo wa kuipatia glucose.

Kwa kuanzia insulin resistance inapoanza excessive glucose inapelekwa kwenye ini (another natural storage area of glucose even without diabetes), ini ikizidiwa ndio glucose inatolewa na kupelekwa kwenye figo na kutoka kama mkojo to do that inatumia maji yaliyopo mwilini, leading to dehydration na kunywa sana maji and the cycle begins.

Ukishaona umefikia hapo hiyo ni pre diabetic na usipofanya mazoezi ndio mziki unaanza kunoga kwa sababu ini isipowenza tunza glucose za ziada baadhi zinaanza kubaki kwenye mishipa ya damu na ku affect flow rate ndio maana inakuja blood pressure, moyo inabidi ufanye kazi ya ziada kwa sababu damu aiji kwa wingi kwa ivyo nguvu nyingi inahitajika ku pump damu kwenye mwili matokeo yake na moyo wenyewe unakorongoka ndio maana magonjwa ya moyo na diabetes ni ndugu; story ni ndefu na madhara ni mengi.

Mweh ngoja nitafute topic nyingine japo article yangu ingekuwa somewhat different na hii yako maana kuna mambo ya Hb1ac risk za kupata DKA level za sukari zikizidi, four stages za type 2 diabetes, kwanini watu wengi wanayo ila awajui tu bado, kwanini inakuwa kwa watu over 40, figo linaharibika wakati gani, foot ulcers zinakujaje namna ya kujikinga etc.
 
Sababu nyengine ni kuwa na msongo wa mawazo isiyokwisha, msongo wa mawazo unauwa kongosho (pancreas), kongosho ikidhoofika inashindwa kumeng'enya chakula hivyo Glugose husafirishwa moja kwa moja kwenda katika damu, ndio maana mazowezi yanashauriwa mno ili kama njia ya kuondoa msongo wa mawazo (Stress)

Unapokuwa na stress au ata ukipata homa ya kawaida, mara zote in self defence kitu cha kwanza mwili unalazimisha ‘adrenal glands’ kutoa ‘cortisol hormones’ jukumu la hizo hormones ni kuuongezea mwili nguvu ya ziada na zinafanya ivyo kwa kubadili stored protein into glucose.

Kwa mgonjwa wa diabetes ukimuongezea glucose inamuongezea matatizo mengine, ndio maana stress sio kitu kizuri kwenye diabetes. Figo lina haribika kwa mtindo mwingine kwa kupoteza uwezo wa kuchuja uchafu kwenye damu ndio maana kuna wagonjwa wa diabetes wanahitaji dialysis.
 
Unapokuwa na stress au ata ukipata homa ya kawaida, mara zote in self defence kitu cha kwanza mwili unalazimisha ‘adrenal glands’ kutoa ‘cortisol hormones’ jukumu la hizo hormones ni kuuongezea mwili nguvu ya ziada na zinafanya ivyo kwa kubadili stored protein into glucose.

Kwa mgonjwa wa diabetes ukimuongezea glucose inamuongezea matatizo mengine, ndio maana stress sio kitu kizuri kwenye diabetes. Figo lina haribika kwa mtindo mwingine kwa kupoteza uwezo wa kuchuja uchafu kwenye damu ndio maana kuna wagonjwa wa diabetes wanahitaji dialysis.
Ahsante sana Mayor Quimby kwa nyongeza nzuri mno, tunahitaji watui zaidi wenye uelewa wa gonjwa hili kama wewe ili Tanzania iwe salama na Kisukari
 
Duh nimeishiwa nguvu zote na mimi nilikuwa naandika kuhusu gonjwa hilo hilo kama vile umechukua maneno mdomoni kwangu kazi kweli kweli halafu nishafika zaidi ya maneno 1000.

Ila type 2 diabetes hapo kwenye insulin resistance kinachotokea ni kwamba cells azihifadhi glucose but also fat acids; ambazo zote hizo (glucose na fatty acids) kazi yake ni kuupa nguvu mwili na kuzipunguza kwenye cells inabidi uwe active.

Usipofanya mazoezi au unapokula sana vitu vya mafuta cells zinakuwa na more reserve of glucose and fat kwa sababu uzitumii, kwa ivyo insulin inapobeba glucose tena kutoka kwenye chakula inakuta cells aziwezi pokea kwa sababu kuna enough reserve already; over time inaharibu cells receptors na insulin inakuwa aina uwezo wa kuipatia glucose.

Kwa kuanzia insulin resistance inapoanza excessive glucose inapelekwa kwenye figo (another natural storage area of glucose even without diabetes), figo ikizidiwa ndio glucose inatolewa kama mkojo to do that inatumia maji yaliyopo mwilini, leading to dehydration na kunywa sana maji and the cycle begins.

Ukishaona umefikia hapo hiyo ni pre diabetic na usipofanya mazoezi ndio mziki unaanza kunoga kwa sababu baadhi ya glucose zinaanza kubaki kwenye mishipa ya damu na ku affect flow rate ndio maana inakuja blood pressure, moyo inabidi ufanye kazi ya ziada kwa sababu damu aiji kwa wingi kwa ivyo nguvu inahitajika ku pump damu kwenye mwili matokeo yake na moyo wenyewe unakorongoka ndio maana magonjwa ya moyo na diabetes ni ndugu; story ni ndefu na madhara ni mengi.

Mweh ngoja nitafute topic nyingine japo article yangu ingekuwa somewhat different na hii yako maana kuna mambo ya Hb1c, risk za kupata DKA, four stages za type 2 diabetes, kwanini watu wengi wanayo ila awajui tu bado, kwanini inakuwa kwa watu over 40, figo linaharibika wakati gani, foot ulcers zinakujaje namna ya kujikinga etc.
Duh samahani sana, kwa uathirika wangu wa hili gonjwa ndio ulionisukuma kuandika hii topic, nisamehe bure, ila mchango wako katika haya maoni ni msaada mkubwa kwangu na kwa wengine pia
 
Nimeipenda sana mkuu,nimekupa vote. Tunakula vitu hatarishi sana,wali,ugali,makande vyote ukijumlisha na kiwango/quantity.. ni kama Tanzania mifumo yetu ya kula ni tunajichimbia kaburi wenyewe, ikiweza kupigwa kampeni kuhusu kisukari watu wakaacha eating habits zao life expectancy yetu itakua kubwa nina uhakika............ Asante mkuu kwa elimu,
 
kwanini watu ambao hawajawahi kuwa na kisukari lakini wakipata covid wakipima sukari inakuwa juu??!!
lakini baadae wakipona sukari inakuwa normal tuu km mwanzo??
 
Kwanza Ahsante kwa kunipa kura dada Rebbeca.

pili ni kweli possion zetu za chakula ni kubwa kupindukia, kinyume na mafundisho ya dini zetu sambamba na hata mapendekezo ya ki Afya.

tuunganeni kama hivi ili kuikoa Tanzania yetu
 
kwanini watu ambao hawajawahi kuwa na kisukari lakini wakipata covid wakipima sukari inakuwa juu??!!
lakini baadae wakipona sukari inakuwa normal tuu km mwanzo??
hili sijaligundu mkuu, ila nitalifanyia quick reseaech ili nipate utambuzi wake. Ahsante kwa kunipa kitu kipya
 
Karibu kaka, ni wajibu wetu sote kutumia mitandao kwa matumizi chanya.

Kura yako muhimu sana
 
Ilim mujarab, shukran kwa andiko hili.

Hakika Kinga ni bora, na kwa walio pata mtihani tunawaombea mpone kabisa kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu.

Nje ya Mada kidogo, kura ya nini??
 
Nje ya Mada kidogo, kura ya nini??
Ndugu, Rejea hii mada: Shindano: Uandishi wa Mtandaoni wenye kuleta tija (Stories of Change)

Picha
1626581378266.png
 
Back
Top Bottom