Watanzania tupo hatarini, tunaweza kupata corona kwa kula mapapai

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
WHO mlisema mnatoa ushauri wa kitaalamu kuhusu corona. Sisi Rais wetu mwenye PhD ni mtaalamu zaidi na kwa mapenzi aliyonayo kwetu sisi raia wake amepima baadhi ya vitu kama mbuzi na mapapai, na kugundua kuwa mbuzi na mapapai vyote Viña virusi vya corona.

Kumbe Yale madumu ya maji tiririka na barakoa hazitusaidii kitu . Maambukizi halisi yako kwenye chakula na matunda.

Shukrani nyingi kwa Rais wetu.
 
nasikia zile mashine ni za kupima DNA ili kugundua Corona na Mapapai yana RNA ,kuna mkenya amenichekesha anadai ndio maana hatutoi daily update za Corona kwa sababu tunapima mapapai na mafenesi
 
Hapana chezea Pombe....kama siyo mashine zilizoborongwa kunao watu waliolishwa chirimiri, ama wakavuta gundi ya viatu😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…