Watanzania tupunguze ushabiki na uzandiki kwa mfano ni kifo cha mtoto mwenye ualbino (Asimwe Novart) kilichotokea huko Kagera

Watanzania tupunguze ushabiki na uzandiki kwa mfano ni kifo cha mtoto mwenye ualbino (Asimwe Novart) kilichotokea huko Kagera

Accumen Mo

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2022
Posts
18,036
Reaction score
39,882
Habari ndugu zangu watanzania,

Kwanza poleni na msiba huu tena unaleta aibu katika jamii ya kitanzania, pia napenda kupongeza hatua mbalimbali zilizoendelea kuchukuliwa ni pamoja na wananchi kuandamana huko kagera , polisi nao kuwashikilia watuhumuwa wawili mpaka sasa kutokana na uchunguzi wa awali .

Narejea kweny mada, kwa nn sisi ni wapenda ushabiki na uzandiki kiasi hichi? Rejea kukamatwa kwa watuhumiwa wawili ambao mmoja wapo ni baba mzazi wa mtoto.

Kwa nn watu wanaongelea yule mwingine ambaye anahusishwa na mambo ya dini? hapo ushabiki ndio unapoanza.

Hivi kweli watu wamsakame yule mtu baki kwa mtoto haijalishi kama ni kiongozi wa dini au laah, halafu wamuache kumsakama baba yake mzazi.

Kama ni kweli wanahusika basi huyo baba yake mtoto ndio mjinga mkubwa zaidi, ebu jaalia mwanao kabisa wa kumzaa kama hauna huruma huyo mtu baki anaweza kumuonea huruma kweli mwanao?​
 
Nadhani kiongozi wa dini anafuatiliwa na watu wengi.
Sawa ila kati ya hao wawili mzazi bado ni sensitive sana kwa mtoto kuliko huyo mwingine ni mtu baki kwa mtoto .

Katika sakata hili ilitakiwa baba wa mtoto ndio wakuzungumziwa sana. Huyo ndio anaishi na mtoto kwa karibu .
 
Maoni yangu binafsi.

Haya matukio yanatokea sana hapa nchini lakini kwanini tukio hili la sasa limepewa nafasi kubwa sana?

Nadhani ni njia ya kuhamisha upepo kuwafanya watu kuwa na focus na hili jambo hasa katika mitandao.
 
Habari ndugu zangu watanzania ,

Kwanza poleni na msiba huu tena unaleta aibu katika jamii ya kitanzania , pia napenda kupongeza hatua mbalimbali zilizoendelea kuchukuliwa ni pamoja na wananchi kuandamana huko kagera , polisi nao kuwashikilia watuhumuwa wawili mpaka sasa kutokana na uchunguzi wa awali .

Narejea kweny mada , kwa nn sisi ni wapenda ushabiki na uzandiki kiasi hichi ? Rejea kukamatwa kwa watuhumiwa wawili ambao mmoja wapo ni baba mzazi wa mtoto .

Kwa nn watu wanaongelea yule mwingine ambaye anahusishwa na mambo ya dini ? hapo ushabiki ndio unapoanza .

Hivi kweli watu wamsakame yule mtu baki kwa mtoto haijalishi kama ni kiongozi wa dini au laah , halafu wamuache kumsakama baba yake mzazi .

Kama ni kweli wanahusika basi huyo baba yake mtoto ndio mjinga mkubwa zaidi , ebu jaalia mwanao kabisa wa kumzaa kama hauna huruma huyo mtu baki anaweza kumuonea huruma kweli mwanao?​
Ata hii mada umeileta kwa nia unayojua wewe. Katika wafia dini hapa jf. Wewe huwezi kukosekana hivyo ajenda yako inajulikana kwa nini umeanzisha hii mada. Kua tu mkweli unaona raha sana jambo baya likiwapata upande uliotajwa
 
Ukishakuwa kiongozi wa dini unapaswa kuwa mfano. Macho mengi yanakuangalia. Unavyokengeuka basi jamii lazima ipatwe na mshtuko.

Lakini pia, pengine anazungumziwa yeye kwa sababu ndiye kafanya dili hilo kwa nafasi kubwa. Moja, kuongea na mzee mwenye mwana. Pili, kumsaka mganga na gharama zote juu yake.

Jamii ina imani kubwa sana juu ya viongozi wa dini. Hivyo, hii kelele inaweza kusaidia kuamsha uelewa kuwa hawapaswi kuaminiwa 100%. Ukiacha Masheikh kulawiti madrassa, wapo viongozi wengi wanaopaswa kutiliwa shaka.

Hivyo, yeye ndiye stakeholder mkubwa zaidi kwenye dili hilo la kiharamu. Anapaswa kulaaniwa zaidi.

Wavaa makobaz (akiwemo muanzisha mada) wanaweza kuwa na agenda nyingine, ila kwa ukweli na uhalisia wa tukio basi anayepaswa kupigiwa kelele zaidi ni huyo mwanaharamu.
 
Habari ndugu zangu watanzania,

Kwanza poleni na msiba huu tena unaleta aibu katika jamii ya kitanzania, pia napenda kupongeza hatua mbalimbali zilizoendelea kuchukuliwa ni pamoja na wananchi kuandamana huko kagera , polisi nao kuwashikilia watuhumuwa wawili mpaka sasa kutokana na uchunguzi wa awali .

Narejea kweny mada, kwa nn sisi ni wapenda ushabiki na uzandiki kiasi hichi? Rejea kukamatwa kwa watuhumiwa wawili ambao mmoja wapo ni baba mzazi wa mtoto.

Kwa nn watu wanaongelea yule mwingine ambaye anahusishwa na mambo ya dini? hapo ushabiki ndio unapoanza.

Hivi kweli watu wamsakame yule mtu baki kwa mtoto haijalishi kama ni kiongozi wa dini au laah, halafu wamuache kumsakama baba yake mzazi.

Kama ni kweli wanahusika basi huyo baba yake mtoto ndio mjinga mkubwa zaidi, ebu jaalia mwanao kabisa wa kumzaa kama hauna huruma huyo mtu baki anaweza kumuonea huruma kweli mwanao?​
Mkuu kwaanzia leo you have got my absolute respect. Hivi karibuni nimekuwa na kustudy kwa karibu nikagundua wewe siyo msela mwenzetu kama kina adriz Chaliifrancisco hydroxo. Na huenda hupo hadi kwenye kitengo.
 
Maoni yangu binafsi.

Haya matukio yanatokea sana hapa nchini lakini kwanini tukio hili la sasa limepewa nafasi kubwa sana?

Nadhani ni njia ya kuhamisha upepo kuwafanya watu kuwa na focus na hili jambo hasa katika mitandao.
Ni ujinga wa watu wachache waliokosa weledi.watu wanakurupuka na kushadadia mambo wasioyoyajua.wengine wamepewa dhamana kubwa na watz lkn matendo yao ni ya kijinga.kama hakuna mifumo ya kuwajibishana ktk nchi hii huu upuuzi utaendelea kujikita kileleni
 
Viongozi wa Kanisa Katoliki Kagera.
Screenshot_20240620-124948.jpg
 
Habari ndugu zangu watanzania,

Kwanza poleni na msiba huu tena unaleta aibu katika jamii ya kitanzania, pia napenda kupongeza hatua mbalimbali zilizoendelea kuchukuliwa ni pamoja na wananchi kuandamana huko kagera , polisi nao kuwashikilia watuhumuwa wawili mpaka sasa kutokana na uchunguzi wa awali .

Narejea kweny mada, kwa nn sisi ni wapenda ushabiki na uzandiki kiasi hichi? Rejea kukamatwa kwa watuhumiwa wawili ambao mmoja wapo ni baba mzazi wa mtoto.

Kwa nn watu wanaongelea yule mwingine ambaye anahusishwa na mambo ya dini? hapo ushabiki ndio unapoanza.

Hivi kweli watu wamsakame yule mtu baki kwa mtoto haijalishi kama ni kiongozi wa dini au laah, halafu wamuache kumsakama baba yake mzazi.

Kama ni kweli wanahusika basi huyo baba yake mtoto ndio mjinga mkubwa zaidi, ebu jaalia mwanao kabisa wa kumzaa kama hauna huruma huyo mtu baki anaweza kumuonea huruma kweli mwanao?​
Kilichopelekea kumsakama baba paroko, ni kutokana na taarifa kuwa yeye ndo aliyekuwa akimshawishi baba mzazi, sasa jamii ilitegemea kuwa yeye ndo awe mstari wa mbele kukemea kama wanavyokemea wakiwa Madhabahuni nadhani msakamo umeanzia hapo
 
Wananchi tunaiomba Serikali hii kesi iwe ya public.
Wananchi wote tunataka kuifuatilia Neno hadi neno.
Hatutaki Paroko aonewe.
Tunataka kumsikiliza live kabisa na baba wa mtoto.

Hili tukio limetuhuzunisha sana sisi wananchi.
Tunataka tufamishwe tarehe rasmi ya kesi
Na muda na mahali kesi itakapo sikilizwa.

Wengine tupo radhi kusafiri kwa ghalama zetu ili tuisikilize hii kesi live bila chenga.
Mtoto wetu, Binti yetu ametuhuzunisha sana sana na hatuna msamaha kabisa kwa hili tukio.
 
Back
Top Bottom