Watanzania tusijidharau kupita maelezo, ushindi dhidi ya Uganda utujaze mioyo ya kujiamini

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2015
Posts
18,487
Reaction score
13,611
Mwaka 1980 ni miaka 39 iliyopita. Ni kitambo. Tanzania ya wakati ule ilikuwa bado ni nchi ndogo sana. Kiuchumi na hata katika suala la idadi ya watu.

Mwaka ule mtu ukikatiza mbele ya meza ya magazeti unakuta yanayouzwa hayazidi matatu. Uhuru na Mzalendo, daily news na sunday news, siku za jumamosi litatoka gazeti la mfanyakazi.

Ni mwaka ambao wimbo wetu wa taifa uliimbwa kabla ya mechi tatu za hatua ya makundi ya kombe la mataifa huru kule Nigeria. Ni mwaka ambao ulikuwa ndio wa mwisho kwa Taifa Stars kuonekana katika michuano mikubwa.

Vijana kina Samatta, Msuva na wengine wametutoa kimasomaso na wimbo wetu utasikika tena kule Misri katikati ya mwaka huu. Vijana wetu wataonekana kwenye runinga wakiuimba wimbo huku mikono yao ikiwa katika eneo la moyo.

Heshima imerudi tena, na heshima hii iwe ni somo muhimu kwetu. Tuache kujiona hatuwezi, tuache kuwa na roho ya kuiombea mabaya nchi ambayo wazazi wako wote wawili wamezaliwa na kukulea wewe kwa upendo wa hali ya juu.

Kufanikiwa kwenda Misri inaweza kuonekana ni bahati kama mtu hajishughulishi katika kuwaza kwa kina.

Samatta yupo Belgium pengine msimu ujao anaweza kununuliwa Uingereza. Msuva yupo Morocco
pengine msimu ujao anaweza kununuliwa Hispania. Ambokile yupo Afrika ya Kusini pengine misimu miwili ijayo anaweza kuuzwa Ulaya.

Wachezaji wetu wameanza kujiamini na kutoka nje ya Tanzania kwa kasi kubwa, tuwaunge mkono kwa kila namna. Wanajazwa wivu kila wanapomuona Samatta akifunga magoli Belgium.

Ikiwa vijana wadogo wanajiamini na kwenda nje kutafuta fursa, inashangaza sana kumuona mtu ambaye anaitakia mabaya Tanzania. Inakera pia kumsoma mtu mwenye kuombea mabaya Taifa Stars isionekane kimataifa.

Watanzania tuachane na hizi hulka za kujiona hatuwezi, kujiona sisi tumeumbiwa kukosa.
 
Heshima gani imerudi? Kila mtu nasikia anasema heshima yetu imerudi, heshima gani? Tulikua na heshima gani na tuliipoteza lini?

Heshima , heshima heshima, heshima gani hiyo?

Jambo la pili, ilikua jana obvious ushindi uwe kwetu kwa sababu Uganda had nothing to loose. Hiyo heshima tuliyoipata ni ipi?
 
Mkuu, kitendo cha kushiriki AFCON ni heshima kwa nchi. Wewe unaweza usiione kwa mtazamo wako na ni haki yako kuwa na mtazamo huo.
 
..kuna baadhi ya waTz hawatendewi HAKI na watawala wa nchi hii.

..pia watawala wamejenga mazingira kwamba hiyo timu si ya waTz wote, bali ya kwao watawala.
 
Mkuu, kitendo cha kushiriki AFCON ni heshima kwa nchi. Wewe unaweza usiione kwa mtazamo wako na ni haki yako kuwa na mtazamo huo.
Hakuna kitu hapo mkuu, hii ni sawa na mwl awahamishe mtu wa 1 hadi 20 katka darasa halaf matokeo yajayo wewe uliyeongoza unashangilia kwa ushindi ulioupata, mimi sijaona mpira wa kutufanya tutoboe misri.
 
Inasikitisha Sana Mwaka Jana Nilienda Lagos Nigeria Tanzania Hawaijui Kabisa Mtanzania Pekee Anaejulikana Kidogo Ni Diamond Platnumz. Ni Muda Wa Kujitangaza Sasa
 
Hakuna kitu hapo mkuu, hii ni sawa na mwl awahamishe mtu wa 1 hadi 20 katka darasa halaf matokeo yajayo wewe uliyeongoza unashangilia kwa ushindi ulioupata, mimi sijaona mpira wa kutufanya tutoboe misri.
Mkuu tuliposhiriki AFCON ya mwisho mwaka 1980 wengine tulikuwa watoto wadogo ambao ili kwenda mjini ni lazima uende na mtu anayekushika mkono.

Ni kitambo sana. Tatizo la wabongo hatuna unyenyekevu, tunajiona kuwa tunastahili mambo makubwa sana.
 
Acheni mbwembwe....
Maisha yanaendelea....
Utafikiri mmechukua ubingwa...wa afcon

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
1980 ni kitambo sana. Hatujachukua kombe la dunia, bali tumepata nafasi ya kuvitangaza vipaji vyetu. Kina Msuva na Mudathir Yahya wamepata mahali pa kuonyesha uwezo wao, washindwe wenyewe.
 
Wamejitahidi sana wanastahili pongezi ila wasibweteke. Serikali pia iongeze nguvu yenye muendelezo
 
Hakuna kitu hapo mkuu, hii ni sawa na mwl awahamishe mtu wa 1 hadi 20 katka darasa halaf matokeo yajayo wewe uliyeongoza unashangilia kwa ushindi ulioupata, mimi sijaona mpira wa kutufanya tutoboe misri.
Nakuhakikishia Tanzania hatuna mpira wa wakupata hata point 1 Misri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…