Watanzania tutabadilika lini?

Watanzania tutabadilika lini?

kangesa

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2023
Posts
551
Reaction score
1,063
Habari ya weekend na simba day kwenu wote?

Watanzania ifike mahali tubadilike,kuna vitu kwa binadamu kuvishangaa mtu akikuuliza unaonekana ni ushamba na kutojitambua kabisa.

Iko hivi,leo nilidamka mapema kwenda k/koo. Sasa kabla ya kutoka ikabidi ninywe pepsi ili kuweka koo sawa

Nimefika kule katika mizunguko na hali ya hewa leo na haka kamvua nikabanwa na mkojo nikiwa bado na mizunguko yangu nikajisemea ngoja kwanz nimalize mishe zangu ndyo nifute washing rooms zilipo.

Namaliza mizunguko yangu najikuta nipo maeneo ya mtaa wa agrey pale,najaribu kutafuta eneo la kujihifadhi nakosa. Nikaona syo kesi wacha niulize wafanya biasgmhara wa hapa.

Aisee nimeuliza kama watatu hivi lakini cha ajabu wote wanaishia kunishangaa kana kwamba ni kama ushamba au aibu sana kwa kitu nachouliza.

Nimezurula sana baadae nikaona bora nipande gari zinazotoka karume kwenda mnazi mmoja pale kituo cha mwisho nikajisaidie pale kwasabu ndipo napopajua.

Niliamua kupanda gari japo ni kipande kifupi kwasababu kutembea kwa miguu na nilivobanwa nahisi ningetrend mitandaoni zaid ya simba day.

Isivyo bahati tena nafika pale mnazi nakuta wamefunga,yaani wanakarabati. Nikamuuliza jamaa yuko mle ndani ananiambia labda niende kwenye stand ya gongo la mboto.

Ikabidi jamaa yule nimuombe kwa kuuieleza kwa uchungu mno ndyo akaniambia niingie mle ndani ase nikamaliza shida yangu.

WATANZANIA tubadilike!!!! Kuuliza baadhi ya vitu isionekane ni ajabu.
 
Kkoo vyoo vya kulipia vipo vingi Sana cjui we ulikosaje hata Kwa kuangalia mwenyewe Tu!
 
Kariakoo vyoo viko vingi mno ndio maana hakuna complain ya “vyoo”
Ngoja nikupe moja mbili

1. Sehem yeyote yenye bango la HOTEL, LODGE ingia huko choo ni bure kama Wanyama na Valentino

2. Sehemu za kula RESTAURANTS kama Raha ni bure

3. Sehemu zenye bango “CHOO CHA KULIPIA” kama stand ya Gerezani ya mwendokasi
 
Mkuu siku nyingine tafuta ukuta ugeukie Kisha kojoaa,ukimaliza kun'guta sepa haya mambo yakuuliza wanaume wenzio ukojoe wapi ni mambo ya upinde.Na inawezekana uliomba wakuonyeshe( washroom)..what the fvck
 
Back
Top Bottom