econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 20,189
- 29,663
Kwa Sasa kumezuka madhehebu mengi ndani ya dini ya ukristo. Kuna madhehebu baadhi hayafuati misingi ya kikristo bali Imani potofu ambayo ni kinyume na ukristo lakini tunalazimisha ni ya kikristo.
Madhehebu yaliyomo kwenye ukristo lakini yapo tofauti na imani ya kikristo tunayaita ni cult.
Sifa za cults ni Kama ifuatavyo.
1. Msingi wake ni kiongozi wa kanisa sio Mungu. Cults nyingi zinaamini ya kwamba kiongozi wao ndio kila kitu na yeye ndio mwenye nguvu. Humsikiliza yeye na kufanya yale ambayo anawatuma kufanya hata Kama ni kosa au dhambi. Kwa mfano, kiongozi wa cult moja anaitwa charles mason aliwatuma waumini wake wakafanye mauaji na kweli waumini wake waliua watu wengi Sana. Maana kiongozi wao kawatuma.
2. Cults huyapa nguvu mafunuo na maono kuliko Neno la Mungu au Biblia. Kiongozi akiota ndoto usiku au amepata mafunuo basi hiyo ndoto na mafunuo ndio yanakuwa msingi wa Imani wa Hilo dhehebu hata kama linaenda kinyume na Neno la Mungu.
Mfano, Kule Uganda kiongozi mmoja wa dhehebu aitwaye kibwetere aliota ndoto kwamba mwisho wa dunia ni mwaka 2000. Waumini wake wakamwamini baadala ya kufuatilia Biblia Inasemaje kuhusu siku za mwisho, kwamba ule mwisho hautafika mpaka injili imehubiriwa Mataifa yote.
3. Cults hupunguza nguvu ya uwezo wa jina la Yesu Kristo. Kwenye Cults jitihada kubwa hufanyika kuonesha kwamba jina la Yesu Kristo halina mamlaka hivyo uponyaji na maombezi hufanyika kwa kutumia vitu vingine Kama maji, mafuta, chumvi, udongo na keki.
Kwenye Imani ya kikristo, Jina la Yesu Kristo ndilo lenye mamlaka kuliko yote, hivyo mamlaka ya kutoa pepo na maombezi yasimame katika kutumia Jina la Yesu Kristo. Hivyo Cults, huondoa hayo mamlaka na kuyapa vitu vingine na kuaminisha ya kwamba hivyo vitu ndivyo vitakusaidia. Hivyo Imani juu ya Yesu Kristo inaondoka na imani inakuwa kwenye mafuta na maji nk.
4. Cults huamini kwenye ishara na miujiza sio utakatifu. Misingi ya hizi cults Ni miujiza na ishara mbalimbali. Hivyo waumini hata wawe wazinzi, nyumba ndogo, wezi, wadengenyaji nk, Hilo halipewi nafasi. Kinachopewa nafasi ni unabii na uponyaji. Hivyo waumini wengi wa Cults hawaendi kumtafuta Mungu au mabadiliko ya kiroho bali wanaenda kutafuta uponyaji na ishara lakini dhambi zipo palepale.
5. Mwisho wa hizi cults huwa ni mbaya Sana. Cults nyingi hazina mwisho mwema. Fuatilia kuanzia Jim Jones , David Koreishi na Applewhite utagundua Cults hazina mwisho mwema kabisa. Kwa mfano Jim Jones aliua waumini wake wote wapatao 900 kwa njia ya sumu akiwaambia ni meza ya Bwana mwaka 1978.
Hitimisho. Ni muhimu sana kutofautisha Kati ya Cult na ukristo na sio kuvichanganya pamoja.
Cult ni tofauti na ukristo. Ukiona kiongozi wa dhehebu anatumia uchawi au utapeli huyo sio mkristo, maana misingi ya kikristo inataka utumike ndani ya mapenzi ya Mungu. Ndio maana hata Biblia inasema ya kwamba, " siyo wote waniitao Bwana Bwana wataingia kwenye ufalme wa Mungu Bali wale watendao mapenzi ya Mungu".
Hivyo watakuja watu wakisema tulitoa pepo kwa jina lako au tulitoa unabii kwa jina lako atawaambia tokeni hapa siwajui nyie mtendao dhambi.