Watanzania tutumie fursa ya amani kufanya biashara

Isombilege

Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
92
Reaction score
54
Wapendwa salaamu;
Mungu Mwenye enzi na mamlaka zote anatulinda vyema sisi kama Taifa pendwa la Tanzania.Binafsi naipenda Tanzania.

Nijikite kwenye hoja yangu :
Tanzania ni nchi ya amani ambayo ni rahisi kufanya biashara kwa KUZINGATIA sheria zilizopo.

Nashangazwa sana na wafanya biashara kufunga biashara zao mapema sana
Yaani saa nne usiku unakuta maduka yote yamefungwa hadi maduka ya madawa sasa najiuliza hii amani tuliyonayo tunaitumiaje kama kichocheo cha kibiashara?

Mwezi wa 8 nilikuwa na Safari nakwenda
Arusha, mie napenda kusafiri usiku hivyo saa 5:45 nilikuwa Msata.Wenyeji wa pale wafanya biashara walionekana kukerwa na sheria zinazowataka wafunge biashara saa 5 haswa ukizingatia mahali pale ni barabarani.

Huku Dsm ikifika saa sita nihekaheka mapolisi kukamata wafanyabiashara waliokiuka hii sheria.

Kwa vile Tanzania ni Taifa linalokua kiuchumi napendekeza sheria zibadirishwe watu wapewe muda wakufanya biashara
 
Viongozi wetu wanataka uchumi ukue wakati hawajui hata vitu virahisi tu vinavyochochea uchumi kukua. Majiji makubwa ya wenzetu maduka hayafungwi 24/7. Hapa kwetu kuna muda mnaambiwa msifungue biashara kuanzia asubuhi mpaka saa 4 eti siku ya usafi. Pathetic.
 
sera zinaruhusu??? TRA wametujengea mazingira ya kufanya biashara???
 
Tatizo viongozi wa kikoromije huwa hawa hawafikirii vizur, Sasa cjui uchumi utakuaje wakati watu wanapangiwa mida was kufanya biashara
 
Tatizo ni sheria ka mtoa mada ulivyosema kunahaja ya sheia kubadilika ili watu wafanye biashara wakati wote ila kunachangamoto ya usalama ka unavyofahamu vyombo vyetu vya ulinzi nguvu yao katika number ni ndogo haiwezi kutosheleza ulinzi kikamilifu kwahiyo kunahaja ya vyombo vyetu kuongezewa nguvu vifaa pia idadi yao kuongezeka ili iweze kutawanyika sehemu kubwa maana wote ni mashahidi kuwa kunabaadhi yavijiji kibao havina hata kituo cha polisi kisa uhaba wa askari hata huku mjini nako hawatoshelezi,,

sheria zetu pia zifanyiwe marekebisho ziruhusu biashara zifanyike wakati wote usafiri wakati wote yani kusiwe na kipingamizi chochote kikubwa ni wao kuhakikisha usalama katika mazingira hayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…