Tanzania ni nchi yenye Mipango, sera na mikakati mizuri lakini mipango hiyo huwa inatekelezwa chini ya kiwango au kutofikiwa kabisa mfano ukisoma dira ya maendeleo iliyo andikwa mwishoni mwa miaka ya tisini ikilenga mpango wa maendleo wa miaka 25 kutoka 2000 hadi 2025 mipango ile kama ingetekelezwa kwa dhati kwa kila mdau kutimiza wajibu wake basi tanzania isingekua nchi masikini leo hii.
Katika kuifikia Tanzania tuitakayo ni wajibu wa kila mtanzania kuwajibika kwa kutimiza majukumu yake ipasavyo ili tuweze kufikia maendeleo ya kweli. Andiko hili litaelezea kwa kina ni kwa namna gani kila mtanzania akiwajibika ipasavyo katika nafasi aliyopo basi ujinga,umasikin na maradhi hayata kuwa matatizo yanayotushinda kuyatatua. Nitaelezea uwajibikaji wa watanzania kisiasa, uchumi, utunzaji wa Mazingira, maadili,utamadi na michezo.
Uwajibikaji katika siasa na utawala bora, inasikitisha pale unapo msikia kiongozi wa juu wa nchi anapo idharau katiba pale anaposema katiba ni kijitabu tu kinaweza kikawepo na kisifatwe. Kwa kauli kama hizi tusitegeme utawala bora na wezi wa mali za umma kushughulikiwa ipasavyo kwani katiba kama msingi wa kutambua wajibu wao ni upi hawaiheshimu.
Mwaka 2020 ulipitishwa muswada Bungeni uliokuwa unawapa ruhusa ya viongozi wa mihimili mikuu ya serikali kutowajibishwa pale wanaposhindwa kutimiza wajibu wao na hata wakishitakiwa ni mwanasheria wa serikali atashitakiwa na sio viongozi wakuu wa mihimili sheria kama hizi zinaonyesha ni kwa kiasi gani viongozi wa mihimili wanakwepa kitimiza wajibu wao na kwa hivo tusitegemee kama mtumishi wa ngazi ya chini akikosea atachukuliwa hatua mfano kuna kesi nyingi huwa zinafutwa mahakaman na serikali kwa kigezo anaetakiwa kupeleka mahakaman kesi hizo ni mwendesha mashitaka ya serikali. Lakini na sisi wananchi lazima tuwawajibishe viongozi wetu pale wanapokosea kwa kubadili katiba ili waweze kushitakiwa pale wanapo kosea au kushinikiza wajiuzulu.
Uwajibikaji katika Uchumi, Bajeti ya nchi yetu haijitoshelezi na hatuwezi Jenga uchumi imara kama hatuna fedha za kutosha kugharamia miradi ya maendleo. Wananchi wajibu wetu ni kulipa kodi na tozo mbalimbali ili serikari iweze kugharamia miradi hiyo. Kitu cha kusikitisha fedha za umma zinaibiwa na hakuna anaewajibishwa na wananchi hatutimizi wajibu wetu wa kulipa kodi kwani tumepoteza imani tunajua kodi tunazo lipa zinaliwa na wajanja wachache.
Uwajibikaji katika utunzaji wa Mazingira, Wananchi inabidi tutimize wajibu wetu kwa kuacha kulima karibu na vyanzo vya maji,ujenzi holela wa makazi na viwanda, matumizi ya kuni na mkaa vyote hivi vinaharibu mazingira yetu. Sera za mipango miji zipo , sheria za kutunza mazingira tunazo, kinacho kosekana ni uwajibikaji kwa serikari na wananchi, serikari isimamie vyema hizi Sheria na kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi.
Uwajibikaji katika michezo, utamaduni na maadili yetu, katika michezo wana michezo na wapenzi wa michezo hututimiz wajibu wetu kwa kuchangia mapato katika timu zetu mtu halipi ada ya uanachama, hanunui jezi halisi za timu na haendi uwanjani lakini anategemea timu yake iwe nzuri kiuchumi bila yeye kutekeleza wajibu wake wa kuchangia mapato katika timu.
Ni kawaida siku hizi matendo ya ovyo kufanyika hadharani na wanajamii kuyakalia kimya masuala kama ya ushoga, ubakaji, ukatili wa kijinsia na mengineyo hayatiliwi mkazo na wanajamii kitu ambacho ni hatari kwa ustawi wa vizazi vijavyo. Mashoga wapo tunaishi nao katika jamii, michezo ya kubahatisha inavomaliza nguvu kazi vijana hawafanyi kazi wanaamini katika bahati nasibu. Ni wajibu wetu kama jamii kuungana pamoja na kupinga vitu hivyo lazima tuwe na mpango kama Taifa wa pamoja kupinga maswala hayo ili kulinda kizazii hichi na vizazi vijavyo.
Ili kufikia tanzania tuitakayo lazima kama taifa tutambue umuhimu wa kila mtu kuwajibika katika ngazi zote na ni lazima kuwe na somo maalumu katika hatua zote za elimu kuanzia msingi mpaka chuo kikuu litakalofundisha uwajibikaji na uzalendo kwa taifa hili. Kwa sababu Mipango ipo na ni mizuri sana shida ni uwajibikaji watu hawatekelez majukumu yao ipasavyo.
Vijana wengi tunataka maendeleo ya haraka haraka bila kutimiza wajibu wetu wa kufanya kazi kwa bidii. Katika utunzaji Mazingira wananchi kwa kutokujua au kukusudia au ugumu wa maisha wanaharibu mazingira, Serikali ipo inaona mashirika yapo yanaona na wanaofikishwa mbele ya sheria hongo na rushwa vimetawala, lakini pia, halmashauri nyingi kuna upotevu wa mapato yanayo kusanywa kwa kisingizio cha mfumo lakini hakuna hatua kali zinachukuliwa dhidi ya walioiba fedha hizo
Ni wakati sasa kama taifa kubadili Katiba Mpya ili kila mtu aweze kuwajibishwa pale anaposhindwa kutimiza wajibu wake mfano kama Rais alipokuwa madarakani alifanya makubaliano au akaingia mikataba ya ovyo au akatoa na kupokea rushwa lazima katiba yetu iweze kumuwajibisha sababu hakuna sababu ya msingi kumpa Rais au mtu yeyote kinga wakati ni mwanadamu anaweza kukosea na lazima awajibishwe kwa makosa yake.

Upvote
2