Trust None
JF-Expert Member
- Feb 12, 2018
- 1,260
- 4,419
Tulishaambiwa mapema kuwa MB1 itauzwa kati ya Tsh. 2 hadi 9 lakini kwa kuwa wengi wetu tuliikimbia hesabu, hatukuliona hili. Mfano: MB 1 ikiuzwa kwa Tsh. 2 maana yake GB1 yenye MB 1000 itauzwa sh. 2000, MB 1 ikiuzwa kwa Tsh. 3 ni kwamba GB1 itauzwa Tsh. 3000 na kuendelea kulingana na hesabu hiyo.
Watanzania ni wavumilivu sana, tumevumilia kupanda kwa bei za sukari, mafuta pamoja na bidhaa zingine, iweje tushindwe hili la vifurushi?
Watumishi wa umma tumevumilia kutopanda madaraja, kutopata increment, kutopanda vyeo na kutobadilishiwa miundo ya utumishi, kutopata uhamisho hata wa kubadilishana, iweje tushindwe hili la vifurushi?
Wahitimu wa vyuo tumevumilia kukaa mtaani kwa miaka mingi bila ajira, iweje tushindwe hili la vifurushi?
Wakulima tumevumilia kukosa bei nzuri za mazao yetu, tumedhulumiwa, korosho ni kilio, siyo pamba, mbaazi wala kahawa yenye unafuu, iweje tushindwe hili la vifurushi?
Tumevumilia kikokotoo, kupanda riba ya HESLB (8%_15%), wastaafu kukaa miaka bila kupata mafao, iweje tushindwe hili la vifurushi?
Wafanyabiashara tumevumilia kodi kubwa za bidhaa tunazolangua, iweje tushindwe hili la vifurushi?
Hii ndo Tanzania ya wanyonge, 'wanyonge' laweza kuwa na maana mbili:
1. Kitenzi
2. Nomino