Watanzania tuwe wazalendo, utanzania ni kama ngozi

Watanzania tuwe wazalendo, utanzania ni kama ngozi

Lubengera

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2019
Posts
963
Reaction score
1,551
Kiukweli inasikitisha sana kuwa, moja ya mambo yanayo rudisha nyuma maendeleo ya miradi na maendeleo kwa ujumla ni sheria ya manunuzi ya umma.

Nadhani wengi wetu tumeona waraka kupitia whatsap grup na sociali media nyingine juu ya kurekebisha kanuni za manunuzi ya umma.

Kwakuwa hii ndio fursa kwetu, kwann tusitoe maoni yetu hasa kwa maeneo ambayo hayako sawa, ili kuharakisha upatikanaji wa bidhaa na huduma.

Kupitia uziefu wangu wa ukaguzi na maoni ya watumishi, Tanzania bado tuna mapungufu ya uboreshaji wa sheria pamoja na kanuni zake.

Niwazi kuwa sheria zimekuwa zikitungwa kama kumkomoa anae zisimamia, lakini impact yake inaonekana kwa taasisi kwa ujumla! hii haikubaliki..

Mimi binfsi kwa uzoefu wangu, nashauri haya.

1. Sheria ipunguze nyaraka za manunuzi, paper works (hili ni tatizo) ndio mana watu wa manunuzi siku zote ni watu wanao onekana kukiuka taratibu ambazo kwa wingi wake hazina madhara wala hasara.

2. Sheria bado inamapungufu makubwa katika kutambua professional ya watu wa manunuzi, ndio mana inaipa bodi ya tenda nguvu kuliko watu walio somea manunuzi pasee.

3. Ni wakati sasa wa kupunguza mlolongo, bureucracy katika manunuzi mfano, kutoa bodi ya zabuni, na bodi ya tathmini ili kupunguza mlolongo wa taratibu, na kubaki na body itakayo simamia manunuzi kwa ujumla ikisaidiwa na wataalamu wa manunuzi ( pmu).

4. Sheria za manunuzi ya dawa na vifaa tiba ziwe na sifa za ziada tofauti na manunuzi ya karatasi, computer na vitu vingine, mfano, wanapokosa dawa msd sheria iruhusu kwenda kwa wauzaji bila kufuata taratibu za tenda. kwa watu tuliowahi kukosa dawa hospitali, hii ni sabab kubwa sana , taratibu ni kikwazo cha upatikanaji wa dawa mahospitalini. msd wawe na wauzaji waliyo tayari ili kurahisisha upatikanaji wa dawa

5. Sheria iongeze threshold ya ununuzi wa manunuzi modogo madigo, iliyopo sasa ni 5m, nadhani kwakuwa 5m ya sasa imekuwa haina thaman sana, basi waongeze hadi kufikia 15m. hii itawasaidia sana hasa watu walioko hospitalini.

Naomba na wenye maoni zaidi waje kuchangia juu ya hili. nadhani waiziri mwenye dhamana atachukua yaklyo muhim zaidi.

Tuachane na mambo ya manzoki wala mayele, hawa sio watanzania, na fedha zao hazituhusu! hadi leo ilipaswa kuwa na wimbo wa lunyamila, boko, mrisho ngasa etc.

Lakini, tumekalia kupiga makelele ya siyo na faida kwa nchi yetu kwa ujumla.

Karibuni kwa michango
 
1-2.jpg
 
Kuwa mzalendo uku ukiwa una nuka umasikini wa kujitakia kwa kukumbatia serikali ovu na najisi ni ujinga ambao hata shetani anashangaa

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Toa maoni yako, usikate tamaa, Tanzania ni yetu sote! mabadiliko yanaanzia kwako na kwangu.

Nataman sana watu kitoa maoni yao! naamini kuna mazuri sana yatachikuliwa
 
Toa maoni yako, usikate tamaa, Tanzania ni yetu sote! mabadiliko yanaanzia kwako na kwangu.

Nataman sana watu kitoa maoni yao! naamini kuna mazuri sana yatachikuliwa
Mazuri gani yatachukuliwa ukitoa maoni? tuanze na kwako,Leta maoni yako ambayo Usha wahi toa na yakafanyiwa kazi na viongozi wa CCM

Marehemu kolimba aliwahi sema "CCM imepoteza dira"hivyo usije tarajia chama kilicho poteza dira na mvuto kutuvusha kwenye matatizo yetu.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
hakuna nchi yoyote duniani ambayo imepinga hatua ya kimaendeleo bila kutoza tozo/kodi.

Watanzania hatuna budi kubadilika, hakuna atakaye ijenga nchi yetu bali ni sisi wenyewe na hakuna misaada ya buree.

Hiyo misaada inayo tolewa kwa nchi pia ni Tozo na kodi za Raia wa nchi za Ulaya/Marekani n.k.

Tulizoea sana vya bureee na matokeo yake tukalemaaa sasa tuache upuuzi, tulipe tozo na Kodi kwa maendeleo yetu.
 
MKuu, amini kuwa Jukwaa la JF lina mchamngo mkubwa sana katika kuboresha mambo mengi yanayofanyika katika wizara zetu, na hasa sera na mipango.

Juzi tu swala la luku na majengo, Kuna mwananJF mmoja simkumbi Jina lake, alikuja na pendekezo hilo miaka kadhaa iliyopita, sasa ivi linatekelezwa vizuri kabisa.

Hivyo usidharau au kuona huna mchango katika kuboresha jambo flani, inaweza isiwe vile ulivyoshauri, lakin ndani ya ushauri wako yakachukuliwa baadhi ya mawazo na kuboreshwa
 
hakuna nchi yoyote duniani ambayo imepinga hatua ya kimaendeleo bila kutoza tozo/kodi.

Watanzania hatuna budi kubadilika, hakuna atakaye ijenga nchi yetu bali ni sisi wenyewe na hakuna misaada ya buree.

Hiyo misaada inayo tolewa kwa nchi pia ni Tozo na kodi za Raia wa nchi za Ulaya/Marekani n.k.

Tulizoea sana vya bureee na matokeo yake tukalemaaa sasa tuache upuuzi, tulipe tozo na Kodi kwa maendeleo yetu.
Nikweli, lakin tozo iendane na kipato cha watu! hii yetu nadhan kuna sehem haiko sawa! watu kufikiria kukwepa bank ujue sio jambo jema!

Kuna haja ya kuboresha namna ya utozaji wa tozo hizo.
 
Back
Top Bottom