Hii video nimetumiwa, jamaa huko mwanza kajirusha alikuwa kwenye daraja la mabatini.
Chanzo inasemekana mambo ya mapenzi. Tukirudi kwenye hiyo video ukiangalia, wakati yuko juu watu wanampita hawana hata habari naye hakuna hata mtu anafanya maamuzi ya kumzuia.
Ukija huko chini napo mijitu imekaa ikimshangaq tu wamemgeuza sinema utafikiri wanangalia tamthiliya zao zile za kituruki.
Mbongo sasa hivi utu, ubinadam umepotea roho mbaya na ukatili unawaingia tu. Ndo maana tunaonaga matukio mengi ya ajali mtu akipata watu wanachofanya kwanza ni kjku record tu msaada hakuna.
hii video nimetumiwa,jamaa huko mwanza kajirusha alikuwa
Kwenye daraja la mabatini
Chanzo inasemekana mambo ya mapenzi
Tukirudi kwenye hiyo video ukiangalia,wakati yuko juu watu wanampita hawana hata habari naye hakuna hata mtu anafanya maamuzi ya kumzuia
Ukija huko chini napo mijitu imekaa ikimshangaq tu wamemgeuza sinema utafikiri wanangalia tamthiliya zao zile za kituruki
Mbongo sahvi utu, ubinadam umepotea roho mbaya na ukatili unawaingia tu
Ndomana tunaonaga matukio mengi ya ajali mtu akipata watu wanachofanya kwanza ni kjku record tu msaada hakuna
Pole sana. Naona umeguswa na kukerwa na Watanzania. Pole.
Walakin, suala hili ni zito na gumu kwa binadamu yeyote yule.
Sasa wewe unadhani kwa kuangalia Video na tukio hilo moja, unaweza kuishutumu Nchi nzima kuwa ni jamii katili na linalopoteza Ubinadamu ni sawa kweli?
Tambua, hakuna aliyeshuku kijana huyo atajirusha na hilo limesemwa na walioshuhudia mkasa/tukio hilo, tena huku wakiwa wanasikitika. Sasa wewe umeenda mbali na kiujumla jumla kuishutumu Nchi Nzima kwa msingi wa tukio hilo moja?
Mrangi, badala ya kutoa lawama ungeomba vyombo husika kuhimiza watu kuwa na ufahamu wakaribu zaidi na wale wa karibu nao kugundua dalili za unyogovu, hilo linaweza kusaidia na kuepusha majanga na matukio kama hayo kwenye Jamii.
Unafikiri ni njia zipi zinaweza kutumiwa kuboresha afya za watu (mental health)kama kijana huyo?
Kama itakupendeza, naomba kuwaombea samahani Watanzania wote kwa yaliyokusibu.
NB: Tujaribu kuepuka na kauli hizo pana, hazileti tija kwa Jamii wala Nchi.
Hapana. Sidhani kama wewe ungekutana na suala kama hilo ungependa ndugu jamaa na marafiki wakuache tu.
Sawa, kila mtu ashinde mechi zake, walakini suala la usongo wa mawazo ni la timu nzima. Jamii, Kijiji, na Nchi yote. Bila hivyo mleta mada asingetuhumu Nchi nzima, ama?
Unashindaje mechi bila ya kuwa na timu? Mayele ameshashinda mechi peke yake? Sidhani.
Kwa maoni yangu, tusaidiane pale panapo hitajika-mfano pale unapogundua ndugu, rafiki, na jamaa wanapitia wakati mgumu.
Ni wazi hakuna aliyekuwa anajua yaliyomfika huyo kijana. Kweli inasikitisha, laiti angetokea huyo mpenzi wake ama ndugu zake waliokuwa na ufahamu wa hali yake ya akili, labda huu uzi usingekuwepo.
Nilivyokuwa darasa la 6 wakati natoka shule nikakuta kuna jamaa anapigwa kipigo moja hevi sana hadi nikaogopa... kuuliza sababu ndo nikaambiwa anaadhibiwa kwa kutaka kujiua.. nikajiuliza mbona sasa kipigo wanachompa ni kama kutaka kumuua tu?
Hata mi nimesikitika sana aisee watu walijuwa kama atajirusha ndo maana wakawa wanashuhudia, angetokea mtu wa kumshika tu asingefanya maauzi yale mbele za watu, vipi alikufa
Uwe unasoma btn the lines!! Nimesema hapo isiwe kipaumbele,sio kwamba isirikodiwe!! Kwenye dharura yoyote kuna vipaumbele,na ndo nilichokizungumzia hapo!!